Helena(Simulizi ya huba)

Helena(Simulizi ya huba)

Mogambi

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2012
Posts
213
Reaction score
357
01


Naikumbuka vema ile siku. Alinipigia simu, nami nikaipokea kwa bashasha na furaha tele. Huyu alikuwa mpenzi wangu, mwanamke aliyenipa raha mara nyingi. Hellen.

'Mambo vipi mpenzi? Uliona email niliyokutumia? Nilikujulisha kuwa narejea nchini, lakini sijapata tena nafasi ya kucheki kama ulijibu. Kuna mambo fulani fulani yalitokeza na kukatisha mawasiliano. I miss you babe!' niliongea kwa sauti ya furaha. Kawaida, mimi hutabasamu kabla hata ya kusikia sauti ya Hellen, yaani ile nikiona kwenye kioo cha simu yangu jina 'Hellen', basi moyo wangu hufukuta kwa fukuto la furaha, hata kama ningekuwa na huzuni, mie huisahau mara moja hadi pale nitakapomaliza mazungumzo. Na ni kweli kuwa jina lake kwenye simu yangu nimelihifadhi hivyo hivyo kavu kavu, "Hellen" isipokuwa tu mbele yake kuna "Hr 301". Kwa wanachuo wanaelewa hili hutokea sana hasa kwa vile mnapopangiwa seminar na kazi za makundi unasevu namba za watu mnaoshiriki hizo kazi pamoja. Na kwa vile chuoni mnakuwa watu wengi, utalazimika kutafuta namna ya kutofautisha majina. Si ajabu ukawa na Hellen kumi kwenye simu yako, na kama hujaweka ubini, ni dhahiri kuwa utahitaji kuwatofautisha kivyovyote vile. Hii ndio hupelekea mtu kuseviwa Vick cheusi, au Vick mzaramo nk. Hellen Ni mpenzi wangu, lakini jina lake sijalisevu kwa zile mbwembwe za 'my love', au 'Honey' au 'laaziz kama ilivyo kawaida ya wapenzi. Unawezajiuliza kwa nini, siyo! Nitakufahamisha hapo baadaye, lakini yeye Hellen anajua kwa nini jina lake nimelisevu kavu likifuatiwa na HR 301.


Sasa basi, naweza kusema, ingawa tupo kwenye mahusiano kwa miezi takribani minne sasa, lakini ukiniona navyotabasamu kumuona Hellen, basi unaweza kukokotoa na kupata jawabu la uongo. Ndiyo, la uongo. Utajua tu kwamba huyu jamaa, ndiyo kwanza kamuona huyu binti na amemzimikia kinoma. Kawaida, pumbazo langu la kwanza nilipokutana na Hellen mara ya kwanza miezi mitano iliyopita, basi limekuwa likibaki hivyo hivyo hata sasa baada ya miezi hii yote kila napomuona. Aisee! Huyu binti kajua kunishika. Mie zuzu wallah!.

Basi, turejee kwenye simu. Baada ya kupigiwa naye na kujitetea kabla hata hajasema kitu, nilisubiri kwa hamu niisikie sauti ya mpenzi wangu, ambayo kuisikia pekee, hunipatia burudani nafsini mwangu.

'Niliiona email Derick, na nimeshaijibu. Uko wapi?' Hellen alizungumza kwa sauti tulivu. Sauti ambayo sikuizoea. Haikuwa na ule uchangamfu wa siku zote. Najua haikuwa nao, japo alijaribu kuongea kwa kuniigizia. Namjua mpenzi wangu bwana huwezi kunidanganya kitu. 'Hellen wangu ana shida gani jamani!'. Nilijiuliza. Ah, sikuvumilia kubaki najiuliza tu, nikaamua kuondoa hilo dukuduku moyoni mwangu.


'Vipi dear, mbona umepoa hivyo mpenzi? Kunani tena darling. Eh mamii, are you sick mpenzi?' nililazimika kuhoji, ile furaha yangu ikiyeyuka kama donge la barafu kwenye joto kali. Aisee, sio siri, niambie habari gani sijui, lakini habari za huzuni hunibeba sana mimi. Nadhani, huu ni udhaifu kwangu mimi mtoto wa kiume, kuwa na hisia nzito sana au tuseme kutekwa kihisia kwa urahisi. Mimi ni mwepesi sana wa furaha na huzuni vile vile. Ndio maana najaribu kusoma soma masuala ya saikolojia, kunisaidia kuwatambua matapeli mapema. Si unafahamu matapeli wanacheza sana na hisia! Naam, matapeli buana wakikujua wewe ni mtu unayepata huzuni ukielezwa tukio la kuhuzunisha, wao ni wepesi sana kupita humo, wakakulisha habari ya msiba, ukajikuta unachangia nauli ya kwenda msibani kwa kuwaonea huruma, kutokana na matatizo chungu nzima watakayokuorodheshea.

Huzuni iliyokuwa moyoni mwangu kusikia tu ukosefu wa uchangamfu kwenye sauti ya Hellen, ungedhani nimepashwa habari za msiba.


'Siku hazilingani mpenzi, hata hivyo kiafya niko poa tu sema nimekumiss. Kama tunaweza kuonana itakuwa poa sana. Nahitaji tuongee!' Hellen alizungumza kwa utulivu ule ule.


'Ok dear, nipo Changanyikeni now. Nije au uje?' nilimtupia swali japo ilikuwa wazi kwamba alinihitaji niende. Kikawaida, akihitaji kuja kwangu, yeye huja baada ya kujibiwa message yake ya neno moja ambayo ni mimi tu naielewa 'Hr301'. Hiki ni kifupisho cha moja ya kozi ambazo zilitukutanisha mimi na Hellen miezi mitatu iliyopita. Usijali. Nitakuelezea. Najua unataka ujue ilikuwa vipi.


Itaendelea.


2


Kwa kawaida vyuoni, kozi huwa zinakuwa na majina ya vifupisho. Mfano hiyo Hr inasimama badala ya kozi inayoitwa 'human rights' (Haki za binadamu …) na hiyo 301, Sina hakika, lakini nahisi inamaanisha mwaka wa masomo. Maana kulikuwa pia hr 101 iliyofundishwa mwaka wa kwanza, hr 201 ilifundishwa mwaka wa pili. Hivyo nadhani kabisa hiyo ndio ilikuwa maana yake, yaani mwaka wa tatu.


Hellen yeye amesoma kozi ya Archaeology, na mimi nilisomea kozi ya Political Science and Public Administration. Kwa hiyo, tulikuwa kozi mbili tofauti kabisaa na ndiyo maana tulikuja kufahamiana mwaka wa tatu. Ajabu ni kuwa, kwenye semester ya pili ya mwaka wa Mwisho wa masomo yetu, mimi niliamua kuongezea kozi hii ya human rights, kama kozi ya ziada tu. Haikuwa lazima kuisoma, kumbe naye, aliamua kufanya hivyo tusijue kama ndio kitu kingetukutanisha.


Mimi ni mtu mmoja ambaye, napenda kubeba majukumu yangu kwa mikono miwili, tena kwa umakini wa kiwango cha juu kabisa. Na hii naweza kukudhihirishia kwa mambo ninayoamua kufanya, ni lazima nione yamekamilika, hapo ndio naweza kurelax. Sasa basi, kwenye hiyo kozi, nikajikuta nimepangwa semina moja na Hellen. Halafu tena, tukapewa group assignment (kazi ya kikundi) watu kumi, mimi na yeye tukiwa miongoni mwa wanakikundi.


Shida ikawa moja, wadau wote niliopangwa nao, ama walikuwa wapuuziaji wa mambo au walikuwa na mishe nyingine muhimu kuliko shule. Watu hawa, tulipokubaliana muda wa kukutana kwa ajili ya kujadiliana na kutafuta majibu ya kazi tuliyopewa, hawakuonekana. Nikajikuta peke yangu eneo la tukio. Bahati mbaya sana ilikuwa kwenye kikao hicho ndio tukabidhiane mawasiliano kwa ajili ya kupeana taratibu na yanayojiri mengine.

Kitu nilichokuja kubaini baadaye, ni kwamba wale wanakikundi wenzangu, kila mmoja kwa wakati wake, alikuwa anajidanganya kwamba ni yeye pekee hajahudhuria kwenye majadiliano, na hivyo kujitia moyo kwamba hakuna kitakachoharibika. Lo! Walijidanganya sana. Baada ya hali kuwa hivyo, basi nikalivalia njuga suala hilo mimi mwenyewe. Nikaanza kuandika kazi ile mimi mwenyewe kwa juhudi kubwa. Uzuri ni kwamba, kwa mfumo wa zile semina za chuoni, kwenye uwasilishaji hoja, angeweza kuteuliwa mmoja akatoa wasilisho lote kwa niaba ya kundi lote, huku wale wengine wakisaidiana naye kujibu hoja ambazo zingeibuliwa kwenye mjadala wa pamoja baada ya wasilisho. Ni kusema kuwa, niliamua kuwa jeshi la mtu mmoja.


Hali hii haikuwa ya kwanza kuwahi kutokea, nilikwishakutana na visa vya namna hii mara kadhaa tangu mwaka wa kwanza, sema hii ilitia fora. Awali nilikuwa nakutana na watu wachache au wengi, wakakosekana baadhi. Lakini hii ilikuwa mara ya kwanza wote kukosekana. Sikujali. Kwanza kabisa, mimi najijua, napenda sana kufanya uwasilishaji, hivyo hata kama ingekuwaje, tuseme kwa mfano angelichaguliwa muwasilishaji mwingine, bado ningelijiandaa kama vile mimi ndio muwasilishaji mkuu. Ndiyo. Kila mtu na ulevi wake bwana, na mimi wangu ulikuwa huu wa kupigiwa makofi na kupewa sifa kwa uwasilishaji bora na wahadhiri pamoja na wanachuo wenzangu. So, kusema kweli, nilijiandaa vema kwa nondo za uhakika.


Siku ya uwasilishaji, mimi nilienda kwenye semina kama kawaida kwa muda uliopangwa. Kumbe bwana, wale jamaa zangu, kwa kutaka angalau wapate point mbili za kujitetea nazo ikitokea wametakiwa kutoa hoja, waliwahi nusu saa kabla ili wakutane na wahusika wengine, wadandie points. Hali ikawa ngumu pale wote tisa walipojikuta hakuna hata mmoja aliyehudhuria kwenye majadiliano. Kimbembe kikawakumba. Wakaanza kuhaminika. Wajadiliane, waandike, wawasilishe, na bado kazi hiyo ilihitaji kukusanywa ikiwa imechapwa!. Walihaha si kidogo. Niliwakuta jamaa wameloa jasho wakihangaika.


Ilikuwa dakika tano hivi kabla ya muda wa wasilisho kufanyika. Dah! walikuwa wamejikatia tamaa vibaya sana. Mwanaume nikaingia kwa mbwembwe na kabrasha zangu kwenye backpack yangu, utadhani waziri wa fedha anaenda kusoma bajeti bungeni.


'Oya waungwana, muda wa kuingia kwenye semina huu. Vipi bado mnagaagaa na upwa?' Nikawauliza.


'Hivi si tupo wote wewe?' Aliniuliza jamaa mmoja anaitwa Stanley.


'Yeah man, twendeni tukawasilishe wazee!' niliwaambia.


'Vipi mwanangu uliandaa wasilisho?' akaniuliza tena.


'Haya ndio mambo niliyofuata hapa mlimani. Hebu njoeni hapa wadau, tuwekane sawa kabisa.' nilitamka kwa sauti kubwa yenye mamlaka. Najua kwa wakati huo walikuwa tayari kunisikiliza kwa hamu zote, si nimekuja kuokoa chombo kisiende mrama? Basi wakanisogelea wakiwa watulivu kama vifaranga walionyeshewa. Nikawaangalia nyuso zao zilivyotia huruma. Mwenyewe nikacheka sana kimoyomoyo.

FB_IMG_1613618916508.jpg
 
Imeandikwa na David Ngocho Samson

HELENA SIMULIZI YA HUBA 03

'Waungwana, tumefeli sana kwenye kipengele cha uungwana, fikiria wote mlikimbia majadiliano na kuniachia mzigo wote nibebe mimi?' nilivyotamka hivyo nikaona nyuso zao zikipata nuru ya tumaini jipya. Kwa sababu walau walipata uhakika kwamba kutakuwa na kazi ya kakabidhiwa kwa profesa.


'Sasa. Hapa nimeshaandaa nondo, nina uhakika wa asilimia mia wa kuwapatieni A ya bure. Lakini mnatakiwa mfahamu kuwa, nimetumia muda na gharama. Hapa tunafanya changisho, ndiyo unapata fursa ya kusaini jina lako kwenye wasilisho. Kila mmoja anachanga buku mbili mbili. Tufanye fasta, naona bado dakika tatu tuingie kwenye semina.' niliongea kwa kujiamini sana nikiwa nimevalia sura ya kazi. Hakuna aliyebisha. Nikazikusanya buku mbili mbili, tukazama darasani.


Kama kawaida yangu, kumbuka nimekueleza huu ndio ulevi wangu. Muda wa wasilisho ulipofika, nilikabidhi nakala ya wasilisho kwa msimamizi wa semina yetu. Profesa Nkungu, halafu nikaanza mbwembwe zangu za uwasilishaji hoja. Huu ndio uwanja naofanyaga mambo yangu, basi nikawa nipo namwaga sera zangu huku nikishuhudia zinavyowaingia wadau. Nikamuona profesa anatikisa kichwa juu chini kukubaliana na hoja zangu. Nilipoweka kituo baada ya wasilisho, chumba kizima walikuwa wanapiga makofi. Kwangu ilikuwa burudani kabisa. Wale jamaa zangu hawakuamini. Niliwapatia alama A kama nilivyowaahidi. Profesa akasifia sana kundi letu.


Basi, tulivyotoka kwenye semina, nikiwa naondoka mdogo mdogo kuelekea kwenye vimbweta nikaperuzi peruzi notes zangu. Nikasikia sauti nyuma yangu. 'Derick'. Ilikuwa sauti laini, sauti ya kike. Ikanilazimu kusimama na halafu nikageuka nyuma, maana chuoni kuna watu wengi na wakina Derick sikuwa mimi pekee.


'Naomba nisubiri tafadhali' yule msichana alitamka. Nikakumbuka ni miongoni mwa wale wanakikundi niliowatoza shilingi elfu mbili mbili.


'Mimi?' niliuliza kwa mashaka Huku nikijisontea kidole kifuani kwangu.


'Ndio, wewe si Derick?' akatamka kwa ulizo.


'Ndio, lakini kwenye chuo kinachodahili maelfu ya wanafunzi, huwezi kudhani utakuwa mtu pekee mwenye jina kama lako, sivyo? Nilimweleza.


'Sawa, upo sahihi nadhani.' alitamka yule mrembo.


'Haina kudhani hiyo, ndio uhalisia wa mambo' nikamuhakikishia.


'Kuna hoja unashindwa kujibu kweli?' mrembo huyu aliniuliza.


'Ah hayo masihara sasa. Of course kila hoja inaweza kujibiwa. Kwa kukubaliwa au kupingwa' nilimwambia, halafu nikaongezea, 'Pale palikuwa na Helen, Mwajuma, Aisha na Doris, wewe utakuwa nani kati yao?' niliuliza nikiwa nimetaja majina ya wasichana ambao walikuwa sehemu ya kundi langu la wasilisho.


'Tabiri!' alinambia akiwa anatabasamu.


'Haha, mie si Sheikh Yahya bwana. Lakini kwa vile umenipa cheo hicho, wacha nijaribu, kwani nikikosea kuna hukumu?' akatikisa kichwa kulia na kushoto kumaanisha hakuna hukumu. Nami nikaamua kwenda na jina la kwanza.


'Hellen' nikatamka bila kupepesa jicho.


'Nilijua unafahamu, sema unataka kuniigizia tu!' aliongea akinisuta.


