Henry joseph anaenda kujaribiwa timu gani??

MtuSomeone

Member
Dec 7, 2008
57
3
Wapenda maendeleo ya soka la Bongo hebu naombeni msaada wenu!
Nimesoma Artcle moja kuhusu Mrisho Ngasa kwenda Norway na kwamba nafasi yake tayari imeshachukuliwa!! Ok Tuyaacha hayo...!!
Mimi hoj ayangu wajameni ni "Timu gani wachezaji wetu wanaend akuchezea"? Je kabla ya kupewa "ofa" hizo huwa wanafahamu wanenda kucheza timu gani au kwenda ulaya tu? Najua wengi wenu mnaning'aka lakini leo nimeona Aarticle inayomuhusu Nahodha wa timu ya Taifa, Henry Joseph kwamba anaenda kufanya majharibio Norway!! Hongera Henry!! (Kama umepata..isije kuwa umepatikana)
Article ya kwenye mtandao wa IPP Media inasema..."Taifa Stars skipper Henry Joseph, who was supposed to board Oslo-bound flight today to join professional ranks, had his flight rescheduled for tomorrow.

Henry, who also features for top flight side Simba Sports Club, has been given go ahead by the Tanzania Football Federation (TFF) to join the Norwegian side Thomson. .......The Sweden-based player`s agent, Grenn Schiller, has been duly informed of the changes by his Dar es Salaam counterpart Mehd Rhemtullah, a well established FIFA approved agent"

OK!! Hapo ni mwisho wa kunukuu!! Sasa nikaamua kuingia kwa website ili nijue Nahodha wetu wa MV Taifa Stars anajiunga na timu ya aina gani??? Katika kutizama kwa kweli jina la hiyo timu (kati ya timu zooote zilizopo kwenye Ligi za Norway sikuliona (tazama list hapo chini)!! Sasa ndiyo najiuliza viiiiiiiipi!!!!???
Lakini kidogo nikapata faraja kuona amepata agent japo ana ka-website:-
BRNČIČ & M AGENCY

Agent network - BRNČIČ & M AGENCY

Lakini swali langu la msingi bado lipo pale pale: Henry Joseph anenda kujaribiwa timu gani kati ya hizi??
 
Semesozi, kwa mujibu wa Gazeti la Majira, Henry Joseph anaenda kufanya majaribio katika timu ya Molde FC. Soma habari ya Majira:-

Maximo: Henry Joseph hataiathiri Taifa Stars

Habari Zinazoshabihiana
• Vijana wa Maximo kazini leo 29.11.2008 [Soma]
• Maximo kuchota ujuzi kwa kocha Bafana Bafana 15.12.2006 [Soma]
• Stars yaondoka Denmaki, yaenda Uswisi 21.08.2007 [Soma]

Na Erasto Stanslaus

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Mbrazil Marcio Maximo amesema kuondoka kwa nahodha wake, Henry Joseph hakutaathiri uwezo wa kikosi chake katika fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani zitakazofanyika mwezi ujao nchini Ivory Coast.

Henry na Emeh Izechukwu, wanatarajia kuondoka leo kwenda nchini, Norway kufanya majaribio katika timu ya Molde FC, ambapo kama wakifaulu Henry atakosa sifa ya kuichezea Stars katika michuano hiyo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Maximo alisema kumkosa nahodha huyo katika fainali hizo, hakutaathiri kwa kiasi kikubwa kikosi chake kutokana na kuwa na wachezaji wengi wenye uwezo.

Alisema kwa kuwa bado hajatangaza kikosi kitakachokwenda katika fainali hizo, ataangalia utaratibu wa kuchagua mchezaji atakayeziba pengo la Henry.

Kocha huyo alisema yeye alikuwa mmoja ya watu waliotoa ruhusa ya mchezaji huyo kwenda kujaribu kucheza soka la kulipwa na alifanya hivyo kwa kuangalia manufaa ya Tanzania kwa siku zijazo.

Alisema nchi kuwa na wachezaji wengi wanaocheza soka nje inaongeza nafasi ya kufanya vizuri zaidi, katika mashindano mbalimbali ya kimataifa kutokana na wachezaji wa nje kuwa na uozefu mkubwa wa michezo ya kimatiafa.

"Nitamkosa Henry lakini hakukuwa na sababu ya kumzuia kujaribu bahati yake ya kucheza soka la kulipwa na akibahatika kupata nafasi, ataitangaza Tanzania katika ulimwengu wa soka," alisema Maximo.

Maximo alizitaka klabu nyingine kutowazuia wachezaji wao, kusaka timu za kucheza nje ya nchi kwani kufanya hivyo ni kuwanyima haki yao ya msingi wachezaji hao na kuirudisha nyuma nchi kisoka.
 
Back
Top Bottom