Changamoto zipo kwenye magari yote. Ninalo liona mimi ni kwamba wengi wanaingia kwenye biashara ya magari bila kujua. Kwanza sishauri hata siku moja kununua lori kutoka kwa Mtu ambae ameshatumia NDANI YA TANZANIA. Kama umetezama kwa ukaribu sana kwa Mazingira ya Tanzania lazima lori uliendeshe kwa miaka 2 kisha uliuze sababu repair and maintenance cost itakuhamisha mji.
Kama hili gari linakupa 250,000 kwa trip na likakupa 4 trip on average kwa siku. Na kama gross margin yako ni 40% basi kama unaendesha siku 6 kwa week, basi kwa mwezi unaweza kuleta 9.6M. Na kama upo makini ina maana gross Margin a year ni karibu na Million 100. Hili lori umelinunua Uingereza, nashauri ukanunue mwenyewe. Anataka kuagiza ani inbox nakuletea bila hata kukucharge shillingi moja, unanilipia nauli ya ndege nalifuata mwenyewe UK. Bei ya Scania ya 2005 ni kama 25,000 USD mpaka ifike Dar na custom na kila kitu gharama itakuwa 36,000 USD sawa na 64Million.
Kama kwa mwaka Gross Margin ni 100M, ina maana ndani ya miezi kumi ume break-even baada ya kutoa direct related cost. Sasa uki run kwa mwaka mmoja zaidi unakuwa umekusanya return yako kwenye asset, na baada ya mwaka wa pili unauza at fair value ambayo piga uwa haiwezi kuwa chini ya 20% below bei uliyonunulia.
Tatizo kubwa nilionala mimi watu wanashindwa kuelewa kuna tofauti kubwa sana kati ya MSHAHARA NA MAUZO, revenue na salary ni vitu viwili tofauti. Sasa kama wewe unatengeneza 400,000 kwa siku alafu unasimama bar unakula 50,000 ujue umetafuna revenue ambayo mazala yake ni 10 times ya pesa uliyokula. Kabla ujadumbukia kwenye biashara tafadhali jifunze heshima ya pesa.