Na kwanini India na England???????
Kwa sababu Shelys ni kampuni ya Wahindi wa Sumaia Group.
Wanaajiri Watanzania Wahindi na Waingereza Wahindi na Wahindi wa India.
Sio kweli kwamba Tanzania hakuna chemists wakufanya kazi Shelys.
Shely's, kama pharmaceutical companies zote Tanzania, wanatengeneza generic drugs. Yaani kopi za madawa ambayo yameshagundulika. Kwa hiyo hawahitaji sana high caliber researchers and technical know-how. Wanafuata written protocols tu.
Hiyo kazi wanaweza kum train chemist yeyote. Hata Marekani ambapo chemist anahitaji skills kali za kufanya kazi kulingana na viwango vya regulation kali za Good Manufacturing Practices (GMP), bado wana train chemistry graduates right out of college kufanya kazi za pharmaceutical production.
Na hata author wa hiyo research paper iliyotundikwa hapa amesema kwamba Sumaia Group wenyewe wamekiri kwamba viwango vyao havifikii viwango vinavyotakiwa kimataifa. Halafu wanatuambiwa Watanzania hatuna chemists wa viwango vyao. Give me a break.
Sumai Group wanakuchukua Wahindi wa India na Wahindi wa Uingereza ili kuwapa ndugu zao vi green card vya kuishi Bongo tu. Wangekuwa kweli wanapungukiwa na local skill wangeenda kukusanya watu Kenya hapo ambapo wasomi wamejaa, badala ya kuingia gharama za kutafuta Wahindi India na Wahindi Uingereza.
Na kile ki research kilichowekwa hapa kuhusu hiyo assertion ya Sumaia group kwamba hakuna skilled workforce Tanzania ni mdosho. Author wa paper , ukisoma paper nzima, hakufuatilia, na mwenyewe kasema hakutembelea hicho kiwanda kuchimbua ukweli. Ila katuwekea sentensi moja ya Uongozi wa Wahindi wa Sumaia Group eti hakuna skilled workforce ya Tanzania.
Huyu researcher wa UNCTAD nae anakubali kuandika nusu ukweli kama sio kashfa za uongo za uongozi wa Sumaia Group sababu tu anajua hakuna atakae mfuata usoni kumswalisha kuhusu report yake mbovu mbovu.
Si kweli Tanzania hakuna chemists wenye uwezo. Si kwa generic drugs production anyway.