Henje Kafulila, Manyanya live Star tv

muhosni

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
1,108
152
Wanaongelea Siasa na ajenda ya ustawi wa maisha ya wananchi.

Kafulila ameshusha takwimu za uchumi na umaskini wa tz kuonesh kwamba tz ni tajiri sana na wananchi wanahoji umaskini unatoka wapi wakati serikali na chama tawala wanashindwa kutoa majibu

Stella Manyanya na mzee mmoja kada wa ccm wanasema Spika aheshimiwe, wanasiasa waenzi amani ndo tutapata maendeleo. Kwamba vyama vya upinzani viache kulalamika, viheshimu serikali, washirikiane na chama tawala

Henje bado hajaongea
 
Waheshimiwe kwa lipi kama wameiba mali za nchi dharau ndio dawa yao mimi naona wananchi wana upendeleo kwanini wanaua vibaka wa mtaani na kuwachoma moto ilihali wezi wakubwa wa mali za nchi wanapita na magari wakitutimulia vumbi,siku moja tusimamishe fisadi mojawapo na kumshughulikia kama kwa vibaka naona ndio dawa iliyobaki tu
 
Hao wasitusumbue spika aheshimiwe kwa lipi,mbona Sitta hakuomba aheshimiwe huyu mama mbovu na wabunge wamepoteza imani kwake hata akifanya vipi hawezi kuwaelekeza kwani anadhani wabunge ni watoto wadogo wa kuwaonyesha hasira zake lakini apandacho mtu ndicho avunacho ccm walimpanda wanalalamika nini angekuwa na uwezo kama wenzake akina Migiro hata wanawake wenzake Tanzania wangemtetea.Lakini tumpe pole kwa kubebeshwa mzigo mzito pasipo ccm kujua uwezo wake
 
mimi nimewaambia siku zote,uvivu wa kufikiri wa viongozi wetu ndio unaosababisha matatizo yote haya,unaona sasa leo wameenda kulalamika na kumtetea spika badala ya kujibu hoja zinazowasumbua watanzania,aiseee nasema hiviiiiiiii huo ni upofu wa mawazo.
 
tatizo kubwa la mama spika wetu ni kuwa anahasira na jazba, yeye anadhani kuwa yupo kwnye bunge la chama kimoja tena kilichosafi, analiendesha bunge kama taasisi ya chama. Anahitaji kusoma alama za nyakati kuwa wabunge wa 1990s sio hawa wa leo asipo kuwa makin atatoa machozi bungen cku moja, pia mkondo wa siasa umebadilika. AMEFIKIA STAGE YA KUTUMA VUVUZELAZ ZIKAMPIGIE UPATU KWENYE MEDIA AHESHIMIWE! TOKEA LINI MAMA AU BABA MWENYE KUIJALI FAMILIA YAKE AKAOMBA AHESHIMIWE!MATENDO YAKE NA MWENENDO WAKE NDIO UNAOWAFANYA WATOTO WAMHESHIMU. mama spika atabue kuwa zigo la ccm halibebeki sasaivi, mzigo uliomshinda makamba hatouweza kamwe.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom