Mgeni wa Mungu
JF-Expert Member
- Mar 5, 2015
- 1,233
- 1,296
Binadamu tuna majaribio mengi duniani, wakati nimeshamaliza kusoma mwaka 2000 kisiwani Pemba nilipata ajira ya kusimamia Guest house nikawa kama manager kipindi icho wageni walikua wengi na wengi walikua wazungu. Ilikua sa1 jioni niliwapokea wageni 2 wazungu walikua ni wale waliomiliki boti iliyokua inaitwa Sepideh. Hawa wageni niliwapokea nikawapa room nikaendelea na kazi zangu. Kwa mshangao mkubwa niliingia chumbani kwao nikakuta begi ya pesa iliokua wazi na dola zilizokua zimejaa mpaka juu kama picha inavoonekana. Kwa kweli nilishangaa sikuweza kuamini kama ni pesa za kweli au ni mtego. Wakati huo chumbani walikua hawamo wako chumba cha pili wanakunywa pombe. Nilijaribu kuzichezea noti za vibulungutu vya 100 vilivokua vimejaa. Kilichofata nikatoka ndani na kufunga mlango kazi iliyobaki nikawa nimeamua kuzilinda mpaka wamalize warudi chumbani kwao. Majaribu ni meng niliwaza sana lakini sikupata jibu sijui kama ni wewe ungefanyaje?