Helmeti zatajwa kuwa chanzo cha maradhi ya ngozi

Babu wa Kambo

JF-Expert Member
May 2, 2016
559
808
Wakati Sheria ya Usalama Barabarani inamtaka kila dereva wa bodaboda kuwa na
kofia ngumu (helmeti) mbili kwa ajili yake na abiria, watumiaji wa vyombo hivyo wapo hatarini
kuambukizwa maradhi ya ngozi.

Hatari hiyo inatokana na matumizi ya helmeti chafu.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk James Kiologwe alisema watumiaji wa usafiri huo
wamekuwa wakitumia helmeti moja bila kujali kama imefanyiwa usafi, huku wengine
wakilazimika kuvaa zilizo chafu ili kutekeleza matakwa ya sheria.

Chanzo:Mwananchi


MYTAKE; Serikali iangalie upya utaratibu huu, suala kama hili halina haja ya kumsubiri Daktari aseme, hata kwa akili ya kawaida tu unagundua lina madhara, haiwezekani mchangie kifaa kimoja cha kuvaa kwenye mwili watu hamsini tena siku moja
 
Wangefanya utaratibu kila dereva wa boda awe na zile soft abiria anapo panda anavaa soft rambo kichwani ndipo anatumbukiza helmeti!
 
Back
Top Bottom