Hey DJ- Sister P

Hey DJ- Sister P

NGAYANIMO

Member
Joined
Feb 17, 2026
Posts
39
Reaction score
55
1775222645235.jpg
1775222634324.jpg
1775222658491.jpg
UGOMVI WA SISTER P & ZAY B

"Tangu zamani nilikuwa naficha lakini leo itabidi niseme ukweli, Mimi na Zay B hazijawahi kuiva, haziivi na haziji kuiva yaani yule mtoto hapana hatuendani, na yeye Zay B ndio hataki kunisikia kabisa"

"Ugumu wa kufanya kazi ukiwa mwanamke kwenye game umezidi tofauti na zamani, watoto wa siku hizi wanatoka kwa ugumu mpaka utoe hongo na kama unavojua kuna hongo kwa hiyo kama binti ana msimamo wake anakosa msaada, zamani ilikua rahisi" - Msanii Sister P

FEMALE RAPPER SISTER P ALBUM..MAREKEBISHO.

SISTER P .

Kasi tulikuwa nayo sisi enzi zile, sasa hivi hakuna anayekuja kwa kasi, huyu (Chemical) anajitahidi kasi sio mchezo bado mapengo yetu yapo makubwa sana sasa hivi fake wengi sana, umarekani mwingi mbwembwe mpaka wanaharibu,” alisema.

“Siwezi kuwataja lakini nikisema fake kila mtu anajua, zamani ilikuwa game la muziki sasa hivi ni game la kibiasharam” aliongeza

TRACK LIST SIDE A AND B.. ( ALBUM MAREKEBISHO).

SIDE A

1. sister p ft ally choki & mkweli - achana nao.
2. Sister p - dj
3. Sister p ft wandago - ndani ya ulingo.
4. Sister p -

anakuja.

Side B.

1. Sister p ft Dataz - Marekebisho
2. Sister p ft lil taqwa - sisi tulivyo
3. Sister p ft focus & thomas - ndani ya MATESO
4. Sister p ft farida - maisha ya uswahilini

Katika Hii Album tack zifuatavyo ndio napenda mara zote kusikiliza .

1. Achana nao
2. Djs
3. Anakuja.

Lakini ukiachana na hizo nyimbo pia zipo zingine ngoma pia huwa nasikiliza kutoka KWA rapa sister p ama ulikipenda muite " snapper"

1. Kivyevyetu
2. Twende Club
3. Nani mkali.

Nyimbo ya " Hey Dj" ni Nyimbo ya msanii Ama Female Raper kutoka Hapa Hapa Bongo anaitwa Sister P leo nimeamua niwaletee Uchumbuzi wa kile alichokiimba msanii huyu wa kike katika wimbo wake unaoitwa " Hy dj " uliokuwa unapatikana katika Album yake ya " Marekebisho" nyimbo no.2 side A. Katika Album hiyo ya " Marekebisho" iliyotoka Miaka 2000 ..

Naanza uchumbuzi Wangu katika Ubeti Ama Verse no. 1 Raper Sister anaanza kwa kusema
"
"Nawashuku Ma - dj Wote Ndani Ya Bongo/
Kwa kupiga Track Zetu kisha Nasi Tuna Make Bingo/

Hapa juu 👆👆👆👆 Anatoa Shukurani kwa Djs waliocheza kazi zake Enzi hizo wakati ndo kwanza anaanza Game akiwa Under Ground ..

Wenye Roho za Korosho Twawalia Mingo/
Machizi Wangu Wote Mnaelewa Hii Hali/
Kwamba Mimi sitishiki Haka ukishika Kisu kikali/

Kisha hapo 👆👆👆👆 anatema shiti kwa wale wasanii na mashabiki wenye Roho mbaya ama wasiopenda mafanikio yake ndani ya Game ya Bongo fleva.

