Hernia Inguinal

nsharighe

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
1,439
2,211
Salamu kwenu JF Doctors,

Naheshimu sana uwepo wenu katika jikwaa hili na natambua mchango wenu katika idara hii ya Afya,

Naomba nijikikite kwenye swala lililonileta hapa, Nina mtoto mwenye umri wa miaka 14, Kwa muda wa mwezi amepata mabadiliko katika balls(Pumbu). Badala ya kuwepo kwa zile balls mbili, kuna kuwa na vibuja buja.

Nilimpeleka chekup Muhimbili wakaniambia ni Ugonjwa wa Hernia Inguinal. Na surgery ndio option peke.

Ivyo nimekuja hapa kupata ushauri zaidi ya ule wa madakatari, uzoefu juu ya ugonjwa huu na Tips anuai..
Pia kama kuna hospitali nzuri na gharama zake nikifahamu itasaidia.

Ahsanteni
 
mkuu kama kiingereza kinapanda google INGUINAL HERNIA, au kwa kiswahili kagoogle MSHIPA WA NGIRI au NGIRI japo utaletewa majibi ya ngiri za aina nyingi ila bila shaka utapata maelezo ya kutosha.

Pole kwa tatizo la mwanao
 
Mkuu nakushauri nenda mbweni hospital gharama ni ndogo,ila kama una kipato kikubwa unaweza ukaenda regency au aga khan au tmj...
 
mkuu kama kiingereza kinapanda google INGUINAL HERNIA, au kwa kiswahili kagoogle MSHIPA WA NGIRI au NGIRI japo utaletewa majibi ya ngiri za aina nyingi ila bila shaka utapata maelezo ya kutosha.

Pole kwa tatizo la mwanao
Nilipitia mkuu, Niling`amua vichache maana lugha ya kisayansi ilitawala...
 
Back
Top Bottom