Aventus
JF-Expert Member
- Mar 8, 2013
- 2,011
- 2,165
..., nchi hii wakati mwingine 'unafiki' na 'ushabiki' unatumaliza haswaa sisi vijana tena wengine ni wenye uelewa na utambuzi.., Wakati mwingine kwa sababu tu ya ushabiki tunatetea hata uovu.,
..., nakubaliana na wale wanaosema njaa haina mahusiano na Rais aliyepo madarakani.., maana hili janga ni la kitaifa.., lakini sikubaliana na kauli ya Rais kwamba kila mtu kubeba mzigo wake.., (hawezi kukwepa mzigo huu, maana ndiye sasa aliyepo madarakani.., hili kombe asimtupie mtu mwingine)..
Kazi ya serikali ni kusaidia wananchi wake kukabiliana na majanga na hasa hili la njaa na ndiyo maana kuna wakala wa hifadhi ya taifa ya chakula (NFRA).., Hali ya ukame kwa maeneo mengi ni kubwa sana.., Kwa sasa debe la mahindi ni katika maeneo mbali-mbali ni Tsh 25,000/- hadi Tsh 35,000/-, unategemea familia ngapi zinaweza kumudu hizo gharama kwa wakati wote huu wa ukame na Kukosekana kwa chakula!?
Na mahindi kupatikana ni shida pia katika maeneo yote nchini.., Tusihitaji majibu mepesi kwa maswali magumu.., Hili ni jukumu la serikali na hakuna namna ya kuweza kukwepa hili wajibiko.., Wananchi wako radhi kulima lakini hali ya hewa siyo rafiki.., Maeneo mengi ni kame hakuna mito hiyo ya umwagiliaji, zana za kilimo na pembejeo ni ghali sana.., Hali inavyokwenda watu watakufa njaa..,
.., Rais anasema serikali haina shamba (watu wanashangilia) hawaulizi yale maghala zaidi ya 31 ya NFRA yana kazi gani.., soon watu watakufa njaa.., kuna ukame mkubwa sana katika maeneo yetu...., wakuu wa wilaya wanakatazwa kutoa taarifa za hali ya njaa.., waandishi wakitoa taarifa hizo wanakamatwa na kusekwaa ndani..,
Kitu kingine.., mawaziri na watendaji wa serikali wamekuwa na unafiki haswaa, sijui wanataka kumfurahisha mwajiri wao au vipi..., oktoba mwaka jana (2015) kwa mujibu wa MER (monthly Economic Review) ya BOT, akiba ya chakula ilikuwa zaidi ya tani 230,000.., kwa sasa, ukisoma MER za BOT, utaona mwaka huu 2016/17 kwa wastani unavunja record ya zaidi ya miaka 10 kwa akiba ya chakula kwa kila mwezi kwa maana ya ulinganisho na miaka hiyo, kwa akiba kuwa ya chini sana!
Haiwezekani nchi yenye njaa na ukame kila mahali.., kipaumbele kikafanywa kuwa ni viwanda.., halafu wakati huo kilimo siyo moja kati ya vipaumbele hivyo vya serikali kwa miaka 5.., halafu Rais anasema kila mtu aubebe mzigo wake.., haijawahi kutokea kauli kama hii kwa mkuu wa nchi...., tangu nimefahamu nini maana ya utawala na uongozi.., watu waubebe mzigo wao wenyewe!? Wakati walikuchagua wewe uwe msaada wao kwenye njia hiyo!?
Tuache unafiki.., tuitake hii serikali sasa iwajibike kwa wananchi wake.., siyo kukwepa wajibu wake kwa maneno rahisi na mepesi hivi..,
NB; JPM km anayaishi maneno yake; amwondoe mkuu wa mkoa wa Mara na mikoa yote yenye njaa.., (maana alitoa ahadi ya kuwatumbua wote wakuu wa wilaya na mikoa ambao watatangaza njaa katika mikoa yao)
Martin Maranja Masese (MMM)