kiben10
JF-Expert Member
- Apr 28, 2018
- 615
- 792
Leo katika harakati zangu za hapa na pale kutafuta riziki nimeiona hii acha nishee nanyi kama itawapendeza pia.
Daladala la Bagamoyo to Tegeta kondakta yuke kajisahau kunitoza nauli nami nikaamua kuunyuti vizuri tu bila hata ya kumpa nauli yake na nikajifanya kulala kabisaaaa. Sasa chakushangaza kumbe yule kondakta bhana ni jirani yangu nyumba ambayo ninakaa kwa sasa kwa miezi 2 tangu nihamie. Kumbe bhana yule kondakta me ananifaham ila me simfaham. Sasa baada ya kushuka pale Tegeta nashangaa ananiita nikajua anataka kunidai pesa yake kumbe ananipa kipaseli( kimfuko cha mahitaji ya home kwake) na kuniambia samahani mpatie mama (KOKU) pale nyumbani. Looooh nilipatwa na butwaa sana na kusema ama kweli ni vema kwa hizi nyumba tunazohamia( kama wapangaji) ni vizuri mkafahamiana mapema sasa ona hii nilijua nimemvesha dalizi mzee baba kumbe nimejivesha mwenyewe tena mbele ya kupewa mzigo nipeleke kwako.