'Haha' nikajichekea zangu. Sikufahamu jina lake, lakini sikuona kwa nini nisitumie lift hii niliyokua napewa bure, ya kufahamu nisichofahamu.


'Enhe nambie Hellen, wewe na wenzio mna tabia mbaya sana. Mbona mkaniachia kazi peke yangu' sikuwa na hoja na kulikuwa kumepita ukimya wa sekunde kadhaa kati yetu, hivyo nikaona niongee kauli hiyo kufufua mjadala. Huwa sipendi nikiwa na mtu kuwe na ukimya kati yetu, hasa kama ni jinsia ya kike. Kuepuka kumtongoza, basi mimi huanza kuleta simulizi za kutunga za uongo na kweli ili kuepuka ukimya. Mara nyingi, nautafsiri ukimya kama mlango wa kuruhusu mwenzako aingie moyoni mwako na kuibua hisia za mapenzi hasa mnapokuwa hamna jambo lingine la kufanya zaidi ya kutazamana.

4

Sio kwamba sipendi kutongoza. La hasha! Ni kwamba, ili kudumisha nidhamu binafsi, sipendi niwe kwenye mahusiano na msichana tunayeonana kila mara. Yaani darasani, kwenye semina, canteen na maeneo mengineyo ya chuoni. Ndiyo maana niliamua kuwa na mahusiano na msichana ambaye anasoma chuo kishiriki cha chuo kikuu Cha Dar es salaam, kampasi ya Duce - Chang'ombe. Anaitwa Welu. Hii ina maana kwamba, tulikuwa tunaonana wikend tu na mara moja moja kati kati ya wiki. Kwangu mimi, hiyo ni heshima. Kuna kumisiana na kutarajiana kunakoamsha penzi na kulifanya liwe kileleni muda wote. Inanipa pia muda wa kufanya ishu zangu nyinginezo bila kuingiliwa na ile michezo ya kimahaba ya kusapraiziana. Pia inaepusha migongano na migogoro midogo midogo inayoyumbisha penzi kama vile wivu pale unapomuona mwenzio anazungumza na mtu wa jinsia yako, halafu ukajikuta unaanzisha zogo. Inakuwa utoto, maana mara kadhaa nimeshuhudia washkaji wanatandikwa mbele ya mademu zao kwa sababu hizo za wivu. Kukaa unaumia moyoni kwa sababu unajikuta umejipachika ukachero wa kumfuatilia mwenzio nyendo zake, kama vile yeye ni mtoto asiyejua anachofanya. Mara unaanzisha zogo na kaka mtu pasipokujua, au mrembo wako anazungumza masuala tofauti na mwanaume mwingine, wewe unahisi anatongozwa, unajitosa umuoneshe umwamba huyo jamaa, halafu unatoka hapo umevimbishwa midomo au umepasuliwa komwe. Hayo ndio mambo naepuka kwa kuwakwepa warembo wa kuonana kila mara. Shida kubwa ya wivu ni kwamba, hujijui kama una wivu, na hata unapofuatilia mambo ya mpenzio, unakuwa pia hujui kwamba ndio umeanza upelelezi. Unajikuta mtumwa wa mpenzio bila kujua. Ah, hayo mie siyataki kabisa.


'Dah, ungejua ungenipa pole mwenzio!' Hellen aliongea kwa unyonge. Ah, kama nilivyokueleza awali, nina wepesi sana wa kubebwa kihisia. Ndio maana, kusema kweli, sipendi kusikiliza simulizi za huzuni, najikuta tu navutwa makini, na hali hiyo huniondolea mudi ya furaha. Mimi napenda habari za furaha, hizo tu, basi. Sasa, ajabu ni kuwa mtu akinijia na simulizi ya huzuni najikuta namsikiliza huku nikibebwa kihisia utadhani suala husika linanihusu.


'Oh Pole sana Hellen.' nilitamka huku nikiingiza mkono kwenye mfuko wa suruali yangu na kuchomoa wallet.


'Naamini sijakutendea haki kuchukua buku mbili zako, bila kujali ulikuwa na madhila gani. Tafadhali nisamehe.' niliongea huku nachomoa elfu mbili kwenye wallet na kumkabidhi Hellen.


'What?? Noo Derick, Noo! Actually nimekufuata kutaka kukushukuru kwa jinsi ulivyookoa jahazi. Mimi napenda sana kushiriki kwenye discussion. Siku ile nilipata dharura, kulikuwa na kikao cha harusi na mimi nilikuwa nahusika kwa sehemu kubwa, so nikakosa namna ya kuomba udhuru, hivyo nikalazimika kukosa.'


'Ah, that's better now. Unajua hakuna kitu kinachoumiza kama kuwa-taken advantage of (kuchukuliwa poa) kwa sababu ya matatizo yako. Kwa hiyo, ulivyoanza kwa kusema nikupe pole, nikajua itakuwa tu ulikumbwa na matatizo. Haha, kwa hiyo anaolewa dada au unapata wifi?' nikauliza kwa utani. Nikaona kama Hellen alishituliwa na swali langu, au kuna namna swali hilo lilimuondolea hali ya kujisikia amani (comfortability).


'Haha, forget about that. Derick, I love your way of doing things. ( Sahau kuhusu hilo, napenda sana unavyofanya mambo yako) Jinsi ulivyoshusha nondo mle ndani najisikia kukutoa out, lakini shida ni moja tu. Natakiwa tena kwenye kikao cha wajasiriamali mjini. So, please accept this as my gesture of appreciation (tafadhali pokea hii kama shukrani na hongera yangu) .' Hellen aliongea huku akinikabidhi noti ya shilling elfu kumi. Wow! Nikabaki nashangaa. Nikawa sina neno la kusema. Hata kusema asante nikasahau.


