Natumai mu bukheri wa afya hapo mulipo, nyumba ninayoishi tuko wapangaji watatu, upande wa mbele kuna wadada wawili wamepanga wanashare kulipa kodi, mmojawapo amechumbiwa na tayari harusi ni mwishoni mwa mwezi huu, lakni huyo rafikiye wanoishi wote jana alikuja kuniomba ushauri kwamba afanyeje kwani anampenda sana huyo mume mtarajiwa wa rafiki yake!! kwa ufipi nilimwambia aachane na hayo mawazo akatafute mwingine huyo si wake, baada ya kumwambia hivyo alikasirika na kunitolea maneno yasiyofaa kwamba mimi si mwanamke wa kisasa ninayeenda na wakati!! nilistaajabu sana nikamwambia sawa akaondoka zake......... jamani hiii imekaaje kwa upande wenu kwani mie niliambulia dharau na maneno ya kashfa.