Hii imekaaje kisheria?

ndandawamalenja

JF-Expert Member
Nov 1, 2012
472
347
Mwaka 1990 tulipomaliza elimu ya msingi jamaa ambaye tumekuwa pamoja tukasoma wote shule ya msingi mkoani Mbeya alihamia Sumbawanga kimaisha na hakuwahi kurudi tena Mbeya. Huko nikawa nasikia ni mkulima vijiji vya mbali kabisa toka mjini. Hatukuonana tena mpaka mwaka huu mwanzoni. Akanipa historia ya maisha yake toka tulivoachana. Iko hivi.

Yeye alikuwa Muslim (Jina tu lakini, kwenye kukua kwetu sijawahi kumuona akienda msikitini wala nini). Mwaka 1994 alioa kwa ndoa ya kikristo (huko kijijini hakukuwa na Uislam kabisa miaka hiyo) akabahatika kupata watoto wawili.

Mwaka 2004 miaka akaenda kutafuta maisha Songea (alipita juu kwa juu hatukuonana). Akakaa huko miaka mingi bila kurudi tena Sumbawanga na hakuwa na mawasiliano kabisa na mke wala watoto aliowaacha huko. Mwaka 2007 akiwa huko Songea akakutana na mwanamke wa kiislam, akafunga nae ndoa ya kiislam. Wakaanza kusongesha maisha kama kawaida, wakabahatika kupata watoto wawili. Huku hatma ya ile ndoa ya kwanza haijulikani.

Mwaka juzi anasema moyo ukamsukuma kurudi Sumbawanga akabahatishe kama atawakuta mke na watoto aliowaachaga kule. AKAWAKUTA. Na mwanamke hajawahi kuolewa wala kuishi na mwanaume mwingine. Akasema alikuwa anamsubiri yeye, nafsi ilikuwa inamwambia atarudi tuu. Wakaendelea na maisha. Na wanawake wote sasa hivi yuko nao. Mmoja alifunga nae ndoa ya kikristo mwingine akafunga nae ya kiislam.

Hii imekaaje kisheria? Ni sawa?
(Najua kidini sio sawa, hasa kikristo)
 
Back
Top Bottom