'Would you mind if I had your phone number?' (naweza kupata namba yako?) Hellen aliniuliza akiniangalia kwa jicho fulani hivi! Sauti hiyo ikanitoa kwenye pumbazo la muda nilikokuwa nimetopea.


'Hellen' nikatamka nikiwa nimekumbatia viganja vyake kwenye viganja vyangu. Kwa muda nikahisi kama nilimpotezea kabisa umakini wake. Kumshika viganja vyake lilikuwa jambo ambalo hakulitarajia, vinginevyo, basi kulikuwa na umeme ambao ulitokea kwa mikono yetu kukutana hata akapatwa na mshituko ule.


'Asante sana, lakini neno tu la shukrani linatosha. Huna haja ya kulipia. You are a nice person. Please keep the money, ok. I appreciate your appreciation.' (Wewe ni mtu poa sana. Hata hivyo, siwezi kupokea fedha yako. Jua tu, nimekubali kunikubali kwako) niliongea kwa sauti tulivu. Sauti ya kunong'ona. Huenda kuna namna sauti hii iliamsha kitu ndani yake. Nilihakikisha anaipokea noti ile ya elfu kumi halafu katika kuua Soo kufuatia ule umeme, nikaanza kuropoka namba yangu.

'My numbers are zero….. ' nikaanza kumtajia namba zangu, lakini nikasikia sauti yake ikisema kwa utulivu

'Wait a minute' (subiri kwanza) nikalazimika kutulia wakati akichomoa simu yake kwenye mkoba. Ilikuwa tablet moja amazing. Of course kwa enzi zile, Ilikuwa ni moja ya simu ya gharama sana. Well, mimi nilikuwa na kismart changu cha tekno, fresh tu!


'Ok, nitajie' alitamka tena Hellen.


'07174117..' nikamtajia na yeye akaziandika kwenye simu yake. Sekunde kadhaa mbele nikasikia kimeo changu kinaita.


'That's my number' akatamka. Halafu akaniambia

'Sasa, mie niwahi bwana!'


Ni kama sikusikia, lakini nilimsikia, sema tu kuna namna huyu dada Hellen alikuwa ananipumbaza kwa sauti yake tamu. Nikiwa nimeganda sijui cha kusema, nikashitukia Hellen amenibusu shavuni halafu yule ananipungia mkono akiwa anaondoka. Nikabaki nimeduwaa. Nilipopata akili ya nini hasa kimetokea, Hellen alikuwa keshapotea kwenye upeo wa macho yangu. Kama vile bwege, nikabaki nimeinyanyua mikono yangu juu, nikimpungia hewani, tabasamu tele midomoni mwangu, nikifurahia ufahamu huo mpya. Naam, ufahamu kwamba Hellen huenda ananipenda.


Itaendelea

FB_IMG_1613618945623.jpg
 
HELENA SIMULIZI YA HUBA 05
DAVID NGOCHO SAMSON

5


Turejee kwenye mawasiliano yangu na Hellen aliponipigia simu mwanzoni mwa simulizi hii.


Nilipomuuliza Kama anakuja au niende Mimi, Nilijua kabisa kwamba alinihitaji niende. Vinginevyo angekuwa ametuma ujumbe wa 'hr301'. Ujumbe ambao ulikuwa na maana kuwa 'nakuja mpenzi'. Tuliamua kutumia hr301 kwa kuwa ni kozi iliyotukutanisha na ndio ilikuwa mwanzo wa penzi letu. Lile wasilisho la hr 301, ambalo nililibeba peke yangu kwa niaba ya watu kumi na kulitendea haki na kuwazawadia alama A wanakikundi wenzangu, ndio lililozaa penzi kati yangu na Hellen. So kutokuiona meseji hiyo, kulinifanya nijiandae ili nikaonane na Hellen chuoni.


Nilizama bafuni, nikajimwagia maji fasta na kutinga suruali ya jinsi la bluu na fulana yenye maandishi madogo kifuani 'University of Dar es salaam, Gender Club', fulana nyeupe. Miguuni nilivaa openshoes, sandals fulani za kimasai zenye mikanda ya ngozi na rangi ya damu ya mzee. Nikachukua kismart changu cha tekno na headphone, nikazining'iza shingoni, nikafunga mlango wa chumba changu, nikatoka na kumkuta Siwema anafua hapo uani.


'White Derrick huyo!' Siwema alinitamkia kwa utani.


'Oh mtoto mzuri Siwema, naona kama kawaida yako unaandaa mitoko' nilimtania.


'Mitoko gani na wewe hutaki kunitoa?' Siwema alinitamkia kwa aibu.


Siwema ni binti mrembo sana. Mtoto wa kisukuma. Ni kwa vile tu ni jirani yangu. Na kwa falsafa yangu, sianzishagi mahusiano na mtu nayeonana naye mara kwa mara, vinginevyo ningekuwa tayari nimeshaanua vyombo, najilamba kwa utamu. Ukweli ni kwamba binti huyu alikuwa ananizimia ile kinoma na nilijua kabisa. Kuna wakati nilitaka kuharibu kabisa kwa kuvunja miiko yangu lakini kaka yake akatokea mapema. Siwema anaishi hapa na kaka yake ambaye anachukua masomo ya uhandisi, computer engineering pale COET. Na huyu bwana ndio anamsomesha Siwema. Siwema yupo kidato cha tano sasa.


