NATA
JF-Expert Member
- May 10, 2007
- 4,492
- 1,313
Dada analalamika boss wake hasafishi kinywa , na wanafanya kazi katika ofisi moja ambayo ni ndogo , Hivyo anateseka sana kwani boss akiongea tu basi harufu hiyo kwake na inasambaa chumba chote na kazi yake huyu dada inamtaka awe kwenye meza yake muda wote.
Huyu ni boss wake na nimkubwa kwake kiumri anatamani amwambie but anaogopa na anamuheshimu sana anashindwa aanzie wapi.
Boss anamke na watoto, sijui huyo mke naye anaogopa kumwambia.
Anatafuta ushauri afanyeje , na kazi anaitaka na muda mwingi wa siku anatumia kuwa katika ofisi hiyo. Pia angependa kujua kama kunamadhara yoyote yatokanayo na bad smelling gases inayotoka katika midomo ya mtu.