Ninapopata 🚬 🚭 Nabaki Natafakari/
Mistari Ishirini Ipo kichwani Me Sijali/
Siku Ta kukutana na Khalifani , Track ya Kwanza ilikuwa kali/
Sasa nije Kwa Hasira kama Vile jabari/
Au Nije kakamavu kama Vile jemedari/
Kutwa Vishindo Vikuu Na Sauti za Ukali/
Ili waelewe "BONGO RECORD" ni label Yenye Nembo Kali/

Hapo juu anaendele anasema akitumia Singara kubwa " anapata mzuka akipewa kipaza nyakati za kuingiza vocal studio na anajivunia kwamba kwa mara ya kwanza alipokutana na khalifani a.k.a P funk Majani aliweza kufanya hit song moja matata sana pale kwenye za " studio za Bongo Record"


Na kuendelea kuisifia kuwa Record label ya Bongo Record ni Bora kuliko Recording lebel zingine hapa Bongo Enzi hizo, kwa Maana Recording label ya Bongo Record chini ya Mtu mzima P funk majani ndio Record label iliyomleta kwenye ulimwengu wa Burudani hadi kufikia kujulikana na Watu Enzi hizo...

Hapa naongeza kitu maana kuna Diss Song ilitolewa na Crew ya Walugaluga clean kupitia Ngoma yao inaitwa " ingekuwa Soo" kwenye Tungo zao walisikika wakisema.

" Bila majani watu fulani Fulani Tusingewasikia Hewani"


Huu mstari ulikuwa maalumu kwaajili ya Sister P " Walugaluga clean" waliingia katika Beef hili ama Diss Track hizi kwa Sababu ya kumsaidia msanii ama wanachama mwezao Zay b kwa maana alikuwa mwanachama wa " Walume ndago family " Crew Ama Muungano wa Wasanii kwa nyakati zile na wasanii wengi katika Muungano huo walikuwa ni wasanii kutoka Wilaya Temeke na Wengi wao walikuwa ni jinsia ya Kiume ..

Na ndio Maana Sister P katika Wimbo wake wa " Achana Nao"

Nafungua ubongo natoa fikra za utumwa kichwani/
kipawa cha toka Kwa mola na wala sija tumia ubani/
Sister p kupata chart watu wanadhani langu utani/
Rap biashara bwana ila angalia usipate Hasara/

Kuuza vitumbua ,pipi & maandazi zote biashara/
Usi dharau hizo biashara watu wataku Angushia msala/
wasomi wengi wamesoma kwa kutumia hizo biashara/
Mashairi sibahatishi na nitauza nyingi nakala/
na sio utani nyota kwangu imeonakana biashara/
Wandago ni rafiki zangu tena wa kina wewe uliza maswali mengi majibu mi sina/
Nakupa Rap shule mashairi yangu yana vina....

Hii verse inapatikana katika wimbo wa sister p akiwa na msanii wa muziki aina ya dansi Ally choki a.k.a mzee wa farasi Pamoja na Raper Marehem Mad brain.

Ni sehemu pia ya maishairi yalikuwa ni kama majibu kutoka kwa Raper sister p kwa msanii Mwana fa kwa kile kilichoonekana kwenye jamii kupitia ngoma yake inaitwa " ingekuwa vipi" akiwa na jay moe project iliyofanyika " mawingu studio" kwa producer Bonnie luv
Kama diss track kwa baadhi ya wasanii hasa wasanii kutoka mtaa wa Temeke. Ambao walifahamika zaidi kama " koo la walume ndago "

Walume ndago ilikuwa ni muunganiko wa makundi mbalimbali muziki Enzi hizo pamoja na wasanii ambao walifanya muziki kama solo Artist nje makundi..

Baadhi ya makundi yaliounda koo hii ya walume ndago ni pamoja na

• Wachuja nafaka
▪︎ gangwe mobb
• wandago family

Lakini kubwa zaidi ni pamoja na msanii sister p nae alikuwa ni sehemu ya wasanii waliounda koo hii ingawa alikuwa akai temeke enzi hizo..

Tafsiri halisi ya neno walume ndago ni Aina fulani ya majani ambayo yanavumilia sana shabani nakuwa kikwazo kwa mkulima katika uzalishaji wa mazao kwa mkulima huyo shabani , kwa kifupi ni mavumilivu hayafi ovyo ama kiurahisi. Yalikuwa yanaitwa ama yalifahamika kwa jina la " ndago"

Kwahiyo chanzo cha neno " walume ndago ndio hiyo.
Wasanii wengi wa Temeke walipenda kutumia jina hilo kwa sababu ya ugumu wa maisha ama mazingira wanaoishi temeke lakini hakikuwa kikwazo kwao cha kuwafanya washindwe kuendelea kuishi temeke , kama ilivyo kuwa ngumu kwa majani aina ndago kufa shabani.

Mwana fa na jay moe katika ngoma ya ingekuwa vip wanasikika wakisema.

Mwanafalsafa: Ingekuwa vipi, maisha ya Temeke yangekuwa juu kidogo?
Unadhani wasanii wangejiita walume ndago?

Jay moe : Ingekuwa vipi Bongo Records isingekuwa ya Halfani?
Watu kama flani-flani tusingewasikia hewani!

Tasfri yake je? Maisha ya temeke yangekuwa ya kishua wao kama wasanii wangejiita " walu ndago"

Ndio sister p nae akamjibu fa kwa kusema. ( achana nao)

Wandago ni rafiki zangu tena wa kina wewe uliza maswali mengi majibu mi sina/

Nakupa Rap shule mashairi yangu yana vina....

Tunaendelea tulipoishia diss track za sister p kuhusu ngoma ya mwana fa na jay moe " ingekuwa vipi.?

Leo tunakutana na clew ya " walugaluga crew " na ngoma yao inaitwa "ingekuwa soo"
Unaweza kuona kama majina hapa idea zinafanana twende kwenye maada..

Sehemu ya majibu ya Walugaluga clane
Kwa mwana Fa & jay moe ngoma inaitwa "ingekuwa soo" bila kusahau kuwa diss " wadango family & sister P..

Katika Verse ..1 Walugaluga clane watoa puch Ryhems zenye mashairi ya vijembe kwenda kwenye Crew ya wandago family. .

"Angekuwepo hai D rob/ na kaka Ramson angekuwa Bongo/ Y Thang bila kidato namrudisha K single/ kwanza ingekuwa mfano kwa ma mc wa Bongo/ na vibaka kama wadango kwenye mfuniko kwenye Udongo..

Hapa walugaluga clane wanadai " kwanza ingekuwa mfano kwa ma mc wa Bongo/ na vibaka kama wadango kwenye mfuniko kwenye Udongo..

Wana maanisha wadango family ni wezi wa idea wameiba idea ya mwana Fa na jay moe kupitia wimbo wao wa " ingekuwa vipi" na wandago family wao wakatoa nyimbo inaitwa " ingekuwa poa"

Originally version ya mwana fa & jay moe ilikuwa inasema hivi Verse..1 ( ingekuwa vipi)

Ingekuwa vipi angekuwa hai D-Rob?
Na Chief Ramso angekuwa Bongo?
Wahisani bila kidato?
Na umrudishe K-Single?

Kwanza ingekuwa mfano?
Au tayari ingekuwa chongo?
Kati ya nani angekuwa uigo?
Na nani angebaki mzigo?
Lakini pia vile vile wana toa diss kwa jay moe mara hii Walugaluga clane wanasimama ama wana mtetea Dully sykes kwa kile alichokisema Jay moe na mwana Fa katika wimbo wao unaitwa " ingekuwa vipi"

Verse ya mwana fa & jay moe hii hapa inasema..

"Mwanafalsafa: Ingekuwa vipi Dully Sykes angeimba Hardcore?
Mashairi kama Jay Mo?

Neno wanasesere n'na imani lisingekuwepo.
Mauzo ya Rap ya bongo yangefika Platinum tano

Jay moe : Mauzo ya rap ya bongo yangefika Platinum tano!

Walugaluga clane nao wakawa jibu mwana fa na jay moe kwa kusema..

"Ingekuwa poa Dully sykes angeimba Hard core/ mashairi kama jay moe hapana..?/ jay moe wanasesere na ndio maana ameimba bishoo/ we Bishoo tu / jamani hi ni nyimbo tu tusije tuona Roho.

Lakini Walugaluga clane hao hao waka engemea upande wa "wandago family " Crew ambayo ilikuwa ni sehemu ya makundi yanayounda koo ya "walumedago " na walikuwa wanaishi temeke .

Walugaluga clane wanasema..

"Ingekuwa soo maisha ya temeke yangekuwa juu kidogo/ unadhani wasanii wangejiita ma bishoo kama jay moe"

Hii verse ilitokana na kipande hiki cha mwana fa na jay moe.

Ingekuwa vipi, maisha ya Temeke yangekuwa juu kidogo?
Unadhani wasanii wangejiita walume ndago?

Jay moe : Ingekuwa vipi Bongo Records isingekuwa ya Halfani?
Watu kama flani-flani tusingewasikia hewani!

Lakini pia walugaluga clane wanaendelea kumdiss sister P na kumpa shavu zay b kuwa yenye ni. Bora kuliko sister P.

Ingekuwa soo Bongo Record nisengekuwa ya Khalifan /
mtu kama sister P tusingemsikia Hewani/
lakini nature na solo tulisha wasikia zamani /

Ingekuwa so kwa sister p angeendelea kumkela zay B/
kwani zay b ni dio Danger ukiendelea kumchezea atakujicha

Hii ni diss kwa sister p coz P funk majani aliimpa fursa kubwa sana sister P katika studio yake ya Bongo Record.

Kwahiyo walugaluga clane walikuwa wana amini bila msaada wa P funk majani wa kurekodi nyimbo Bongo Record msanii ama Raper sister P sio lolote sio chochote in short alionekana kama sio msanii mwenye level kubwa zaidi ya zay b enzi hizo .

Mwana fa aliimba : "Angeimba nini Sister P asingekuwepo Zay B ? Akilenga kum-diss rapa sister P aliyekuwa na bifu na rapa mwenzie Zay B.

Hapa ndipo Sister P alipoingia studio haraka, kumjibu Mwana FA juu ya wimbo wake huo wa "Ingekuwa vipi" hususan katika kipengele alichom-diss moja kwa moja.

Katika wimbo huo uitwao "Hey Dj", Sister P anaimba kumwambia Mwana FA.. "Pumbavu eti unauliza, ningeimba nini Sister P asingekuwepo Zay B ... Malumbano nimeshaacha mi naelimisha jamii."

Sister P, haishii hapo tu, anaendelea kumchana Mwana FA kwa kusema.. "Ungeimba nini Mwana FA wasingekuwepo wasanii....au tumuite Fredo Starr kwa wimbo wake uliouitafsiri ?"

Maelezo hayo ya Sister P yaliwashtua wadau wengi na kuwafanya kuanza kufuatilia kwa kina, juu ya tuhuma za Mwana FA kuiba 'idea' ya wimbo wa Fredo Starr uitwao "What if"

What if history was changed, slavery reversed? Would black ladies see white boys and clench they purse? What if Diallo didn't get shot forty-one times? What if ..

.
Verse ya mwisho Sister P anataja element 5 za muziki wa rap

Break dancing
Mceeing (Msanii wa Hip Hop)
Graffiti writing
Djing
Knowledge

Sikiliza. .Hapa chini nakuletea mashairi ya wimbo wa "Hey Dj " ambao sister P aliimba

SISTER P - HEY DJ
STUDIO : BONGO RECORD

Verse. 1..

"Nawashuku Ma - dj Wote Ndani Ya Bongo/
Kwa kupiga Track Zetu kisha Nasi Tuna Make Bingo/
Wenye Roho za Korosho Twawalia Mingo/
Machizi Wangu Wote Mnaelewa Hii Hali/
Kwamba Mimi sitishiki Haka ukishika Kisu kikali/
Ninapopata 🚬 🚭 Nabaki Natafakari/
Mistari Ishirini Ipo kichwani Me Sijali/
Siku Ta kukutana na Khalifani , Track ya Kwanza ilikuwa kali/
Sasa nije Kwa Hasira kama Vile jabari/
Au Nije kakamavu kama Vile jemedari/
Kutwa Vishindo Vikuu Na Sauti za Ukali/
Ili waelewe "BONGO RECORD" ni label Yenye Nembo Kali/
Kufanya Uongope Kisha Nao wakae Mbali/
Na kila Wanionapo Wawe wanapashana Habari/
Waseme Yule Dada Gaidi/
Lakini mimi Bado Faridi/
Sipendi kuwa VunguVungu , Bado ni Wa moto Au Baridi/
Kuanzisha Marumbano Beef Ni pale inapopidi/
Najipa Cheo kwenye Rap Me ni Study/
Sauti Yangu inatambaa kwenye Beat kama Radi/
Sinunuliwi Ovyo Ovyo jina Langu linajipa Chart/

Chorus:

Hey..!! hey..!!hey..!! Dj
Fanya Ma - Vitu Watu Wawe Crazy
Piga Bongo Fleva Nasi Tu - Dance
Katika Kumbi zote Friday Mpaka Sunday

Hey..!! hey..!!hey..!! Dj
Fanya Ma - Vitu Watu Wawe Crazy
Piga Bongo Fleva Nasi Tu - Dance
Katika Kumbi zote Friday Mpaka Sunday..

