Hiari inapogeuka lazima! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hiari inapogeuka lazima!

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Daison, May 21, 2011.

 1. D

  Daison New Member

  #1
  May 21, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NAKUMBUKA WAKATI NAANZA DARASA LA KWANZA MNAMO MWAKA 1993 ADA YA SHULE ILIKUWA NI SHILINGI 200/- KWA SHULE ZA MISINGI.

  NAKUMBUKA ILIKUWA MZAZI AKISHATOA HIYO MIA MBILI BASI ILIKUWA MPAKA MWAKA UISHE NDIO MZAZI ATOE TENA HIYO MIA MBLI TENA. NAKUMBUKA HAPAKUWA NA KERO ZA MARA LEO MCHANGO WA MADAWATI MARA MLINZI MARA EK NA VIKOLOMBWEZO VINGINE VINGI KAMA NINAVYOVIONA SIKU HIZI

  BALAA LIMEANZIA PALE SERIKAKLI ILIPOSITISHA ADA KWA SHULE ZA MISINGI
  MPAKA INAFIKIA WAKATI NAJIULIZA HIVI INAMAANA KUMBE ADA ILIKUWA DILI KWA WAALIMU WAKUU? MAANA NAHISI WAKATI SERIKALI INATANGAZA KUTOLEWA BURE KWA ELIMU YA MSINGI NI KAMA ILIKUWA INATANGAZA KUPANDA KWA GHARAMA ZA ELIMU YA MSINGI

  MAANA NAAMIN PALE INAPOFIKA MWISHO WA MWAKA INAPOFIKA MSIMU WA KUWAANDIKISHA WATOTO WA DARASA LA KWANZA HUWA NI KIPINDI CHA NEEMA KWA WAALIMU WAKUU
  SASA ACHA KUANDIKISHA HATA KUMHAMISHIA MTOTO KATIKA SHULE { Ikumbukwe hapa nazungumzia shule za misingi za dar es salaam} SASA HAPO NDIPO UTAKAPOJUTA

  UKIENDA KUMTAFUTIA MWANAO NAFASI KATIKA SHULE UTAAMBIWA TOA 50,000/- BILA HIVYO HUPATI NAFASI HAO NI WAALIMU WAKUU WA DAR
  SASA KASHESHE IPO KWA WAALIMU WA MADARASA! MWALIMU WA DARASA ANAANZISHA TUITION AMBAYO AWALI INATANGAZWA KAMA HIARI KWAMBA HII ITAFANYIKA PALE TU MWANAFUNZI ANAPOKUWA NA PESA YAANI MIA MBILI
  LAKINI SASA HIARI HIYO INAGEUKA KUWA LAZIMA PALE WANAFUNZI WANAPOINGIA DARASANI MWALIMU ANAKUSANYA MIA MBILI ZAKE NA KAMA HUNA BASI HUINGII DARASANI
  YAANI UNAKUTANA NA MTOTO MTAANI UKIULIZA KULIKONI UNAAMBIWA NIMERUDISHWA KWA SABABU YA PESA YA TUITION!!

  TUNAIOMBA SERIKALI ITUONDOLEE HUU WIZI UNAOFANYWA NA WAALIMU WA DAR
  TUNAFAHAMU HII YOTE INATOKANA NA TAMAA KILA MTU ANATAKA KUENDESHA GARI LAKE
  NYUMBA YAKE NA HATA MILIONI KADHAA KWENYE AKAUNTI YAKE

  UHAURI WANGU KWA WAALIMU WENYE TABIA HIZO
  MAISHA NI SAFARI NDEFU SANA USIJE KUJIHARIBIA MAISHA KWA TAMAA
  FIKIRIA LABDA UNA MIAKA 3 KATIKA AJIRA UNATAKA KUMILIKI GARI HUYO MZEE WAKO ULIEONA MAFANIKIO YAKE HATA UKATAMANI KAZI YA UALIMU ANA MIAKA 25 KATIKA AJIRA! WEWE MWENYEWE HUONI TOFAUTI? FANYA KAZI KWA UADILIFU UTAFANIKIWA.
  MAFANIKIO NI NDOTO YA KILA MMOJA WETU LAKINI WENGI WETU HUWA TUNAZIHARIBU NDOTO ZETU KUTOKANA NA TAMAA
   
Loading...