SI KWELI Hi hotuba ni ya Traore kweli?

SI KWELI Hi hotuba ni ya Traore kweli?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Wakuu, Je hotuba hii ni ya kweli?
1759562948915.png

 
Tunachokijua
Captain Ibrahim TRAORÉ ni Rais wa kijeshi chini Burkina Faso aliyefanya mapinduzi ya kumtoa Rais wa wa mpito wa wakati huo ambaye alikuwa ni mwanajeshi pia Paul-Henri Sandaogo Damiba September 2022. Aidha Captain Ibrahim anatajwa kuwa miongoni mwa marais wenye umri mdogo zaidi barani Afrika na duniani.

Madai

Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kwa nyakati tofauti imesambaa video ikimuonesha Rais wa kijeshi wa Burkin Faso, Ibrahim Traore akitoa hotuba iliyobeba masuala mbalimbali ikiwemo kuwasema viongozi wa mataifa ya Magharibi.

Uhalisia wa hotuba hiyo

JamiiChek imefuatilia na kujiridhisha kuwa hotuba hiyo si halisi.

Ufuatiliaji kupitia nyenzo za kidigitali umebaini kuwa video hiyo iliyobeba hotuba ya Rais huyo imetengenezwa kwa Teknolojia ya Akili Unde (AI). Video hiyo imetengenezwa kutoka katika moja ya vipande vya video halisi na kisha kuingiziwa maneno kwa kutumia teknolojia ya AI.

Aidha ufuatiliaji zaidi kupitia keyword search hakuna majibu yanayopatikana kuashiria kuwa Rais Traore alishawahi kuzungumza ama kutoa hotuba yenye maneno hayo ambapo pia si rahisi kutolewa na kiongozi wa nchi.

Hata hivyo Traore katika kotuba zake nyingi amekuwa akitumia lugha za asili za mataifa yao kuliko kiingereza kama inavyoonekana katika video hiyo.
VIongozi wa aina hii wanachoweza ni kuongea ongea mambo ambayo hawana uwezo wa kuyatekeleza. Hopeless kabisa
 
Back
Top Bottom