Kipindi cha Nyuma Mama yangu Hakuwahi kabisa kupenda niwe na mahusiano au Mazoea na Mwanamke yeyote, alitaka nisome nifikie Malengo yangu...Kwa Hili Niliona Yupo sahihi!.
Basi nikamaliza Mpaka Form six bado Mama akawa Hapendezwi na mimi kuwa na uhusiano wowote japo mzee hata akipata hizo story Hana Noma utamsikia tu bwana kuwa Makini usiharibu Malengo yako.
Kwa ideology hio nikawa nshajenga picha kwamba mama yangu hapendi niwe na uhusiano na wanawake maana utamsikia kwambaa mara wanawake wana siri nyingi usijione unapendwa, wengine ni mashetani wanakuja kwa dizaini hio kukuharibia Malengo.
Sasa Bwana cha Ajabu, Juzi kati watu wa pembeni walimfikishia taarifa kwamba nadate na binti mmoja hivi....kama kawaida nikajua mama atamind (Namheshimu sana mama na sipendi kabisa akwazike).
Mama akaniuliza Mwanangu Nasikia uko na binti fulani (sura yake ikionesha furaha ambayo nahisi hakuitaka niitambue), nikamwambia ndio ni kweli mama (kwa aibu nilimjibu ivo), kwa kawaida nilijua angemind lakini nashangaa mama hakumind akaniambia kuwa makini yule binti si ndo yupo form six? nikamjibu ndio.
Akarudia Sikuambii ummwache mwanamke wako ila kuwa Makini (Jambo ambalo huwa si kawaida kwa mama), sasa after that mama katokea sana kumpenda uyu binti, kidogo nikifanya ujinga ananitania labdaaooh fulani angejua upo hiivii....n.k.
sasa wadau hii imekaaje sometimes nashindwa kuelewa au mama ananichora? maana binti ambae nampenda the most nae anampenda na anaonesha kila dalili angetaman siku moja nimuweke ndani uyu mtoto.
Je nijipe amani au nachorwa? Maana si kawaida ya Mama navomjua.