Heshimu kila mtu, watu ni walewale - Dotto Biteko

Mohamed Ismail

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2014
Posts
227
Reaction score
246
Anaandika Mo Mlimwengu.

Heshima si utumwa ni miongoni mwa hekaya za wahenga. Waliona umuhimu wa heshima kwamba kumuheshimu mtu haikufanyi uwe mtumwa wake, lakini bado wakaongezea kwamba 'Heshima ya mtu ni utu wake' unapoheshimu wengine unajijengengea heshima yako mwenyewe. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mh Dotto Biteko siku zote amekuwa akielezea mambo ya muhimu zaidi kwa njia rahisi na hii hupelekea kila mtu kumuelewa vizuri.

Mh Biteko anasisitiza kuheshimu watu kwakuwa watu ni walewale, ni maneno ambayo yamebeba dhima kubwa, na hili alichokizungumzia ni wanafalsafa wengi walishakielezea. Immanuel Kant katika falsafa yake ya maadili alisema " Respect for others is the foundation of morality" na akaenda mbali akasisitiza kwamba kila mtu anastahili heshima kwa sababu ya utu, uwezo wa kufikiri na bila kujali hali yake ya katika jamii.
Mwanafalsafa Confucius yeye anasema " Respect yourself and others will respect you " jiheshimu na wewe utaheshimiwa. Bado akaenda mbali akaja na dhana ya Ren ambayo inabeba dhima ya huruma, utu na kutenda wema kwa watu wengine.Akaelezea kwamba hivi vitu inabidi kuonyeshwa kupitia vitendo vya kila siku, kama kuwa na moyo wa kujali watu wengine na kuwa na adabu.

Hii speech ya Mh Biteko wengi walitegemea maneno kama hayo yahubiriwe kwenye nyumba za ibada na viongozi wa dini. Alichokizungumza Mh Biteko unaona hata katika madhehebu yetu ni vitu ambavyo vimebainishwa. Kwenye uislamu Quran inafundisha kuheshimu kila mtu bila kujali hali yake kimaisha na imani yake. Ukisoma Quran 49:13 inaeleza " Enyi watu sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamke na mwanaume. Na tumewajaliieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane" . Hii ni kuonyesha kwamba inabidi tuwe kitu kimoja na tuondokane na dhana ya ubaguzi.
Ukienda kwenye ukristo biblia inahimiza upendo na heshima kwa wote. Mathayo 7:12 inaeleza " Basi yoyote mtakayotendewa na watu nanyi watendeeni hivyo kwa maana ndio torati na manabii ".

Katika kuona umuhimu wa heshima na utu kwenye jamii. Mwandishi John Rawls(1971) aliandika kitabu cha A theory of Justice . Kitabu kinaelezea zaidi muktadha wa heshima kwa kila mtu. Kwenye kitabu chake kaelezea kanuni ya usawa wa fursa, kwamba inabidi fursa zisambawe kwa haki na kaelezea msingi wa haki za uhuru. Kwenye kitabu chake anapendekeza ili kuwa na jamii yenye haki, tunapaswa kuwa na sheria na kuziamulia kwenye mashauri pasipo kujua nafasi yetu binafsi kama hali ya utajiri au maskini, huyu mwanamke au mwanaume na huyu ni kabila gani au anatokea ukanda gani.

Hili somo la watu ni Walewale, Mh Biteko anatukumbusha tuishi na watu vizuri, tusipofushwe na vyeo tulivyo navyo, tusipofushwe na elimu tulizo nazo, tusipofushwe na mali tulizo nazo, tusipofushwe na watu waliotuzunguka kwa wakati fulani. Anatusisitiza kwa mifano rahisi kabisa. Kwamba wote tunahitajiana na hujui hatima ya mwenzako. Kwamba huyu kesho atakuwa pale ila kesho kutwa atakuwa kwingine. Cha muhimu ni tuheshimiane kwa sababu ya utu.

Ukienda mtaani utakutana na mabango wanasema pata pesa tujue tabia yako. Kuna watu baada ya kupata vyeo, wanajitenga na jamii waliyokuwa wakiishi nao. Kuna watu wengine nafasi zao na vyeo vinawapa kiburi wakiona hawatahitaji tena watu.
Speech ya Mh Biteko ni funzo kubwa kwa kila mtu na ukikumbuka tuko kwenye miezi ya ibada ya kutubia kwa mola wetu. Kwa waislamu tutumie ujumbe huu kujitafakari kwenye kipindi cha mwezi wa Ramadhani na kwa wakristo ni kijitafakari kwenye kipindi hiki cha kwarezima.

Mwl Nyerere aliwahi kutusisitiza kwamba tujisahihishe. Heshimu kila mtu na watu ni walewale. Na Mlimwengu mimi ni yuleyule na nyinyi ni walewale.

#mliwengumimi
#watuniwalewale
 
Attachments

  • FB_IMG_1742808607581.jpg
    FB_IMG_1742808607581.jpg
    22.5 KB · Views: 27

TAPELI HUYU. UKIMWONA ANAONGEA KWA MEDIA WAWEZA FIKIRI BONGE LA MTU KUMBE OVYO TU!
 
Mmm...jadili hoja. Hadi hapa umeonyesha hitilifu ya kufikiri na kujenga hoja. Sisi Watanzania ni watu wa ajabu sana. Mimi nimesoma andiko nimeelewa hoja. Yapo muhimu ya kuchukua.🙏🙏🙏
 
Hiyo ndio positive quality, ya Biteko ni down to earth and humble.

Yaani huyu jamaa akiwa anaongea kauli zake namuonaga kama mtu wa ‘mission town’ fulani hivi kuliko kiongozi.

Ana porojo huyo za siasa sijapata kuona.
 
Mjanja tu wa mjini,kageukia kwenye u-motivation speaker,wapumbavu tu ndio wataamini amefika hapo sababu ya kua "humble",
Kazi kulalamika TU,hutamuona anachukua hatua kwenye jambo lolote lile
 
Ajabu ni kwamba CCM hawaheshimu watu.Maana Huwa wanashindwa kabisa kuheshimu maamuzi ya umma na badala yake huiba kura Kila chaguzi ili wandelee kujimegea keki ya taifa
 
Imeletwa hoja. Jadili. Hapa ni kwa great thinkers🙏🙏🙏
 
Huyo uliyemleta ni mungu?............utoe hoja ya kutoa msaada kwa pesa zako za ushoga,na madawa ya kulevya,watu wajadili TU kupokea pesa za haramu?,eti wakimjadili shoga ama druglord hawatakua great thinker?
 
Mmm...jadili hoja. Hadi hapa umeonyesha hitilifu ya kufikiri na kujenga hoja. Sisi Watanzania ni watu wa ajabu sana. Mimi nimesoma andiko nimeelewa hoja. Yapo muhimu ya kuchukua.🙏🙏🙏
Hakika
 
Ajabu ni kwamba CCM hawaheshimu watu.Maana Huwa wanashindwa kabisa kuheshimu maamuzi ya umma na badala yake huiba kura Kila chaguzi ili wandelee kujimegea keki ya taifa
Hata huyu siyo kwamba anaongea yanatoka moyoni ni utapeli tupu matendo yake ni maovu kupita kiasi
 
Huyo uliyemleta ni mungu?............utoe hoja ya kutoa msaada kwa pesa zako za ushoga,na madawa ya kulevya,watu wajadili TU kupokea pesa za haramu?,eti wakimjadili shoga ama druglord hawatakua great thinker?
Nje ya muktadha kabisa. Umekwenda OPP! Kwaheri.🙏🙏🙏
 
Anarudi kwao lini huyu Bahima Empire? Washawaona Watanzania wanapenda kusikiliza maneno ya namna gani hivyo wameamua kuwarubuni ili wawatawale Tutsi Empire hawa.
 
Mkuu shida ya watanzania wengi ni wanafiki, anachozungumza na matendo yake tofauti kabisa , na hii tabia ya kuwa mnafiki ndo shida inayotutafuna kama taifa. Tabia hii imetenezwa na ccm
 
Back
Top Bottom