Heshima kuu kwa PAC, ZZK,Kafulila na wabunge wa upinzani

MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
4,089
5,086
KWA HESHIMA KUU
Naipongeza kamati ya PAC ikiongozwa na ZZK na Deo Filikunjombe.Pia nampongeza Kafulila kwa ujasiri wake na kutokutetereka katika kashfa hii ya escrow.
Tatu nawapongeza wabunge wote wa UKAWA.
Inawezekana hamkufanikiwa kwa asilimia mia moja lakini la muhimu ni kuwa ujumbe umefika.
Kwa wenye macho wameona na wenye masikio wamesikia na wenye utambuzi wanajua nchi inaelekea wapi.
Kama ilivyoelezwa mara nyingi sikio la kufa halisikii dawa na hivi ndivyo ilivyo kwa CCM.
Kwa akili ya kawaida tu mtu kama Chenge anawezaje kuwa na moral authority ya kuchangia katika kutengeneza maazimio ya bunge kuhusu ufisadi huu,ni ajabu kubwa!!!!
Kwa mara ya pili sasa ofisi kuu imetajwa bila kigugumizi na bado tunaamini mikutano ijayo tutajua mengi.Mkapa alitumia Ikulu kupata Kiwira lakini hapa kuna Singasinga tapeli kaiingiza Ikulu mkenge!!
Nampongeza ZZK ametumia hekima ya ajabu,amesikiliza ushauri wa Mwandosya na akanyamazia baadhi ya mambo,huu ndio utu uzima kwani serikali ikianguka leo kwa nchi zetu za kiafrika itakuwa tushatumbukia katika machafuko,well done ZZK,uliona mbali.
Nampenda mno JK lakini naona watu wake wa karibu wanamuangusha,Mungu azinduwe asitumbukie kwenye aibu nyingine,
 
Kuhusu Zito Zuberi Kabwe. Tunahitaji vijana wachache wenye kujitambua. Zzk na kafulila ni kifano hai.
Kuhusu JK Mimi binafsi nilikuwa nampenda kusema ukweli na nilimchagua. Lakini on the way amegeuka jiwe na kuanza kuwadhalilisha waliomchagua na kuwakumbatia ambao hawakumchagua.akasahau kuwa hao ndio kansa ya nchi hii tokea zama. Ndio waliotupelekea katoka umaskini licha ya kubebwa na mfumo. Aasa Mungu amemuacha na anamuonyesha walivyo mchana kweupe! Acha yamkute. Simhurumii hata. Tumegeuka jiwe. Na bado! Mungu ataendelea kudhihirisha makubwa mpaka atubie kwa kuwaachilia huru waliombeba na kumfikisha halo alipo.
 
Back
Top Bottom