Verse.2

"Nini Visado Watu tumechaza Rumbesa/
Na Bado katika Fani Tunazindi kutikisa/
Ni Siste P Mnyamwezi AmsterRap Prado/
Hatu Ogopi Vishindo Vyenu Eti kwamba Upo Gado/
Na Bado Mimi ni Sister P Me Damu Damu Me Naitwa Tandeo/
Pumbavu..!!! Mnauliza Ningeimba Nini Sister P/
Asinge kuwepo Zay B/
Malumbano Nimesha Acha Me Naelimisha Jamii/
Mtakuja na Marekebisho Mnadhani "Anakuja" Ndo Mwisho/
Swali linarudi Kwako Sasa.?
Hahahaha 😆 😂!!
Ungeimba Nini Mwana Falsafa Tusingekuwepo Wasanii/
Au ungekuwa Poyoyo , Bubu katika Fani hii/
Hadhira ingekuelewa Sasa Umeilimisha Nini jamii/
Au Tukuite fredo Star kwa nyimbo uliotafsiri/
Usanii ni Dili Sometime onyesha Wako umahiri/
Umiza kichwa Emcee Toa Tungo zilizo Sahiri/
Hata Machizi wakibaini Wabaki wakishangilia/
Ukiwa Bills family Nao wabaki wakishangilia/
Hi fani si Mchezo Kaka Usipende Kuingilia/
Radio , Djs Wanafanya Kazi Watu Wanafurahia....

Chorus:

Hey..!! hey..!!hey..!! Dj
Fanya Ma - Vitu Watu Wawe Crazy
Piga Bongo Fleva Nasi Tu - Dance
Katika Kumbi zote Friday Mpaka Sunday

Hey..!! hey..!!hey..!! Dj
Fanya Ma - Vitu Watu Wawe Crazy
Piga Bongo Fleva Nasi Tu - Dance
Katika Kumbi zote Friday Mpaka Sunday..

Verse..3

"Hii track Kali waelevu Wamethamini/
Bado Natoa Dozi kwa Maana Nipo kazini/
Ingia Yap Marafiki Wanafiki Ingia Mitini/
Kama Nimekukera Gaidi Ajali Kazini/
Nazo Nguzo Tano "5" za Hip Hop Weka Akilini/
Kwanza Naanza " DJS" Kuweni Makini/
Bila Nyinyi Emcees Hatuto Wine/
Sisi Ni Tengemezi kama Chanda na Pete/
Pili " EMCEE " Jiheshimu Acha Mapepe /
Usilete Mambo Ya Ajabu kuwafanyia Watu Wacheke/
Mashabiki wakusaliti Wenye Furaha kuwa Wabweke/
Nayo Tutu " TUNGO" zako Sharti Ujumbe zibebe/
Zielimishe Jamii kile Utakacho Waelewe/
Tungo zako zikubalike zitumike Hata Kwenye Mashule/
"BLACK DANCER" Nayo Nne Mtindo Wetu Wakati Ule/
Hili Ndilo Darasa Nakupa Hip Hop Shule/
Kama Umeshindwa Rap Nenda kacheze msukule/
Kwa Maana Kwenye Hip Hop Sisi Hatuhitaji Kasoro/
"HIP HOP" , "CULTURE" Nguzo Ya Tano " MICHORO"
Nafungua Ukurasa Kama Unaweza Toa Kasoro/

Chorus:

Hey..!! hey..!!hey..!! Dj
Fanya Ma - Vitu Watu Wawe Crazy
Piga Bongo Fleva Nasi Tu - Dance
Katika Kumbi zote Friday Mpaka Sunday

Hey..!! hey..!!hey..!! Dj
Fanya Ma - Vitu Watu Wawe Crazy
Piga Bongo Fleva Nasi Tu - Dance
Katika Kumbi zote Friday Mpaka Sunday...

Ukwaju wa kitambo

0767 542 202
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom