Hii habari ya uuzwaji wa NBC imenisikitisha sana, naamini itamsikitisha kila mzalendo wa nchi hii

Dah haya bana Tanzania yetu

Kuhusu Africa inabidi Mungu mwenyewe aingilie kati, maana elimu imeshindwa kumkomboa mwafrika.
Haiwezekani zaidi ya miaka 50 tunajaribu halafu tunarudi pale pale mwanzo wa safari.
Haiwezekani kabisaa, hapa hatalaumiwa mzungu kwa lolote.
 
kwa wale ambao hawakupata nafasi jisomeeni hii habari, ni ndefu lakini ni vizuri ukajisomea mwenyewe kuliko kusubiri kuja kuhadithiwa.

aliyekuwa Katibu Myeka wa Mwalimu, Samwel Kassori, ilibainisha namna Mwalimu alivyohuzunishwa na suala la kuuzwa kwa NBC kwa mojawapo ya makampuni kutoka nchini Afrika Kusini.

"Lakini moja kubwa ninalokumbuka ni kuhusu mchakato wa uuzwaji wa benki ya NBC mwaka 1997 mwezi Aprili wakati wa utawala Mkapa ambapo Mwalimu aliwahi kulengwalengwa na machozi akipinga benki hiyo kuuzwa kwa ABSA Group kutoka Afrika ya Kusini.

"Wakati huo nakumbuka serikali ilipanga kumwandalia Mwalimu sherehe ya kitaifa ya siku yake ya kuzaliwa (birthday) ya kutimiza miaka 75 ambazo zingefanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee wa Jijini Dar es Salaam, na jambo hilo lilimshtua kidogo akaniagiza nichunguze fedha hizo zingetoka wapi na kwanini afanyiwe sherehe kubwa kiasi hicho na pia tetesi zilikuwa zimezagaa kuwa NBC inauzwa.

"Wakati huo Waziri wa Fedha alikuwa Daniel Yona, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo alikuwa Peter Ngumbulu na Gavana wa Benki Kuu (BoT) alikuwa Dk. Idris Rashid.

"Baada ya kupata taarifa za kwamba benki hiyo iko mbioni kupigwa bei, Mwalimu aliomba maelezo kutoka kwa wahusika ambao ni Waziri wa Fedha, Katibu Mkuu na Gavana wa BoT.

"Majibu ya serikali yalikuwa kwamba NBC inauzwa kwa sababu taasisi za fedha za Kimataifa za Fedha (IMF) na Benki ya Dunia (WB) ziliagiza Benki hiyo kuuzwa.

"Baada ya kupata maelezo hayo Mwalimu alikasirika kweli kweli, akaniita na tukiwa nyumbani kwake Msasani aliniagiza kumpigia simu Rais wa (WB) wakati ili azungume naye.

"Baada ya kumpata Rais huyo wa (WB) ambaye bado alikuwa akimwita Mwalimu Mr. President (Mheshimiwa Rais), alikana IFM pamoja na Benki ya Dunia kushinikiza au kutoa masharti kuuzwa kwa NBC.

"Namnukuu Rais huyo wa WB aliniambia:"Mr Kasori do me a favour could you request President Nyerere to come to our headquarters in Washington and read the documents from Tanzania government, they are too voluminous but will try to make executive summary of the same"

"Maana yake ni kwamba walitaka Mwalimu akajioonee mwenyewe nyaraka zilizotumwa katika taasisi hizo za kimataifa kuhusu uuzaji wa NBC na walisema wangelipa gharama zote muhimu za safari hiyo.

"Baada ya mazungumzo ya simu siku mbili baadaye tulifunga safari na Mwalimu hadi Washington nchini Marekani ambapo tulikutana na Rais wa WB kwa kikao cha siku nzima na kupitia nyaraka muhimu zilizowasilishwa kwao na serikali ya Tanzania.

"Tulirudi nyumbani baada ya wiki moja na Mwalimu aliniagiza kwanza niwatafute Yona, Ngumbulu na Dk. Rashid ili azungumze nao kabla ya kukutana na Rais Mkapa.

"Basi baada ya mimi kufanya mawasiliano nao wote hakuna aliyeitikia wito wa Mwalimu "walimpuuza" na badala yake walimtuma Donald Kamori ambaye alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC.

"Nakumbuka vizuri kikao na Kamori kilifanyika Msasani nyumbani kwa Mwalimu Nyerere, Aprili 13 mwaka huo 1997, na Kamori alikuwa mtaalamu aliyebobea katika masuala ya fedha na ndiye kati ya wataalamu wazawa walioanzisha BoT.

"Kamori akiwa na nyaraka na takwimu za kitaalamu. Alimweleza Mwalimu bila ya kuficha kuwa kuiuza NBC serikali ilikuwa inafanya makosa makubwa katika sekta ya fedha kwa kuwa Benki hiyo ilikuwa inaendeshwa kwa faida kubwa. Uuzwaji wake ungeleta athari ya moja kwa serikali pamoja na taasisi zake nyeti.

"Mwalimu alitikisa kichwa kwa masikitiko makubwa, akasema &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];ooooh kweli nimesomesha Watanzania' alikuwa amevutiwa sana na maelezo ya kitaalamu ya Donald Kamori.

"Baada ya kupata maelezo ya kutosha kutoka kwa Kamori, Mwalimu aliomba kukutana na Rais Mkapa na kikao kilifanyika Ikulu ambapo alitetea NBC isiuzwe kwani ndiyo ilikuwa nguzo ya serikali hasa wakati inapoishiwa fedha katika mambo "nyeti yanayohusiana na usalama wa nchi" ilikuwa inakopa fedha NBC.

"Majadiliano na Mkapa yalichukua muda mrefu sana kuhusu suala hilo na itoshe kusema kwamba baada ya majadiliano hayo marefu likazaliwa wazo la kugawanywa kwa hiyo na kuanzishwa kwa Benki ya NMB ambayo serikali ina hisa hadi leo.

"Kilichomsikitisha zaidi Mwalimu ni kwamba baada ya juhudi zote hizo Kamori alifukuzwa kazi kama Mkurugenzi Mtendaji wa NBC na kurudishwa BoT bila kupangiwa kazi yoyote.Hakuwa na ofisi pale akifika anasoma magazeti aliyojinunulia na kurudi zake nyumbani.

"Alitishwa sana na kuhojiwa ni kwanini alikwenda kumweleza Mwalimu na kumwonyesha nyaraka za uuzwaji wa NBC kwa Benki ya ABSA ya Afrika ya Kusini?

"Kamori alinipigia simu akanieleza masahibu yaliyomkuta na mimi nikaufikisha ujumbe wake kwa Mwalimu, baada ujumbe huo Mwalimu alisikitika sana, akahoji ni kwanini wanafanya mambo hayo "kumfedhehesha" akiwa hai?

"Huyo Kamori alikuwa mzalendo kweli kweli ni kati ya Watanzania walioipenda nchi yao. Siku hiyo hiyo aliacha kazi akasema hawezi kupokea mshahara asioufanyia kazi na akaenda kufanya kazi zake sijui kwa sasa atakuwa wapi.

"Sakata la kuuzwa kwa NBC kwa kweli ni kati ya mambo yaliyowahi kumchanganya akili Mwalimu na kwa upande wangu uuzwaji wa benki ile ulifungua milango ya ufisadi mwingine uliokuja kufanyika miaka ya baadaye," alisema.

Inasikitisha sana, uzalendo umekimbilia wapi!!!!
 
Huu ndiyo utawala tuliokuwa nao na ndiyo uliyotufikisha hapa tulipo. Watu walikuwa tayari kutumia jina la Mwalimu kujipatia uongozi, ati wana CCM. CCM ilichukiwa sana na Watanzania wengi kwaajiri ya uongozi mbaya wa dhuruma especially wakati wa Kikwete. Rais Magufuli maeirudishia CCM heshima yake, na asingekuwa Rais Magufuli CCM ingezikwa. CCM Mwalimu aliyoiacha ilitekwa na watu wachache ambao walikuwa wakijiita watoto wa CCM wakati huo huyo baba wa CCM walimudharau baada ya kupata madaraka. Mungu mkubwa, kutuletea Rais Magufuli. Rais Magufuli kumufuta machozi baba wa taifa ambaye kwa sasa hatuko naye ni kumutafuta Kamori kama yuko hai amjulie khari yake, na kama hana kazi basi ni mtu anayefaa kusaidiwa kwa kila njia. Rais Magufuli, ajitahidi tu makaburi anayoyaogopa kuyafukua, ayafukuwe tu, Watanzania wapenda haki watamusaidia kuyafukia baada ya kuyapekuwa. Story hii itamutia uchungu kila Mtanzania mpenda haki. Rais Mkapa dharau aliyomuonyesha Rais Nyerere baba wa Taifa, janga litamukuta akiwa hapa hapa duniani. Unachopanda ndicho uvunacho.
 
Unauhakika unayosema?

Mtu unaweza kufa kwa majonzi. Ukiwa na majonzi mengi kutokana na dharahu kutoka kwa watu uliowaamini, unashikwa na hasira, unakosa raha, immune yako inashuka na maradhi kama cancer yanakushambulia. Ndiyo vitendo vya dharau kama hivi inawezekana vilimuletea Mwalimu majonzi makubwa na immune yake ikashuka na kupata maradhi. Sasa huu sio uuwaji?
 
Inasikitisha sana, uzalendo umekimbilia wapi!!!!

Tulikuwa hatuna uwongozi wa kweli, wala uzalendo wa kweli, mawazo yalikuwa ni pesa tu. Nani atavuna kwenye shamba la bibi zaidi ya mwingine. Binaadam ni hatari kushinda nyoka.
 
Unauza Benki yenye Majengo na Mali zingine nchi nzima, Rasilimali watu, ina wadai watu/kampuni mabilioni kwa bilioni 16 na benki ilikuwa inatengeneza FAIDA, hivi hawa viongozi wetu kweli huwa wanaamu mambo kwa maslahi ya mwananchi? Tunaona hata viongozi wanasaini mikataba Miiiiiingi wanasema ni kwa ajili ya Nchi (Wananchi) lakini mikataba hiyohiyo tunaambiwa ni SIRI

Kila mkataba ni siri utazani Tanzania ilikuwa yao peke yao. Sasa siri hizo tutazisoma pole pole wakati watoto waliojiita wamekulia CCM kujulikana hata mwenye kuanzisha hiyo CCM hawakumuheshimu bali walikuwa wakitumia jina lake tu. Story hii itamushushia Mkapa heshipa kwa Watanzania wengi wapenda haki. Dhuruma walizofanya Marais waliopita kwa Watanzania hazisemeki ni Mungu tu anajuwa.
 
Makampuni mengi,na mashirika ya umma,yalikuwa yanajiendesha kwa hasara tupu,mwisho wa mwezi,yanaomba fedha kutoka hazina kwa ajiri ya kulipa mishahara.
Usimamizi ulikuwa mbovu sana,waliopewa wayasimamie,waliishia kuajiri ndugu,na wizi,
Hata ATCL,hii ya Leo,ilikuwa imefika sehemu,watu wanaenda ofcn kusoma magazeti,harafu mwisho wa mwezi wanataka mishahara,
Mkapa licha ya kuunda TRA,Tasaf,Tanroads,
Alituingiza chaka kwa kununua rada ilimradi kampuni ya UK isifirisike,sie tukabeba Mzigo,sie tuumie,wazungu wasikose ajira!!!
Tanesco ilikuwa imejaa majizi,yeye akavuruga kabisa,akaleta management ya nje,
Kwa ujumla madhambi alitotufanyia,ilibidi afie jela
 
Back
Top Bottom