Hii imekaaje ndugu zangu sana sana wale wanaojali nchi yetu??Ati Waziri anagoma kujiuzulu????Kunani!

kahaluaJr

Member
Apr 6, 2012
44
11
Kwanza kabisa nasikitika sana kusikia kauli za Jakaya Kikwete ati ni upepo tu utapita kwa maana hiyo anawafanya Mawaziri wake watembee kifua mbele.Hii sasa moja kwa moja inadhihirisha kuwa Jakaya Kikwete ndio kiongozi wa Ufisadi nchini pia mpaka hapa ndio tunaamini aliyosema Edward Hossea kuwa Kikwete anawakingia kifua mafisadi wasishitakiwe hii haijatulia kabisa kwa jinsi Kikwete anavyofanya, Kikwete anatakiwa asome alama za nyakati kuwa nchi hii sio yake so wanachoamua wananchi through kwa Wabunge wao waliowachagua ni kwamba moja kwa moja ni sauti ya wananchi.Sasa mtu kama Cril Chami ati anasema wananchi wafanye tathimini waone kama ana makosa then kama wataona kama ana makosa basi atajiuzulu hii kauli ni dhaifu sana,hana hoja kaabisa.
Hapa pia kwa Mkulo kuwa nje ya nchi haimaanishi ati hawezi kuaandika barua ya kujiuzulu,kwani yuko nje ya Dunia kiasi kwamba hawezi kuandika,lazima nae atoke
 
tatizo sio kujiuzulu sababu ni ulaji ndio unawazuia kuachia ngazi unachezea kukaa kwenye STK mpya, viyoyozi na bata.
 
Back
Top Bottom