Nashindwa kuelewa serikali
ina mpango gani na walimu jamani? mtu anajitahidi kusoma kacertificate
kake au kadiploma, au hata kadegree kamoja jamani kwa tabu zake zoote,
wengine kwa kuungaunga wengine kwa kuunganisha anabahatika kuchaguliwa
then unampeleka sehemu kama hii kweli?? hebu chunguza hilo eneo kama
utampata hat mkaza mjomba wa raisi kikwete au hata mawaziri au kiongozi
yeyote wa kisiasa, nani atakaekubali ndugu yake alale kwenye nyumba kama
hii? Mimi siyo mwalimu lakini ninaumia sana ninapopata taarifa kama
hizi, mara ooh mwalimu mkuu kaangukiwa na nyumba, mara oooh mwalimu
anaishi ofisini,. this is too much! kama mtu anashindwa kukufanyia dogo
kama hili jamani utatarajia kubwa litoke wapi? hebu wananchi tuamke
jamani, tunajua kuna mambo meengi sana yamefanywa na serikali ili
kuboresha elimu lakini kwa hili, hamjaniambia kitu,. kuna msemo
tunaoutumiaga kule uchagani unasema hivii..."UKUNDI MANYA KYA NUMBA
AMBIYA KYICHUMI" maana yake ni kwamba ukitaka kujua kilicho nyumbani mwa
mtu angalia mlango wa kuingilia, au angalia getini mazingira
utakayoyaona ndivyo nyumbani kulivyo,.sasa kweli mwalimu ataishi kwenye
nyumba kama hii then elimu ifanikiwe vip hapa? mwanafunzi atashindwa
kuingia form one bila kujua kusoma? ari ya kufundisha ipo wapi?
tusidanganyane bwana, kama ni kuboresha elimu tusifanye theoritically
bali tujaribu kupractice kweli,.Tusiishie kutazama chama tu jamani
tuangalie na watu waliomo huko kwenye chama, tuache unafiki, tuungane
kuleta mabadiliko.
[h=3]hii ndio nyumba ya mwalimu mkuu iliyobolewa na mvua.[/h]
Nyumba ya mwalimu mkuu Chilaile wilaya ya Nachingwea
yabomolewa na mvua
Wanafunzi wakimjengea mwalimu mkuu baada ya
kubomolewa na mvua
Hebu niambieni wadau jamani kwa mtindo huu tutafika kweli? madogo
wanaacha kusoma wanajenga nyumba, jamaniiii????:A S cry: