mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,910
- 18,558
Heslb wanapanga mikopo lakini mchanganuo unabaki siri mpaka utakapofika chuoni, kwa hiyo unakuwa huna maandaliziyoyote ikitokea umepata mkopo kiduchu. Kuna wanafunzi wamepata mshtukomkubwa baada ya kukuta kati ya milioni tatu za tuition fees pale St Johns kwa kozi ya pharmacy, wamepewa mkopo pungufu ya laki tano hivyo kutakiwa kujilipia zaidi ya milioni mbili na laki tano. Kama wangepewa mchanganuo mapema kabla ya kwenda chuoni kama ilivyokuwa miaka mingine mzazi angeona afanyeje mapema kama ni kuahirisha mwaka au vyovyote vile. Heslb walikwepa makelele waliyoyatarajia kwa kuwa walijua wametoa mikopo kiduchu sana kwa baadhi ya watu, na kujikuta wamewaumiza sana wanafunzi wengi kisaikologia. Ona wanavyosema:
- Nitajuaje kiasi cha mkopo nilichopangiwa?
- Jibu: Orodha ya majina kwa waliopangiwa mikopo pamoja na mchanganuo wa kiasi alichopangiwa kila mwanafunzi, hutumwa vyuoni walikodahiliwa kwa kuthibitisha udahili wao.