'Unataka nitandikwe fimbo za kisukuma nini? Si nasikia wasukuma ni noma kwa kupigana kwa fimbo!' niliendelea kumtania.


'Unajua sio poa Derrick, naona tu unaleta kutoka mbali wakati nami naishi hapa hapa na nakuhitaji' Siwema alilalama, haikuwa utani. Kuna vile nilimuonea huruma kabisa.


'Ah, unajua shida ni braza yako, keshanipiga biti juu yako.' nilimweleza huku nikianza hatua moja baada ya nyingine na kuondoka.


Siwema alikuwa ananizimia sio kidogo. Ile siku ambayo ilikuwa kidogo niharibu, nilikuwa nimeenda zangu bafuni kuoga. Niliporudi tu ndani, nikamkuta Siwema yupo chumbani kwangu ameketi kitandani. Ah, aisee, acha kabisa, ilikuwa bonge la jaribu. Maana mtoto alikuwa ameketi kitandani na nilipoingia tu, akanipokea kwa busu moto moto. Mara, kabla hakijafanyika kitu, tukasikia mluzi ambao sote tunaufahamu, ilikuwa kaka yake. Mshikaji alikuwa na itikadi za kihenga sana. Yaani alikuwa akirudi, basi lazima ajipigize miluzi halafu anaelekea chooni kwanza, akitoka huko sasa, ndio anaingia chumbani kwao. Nadhani alikuwa sahihi lakini, maana kuishi chumba kimoja na dada yako na wote mkiwa watu wazima ni changamoto. Lazima kuweka tahadhari, vinginevyo unaweza kumkuta nduguyo anavaa nguo, au ametoka kuoga, ikazua kizaazaa!

Loh, kwa haraka Sana, Siwema akatoka na kuingia chumbani kwao. Maana chumba cha kaka yake kilikuwa unatoka kwangu unaingia kwao. Daa! Hivyo ndivyo nilivyookoka na lile jaribio la Siwema..

Basi nikaendelea zangu nikipiga hatua moja baada ya nyingine, nikimwacha Siwema anasikitika, nikawa nazitoa headphones shingoni na kuzipachika masikioni. Hatua kwa hatua nikawa nasikiliza makala hamasishi kutoka kwa mhamasishaji maarufu huko Marekani mwenye asili ya kiafrica, Les Brown. Hizo ndio mambo zangu. Napataga maujanja mengi sana kwa kuwasikiliza hawa motiveshono spikaaz na ndio maana mimi mwenyewe nipo vizuri kwenye uwasilishaji hoja.


Haukupita muda mrefu, nikawa naingia pale chuoni, nikajichukulia maji kubwa kwenye duka, nikabugia nusu yake kwa mkupuo, maana joto la jiji hili si la kitoto. Baada ya kuridhisha kiu yangu, nikafuta jasho usoni kwa kitaulo kidogo cha mkononi, nikaanza kushuka taratibu kuelekea kule Hall 3. Pale kuna viunga vya nyasi maridadi sana ambako mara kadhaa mimi na Hellen hukutana na kupata faragha ya kuzungumza mambo yetu kama wapenzi.

Najua unajiuliza tulifikiaje kuwa wapenzi baada ya lile busu la kushitukizwa sivyo? Haha. Mapenzi yaache yaitwe mapenzi bwana.

Ilikuwa hivi.


Itaendelea….


6

Baada ya kuachwa pale na Hellen nikiwa nimeduwaa napunga mikono hewani kama zuzu, hatimaye nikashangaa kuna mtu anaishusha mikono yangu chini kwa nguvu.

'Oya, acha ubwege wewe. Unampungia nani mikono sasa? Haha!' Ilikuwa sauti ya rafiki yangu Issa Kalinga.

'Haha, kwani hujamuona yule mtoto mzuri aliyekuwa ananipungia mkono?' nikaongea huku nikimwonyesha kule alikokuwa ameelekea Hellen. Mara kule napomuoneshea, akawa anatokeza madam Bernadette, huyu ni professor wa lugha za kigeni hapa chuoni.

'We usinambie unatoka na profesa, kijana ume-advance sana kama unaweza kuwa unatoka na hadi maprofesa.' Isa akaendeleza utani.

'Sio huyo bwana, enewei, forget about it. Enhe nambie, hivi yule mtoto white alijipa?' Nikamtupia swali katika kujaribu kuua soo.

Issa ni mtu mmoja anapenda sana gymnastics. Yeye anajua kucheza karate, Judo na kungfuu. Yeye anaishi mabibo hostel block D. Ni wale Jamaa ambao ukiingia room kwake, huko unakuta amejaza DVD za mapigano ya kina Jet Li, Bruce Lee, na wakali wengine wa kungfu. Ukitoka hapo, utamkuta kwenye muvi za kihindi. Hizo ndio aina ya muvi anaangalia. Sasa, kutokana na hulka hiyo, yeye huvutiwa zaidi na mabinti wanaopenda mazoezi. Mwaka jana kabla sijaondoka Mabibo hostel na kupanga huko Changanyikeni, tulikuwa sisi ni watu wa shato pori (kutembea kwa miguu). Kwa maana ni mara chache sana tulipanda shuttle za kubeba wanafunzi kutoka Mabibo hostel kwenda mlimani. Hatukuona haja ya kufuja fedha kila siku kwa umbali ambao tungemudu kutembea kwa miguu. Kwa hiyo, tulikuwa tunapiga misele, tunakatiza mitaa kwa mitaa kutoka Mabibo hostel hadi chuoni, mlimani. Hasa sana muda wa kutoka chuoni jioni. Asubuhi kuna wakati una kipindi cha saa moja, inakulazimu kuwahi kwa kupanda shuttle. Lakini kama kipindi kinaanza saa mbiIi, tatu au nne huko, tulikuwa tunaenda kwa shuttle pori, yaani miguu yetu.


Sasa, jioni moja tukiwa mdogo mdogo kurejea Mabibo hostel, mitaa ya swimming pool, tukamuona dada mmoja hivi white anapiga mazoezi peke yake. Dah Issa akachanganyikiwa kabisa. Akanambia

'Oy, yule mtoto namuona leo mara ya pili. Kama vipi we tangulia ngoja leo nimpe hai mtoto mkali. Hawa ndio mademu smarter.'


Basi mimi nikaendelea zangu nikimwacha Issa akimfuata white. Hilo ndio jina tulilokuwa tunamwita mrembo yule kwa vile hatukujua jina lake. Baadaye, tulikuja kujua kuwa anaitwa Irene.

Huyo ndio nilikuwa nimemuulizia habari zake katika kuua soo la kunibamba kwenye pumbazo langu kwa mtoto Hellen.

'Anakataaje sasa.' Isa aliongea kwa majivuno na hapo ikawa kama nimefungulia redio, maana jamaa kwa kuongea, dah. Jamaa akatiririka maneno hadi ikawa simsikilizi tena bali naelea kwenye mawazo yangu juu ya mtoto Hellen. Baadaye tukaachana na Issa akaelekea zake Mabibo na mimi nikapandisha zangu Changanyikeni mdogo mdogo.


Jioni ya siku hiyo ya kubusiwa na mtoto Hellen, nikiwa zangu Changanyikeni, simu yangu ikapata ugeni wa meseji. Nilipoikamata, nikaangalia ujumbe ule, ulikuwa umetoka kwa Hellen. Nikajikuta natabasamu.


'Mambo Derick, Kesho jumamosi una ratiba gani? Nataka nikualike kwenye semina ya ujasiriamali'

'Nitakuwa free tu, muda gani?' nikajikuta nimeshajibu tayari bila hata kuwaza. Ukweli ni kwamba, siku hiyo ni siku ambayo mimi hukutana na my babe, Welu. Yule wa Duce. Lakini kwa siku hiyo nilikuwa nimemjulisha Welu kuwa ilikuwa nihudhurie kwenye harusi ya braza mmoja anaitwa Toma, ambaye alinipa kadi ya mwaliko licha ya kuwa sikutoa mchango wa harusi. Kwa kweli kipindi cha uchangiaji, nilikuwa na hali ngumu sana mfukoni, bumu lilikuwa limekata na nilikuwa naishi kwa kumpiga mizinga mama. So sikuchangia lakini braza akaamua kunipa mwaliko hivyo hivyo, nahisi alijua ni ukata maana yeye alikuwa kamaliza chuo miaka miwili iliyopita. Hivyo, mimi na Welu ambaye nilikueleza anasoma Duce, hatungeonana wikend hii. Maana yeye pia alinambia alikuwa aende nyumbani kwa shangazi yake jumapili, pale Kurasini, Shimo la udongo.


Kwa hiyo, ujumbe wa Hellen ulinifanya nipotezee kabisa ratiba hiyo ya harusi ili niende naye huko kwenye semina. Nikahisi hii ni fursa ya kujiweka Karibu na Hellen. Amin, sikuwa na dhamira yoyote ya kuanzisha mahusiano naye, bali kuna vile unajikuta under someone's spell (yaani kuwa kama zuzu). Nilijikuta tu natamka kukubali bila kuishirikisha akili yangu. Haikuwa poa, maana nilipokutana na braza Toma wiki mbili baadaye, alinimaindi kichizi.

Itaendelea..
FB_IMG_1613618969482.jpg
 
HELENA SIMULIZI YA HUBA 07
DAVID NGOCHO SAMSON

7

'We dogo unadhani maisha umeyapatia sana, siyo? Huwezi kushiriki kwenye shughuli za wenzio, siyo? we ngoja nawe utafikia hatua hizi!! Upo jijini, tena wikend unashindwa kuhudhuria harusi yangu?' dah, braza Toma alinimaindi sana. Enewei tuachane na habari za braza Toma. Ujumbe wa Hellen uliingia kwenye simu yangu kunipa maelekezo zaidi baada ya kumuuliza semina hiyo ingefanyika muda gani.

'Kuanzia saa nne hadi saa nane hivi. Lunch itakuwepo free na eneo la semina ni Millennium tower- makumbusho' ulisomeka ujumbe wake. Nikasema poa. Nitaenda na Hellen.

'Poa, tutaonana wapi?' nikatuma ujumbe huo.

'Tukutane kwenye ATM machine za NBC Karibu na cafeteria.'

'Fine' nikamjibu. Basi ikawa hivyo.

Usiku kwenye saa nne hivi, nikapata ujumbe tena kutoka kwa Hellen.

'Mambo Derick?'

'Poa, nambie Hellen!'

'Poa. Ushalala?'

'Hapana bado sijalala.'

