Pole sana binti.
Wewe una tatizo,kitaalam linaitwa Schizoid Personal Disorder. Dalili zake ni pamoja na kujitenga na watu,kutoshirikiana na watu,kukosa hisia za kua na watu nk.
Hili tatizo mara nyingi hudhaniwa linatokana na matatizo au ulezi mbovu aliopitia mhusika,alinyanyaswa,kuteswa,kutengwa nk. Mfano mzuri unaweza kuupata kwa watoto wa mtaani,ukimchukua ukae nae utagundua hapendi kuwa na wenzake. Sijajua kama na wewe ulipitia huko au ulikosa mapenzi utotoni.
Wagonjwa wa tatizo hili huwa hawataki au hawana hisia za ngono kabisa na wengi wao hawana matatizo ya anorgasmia(kukosa kusisimka ukiwa unafanya ngono),au wewe uko hivyo?sidhani kama una mpenzi.
Hiyo social alienation uliyonayo inatokana na tatizo hilo,wenye matatizo hayo huwa hawajijui hadi waambiwe,kama ulivyoamiwa,ni tatizo na unahitaji tiba ya kitaalam.
Tiba yake,unatakiwa kuwa karibu na watu,mtu anaeweza kuzisikiliza hisia zako,inatakiwa clossness,emotional intimacy zinazaidia ingawa sio rahsi sana maana watu wa tatizo hilo hawapendi ukaribu na wengine.
Kwa ushauri waone Behaviorists wakufanyie Cognitive/Behavioral therapy au Talk therapy. Atakavyoona mwenyewe,mimi nimeenda moja kwa moja kwenye tatizo kama ulivyolielezea,ila inawezekana kabisa tatizo lako linatokana na Obssessive Compulsive Disorder.