"Unafanya nini?'

'Nipo nacheki muvi, wewe je?'

'Ah mi nipo nachati na wewe'

'Kabla ya kutuma message ulikuwa unafanya nini?'

'Nilikuwa nafuatilia mahubiri ya TB Joshua.'

'Anhaa, sawa sawa. Kumbe wewe mlokole eeh?'

'Ndio, nimeokoka na nampenda Yesu.'

'Bwana Yesu asifiwe mpendwa.'

'Amen, vipi wewe unasali wapi Derick?'

'Mh, dah nina kamuda sijaenda kanisani. Naomba nisikudanganye bure mtoto wa Mungu.'

'Sisi sote ni watoto wa Mungu, Derick.'

'Yeah, I guess you're right'

'Yeah, we all belong to him'

'I agree'

'Enhe so, nikupitie jumapili twende church?'

'Ah let me be honest. Umenishtukiza mnoo'

'Haha ok.'

'Yeah'

'So, I can't wait to see you tomorrow tukienda kwa semina.'

'Yeah Mimi pia, I hope soon nita-join club yenu ya wajasiriamali.'

'You're warmly welcome. Asante kwa kunipa muda wako Derick.'

'Don't mention it, kwa mtoto mzuri kama wewe hata bahari naweza kukumilikisha'

'You are very funny Derick'

'You sure?'

'Haha, Derick bwana. Sleep tight, ok?'

'And you, sleep loose, haha'

'Hahaha'

'Asante'

'Mh Asante ya nini, Derick?'

'Hujui tu usiku wangu utakavyokuwa murua'

'Kiaje'

'Sio kila mwanaume anapata fursa ya kupewa usiku mwema na mtoto mzuri kama wewe.'

'Niache nilale bwana'

'Didn't think I held you'

'Derick'

'Naam'

'Usiku mwema ee'

'Asante Hellen na kwako pia. Naomba nikuote ee'

'Ruksa!'

'Thank you.'

Basi Ilikuwa burudani kuchati na Hellen. Actually huo utani niliokuwa nachomekea kwenye chat na Hellen niliufanya tu kama utani. Sikuwa namaanisha chochote kitu, hasa baada ya kubaini mtu mwenyewe ni mcha Mungu. Nadhani nilikuwa nataka tu kuona mwitikio wake unakuwaje hasa baada ya kunibusu vile mchana. Nafahamu watu tuna makuzi ya tofauti tofauti, kwangu mimi ah, haya mambo ya kubusiwa nilifanyiwa nikiwa mdogo. Walikuwa wakubwa wakinibeba, utasikia 'hujambo totoo', basi wananizawadia busu shavuni. Na dada yangu Sarah, yeye alikuwa ananikomesha kwa mabusu motomoto yale ya 'abrurrr' tumboni. Basi burudani sana maana hapo ningecheeka hadi nitokwe machozi.

Kwa jinsi nilivyomuona Hellen, alikuwa ni mtoto wa kishua. Nikajua kabisa kwamba, hata lile busu aliloniachia mchana, ilikuwa ni mambo ya kawaida huko ushuani. Mtu akifurahi anatoa busu na inakuwa imeisha hivyo. Pia nilipojaribu kukokotoa kwa kina, nikajipa majibu mwenyewe, lile busu la Hellen la mchana, bila shaka ni busu takatifu la kipendwa la kusema Asante. Nikajisemea kimya kimya 'amen'. Nikatafakari kwa upande wetu waswahili, dah, sisi waswahili buana, ukipewa busu unadhani kuna kitu kinatokota nyuma ya mapazia.. Utani wangu hata hivyo ilikuwa kumpima tu nione kama ni easy target audience la!. Kama ambavyo umeona chat yetu hapo, huwezi kujua kama mtoto amejipa au la! Maana chat na maneno yake yapo kimtego sana. Hata hivyo, wala sikuwa na nia kabisa ya kumwingiza kingi. Lakini kuna namna nilikuwa nafurahia sana ukaribu wetu huu uliokuwa umeanza kuchipuza. Kuna namna nilikuwa nahisi upweke nisipomuona. Kuna vile aliishughulisha akili yangu kila mara. Nililala nikiwa na tabasamu usoni.


Jumamosi asubuhi nilimpigia simu Hellen.

'Good morning mrembo' nilimsalimia Hellen halafu kabla hajaitikia nikakumbuka huyu ni mtoto wa TB Joshua, haraka sana nikaongezea

'Bwana Yesu apewe sifa'

'Amen Derick, umeamkaje?'

'Salama tu mpendwa.' nikajibu na kumwachia nafasi.

'Mimi pia nimeamka salama.' Hellen akajibu. Nikagundua nilikuwa nimeishia njiani. Nilipaswa kumuuliza ameamkaje.

'Hellen, about the seminar later in the day…'(kuhusu semina ya ujasiriamali hapo baadaye….) nilikuwa naendelea kuongea alipodakia na kutamka;

'Please, don't tell me you won't make it!' (tafadhalali usinambie huji) aliongea kwa masikitiko tayari.

8

'Noo, on the contrary, nimepania kweli kweli kuwepo. Nimepiga ili unifahamishe dress code (uvaaji) ya event (tukio).' nilimweleza nikimalizia kwa kicheko laini. Nina kicheko laini, ambacho hukitumia kwa nadra sana hasa baada ya kugundua ndicho kilichomvutia mpenzi wangu Welu hapo awali wakati namlia mingo. So huwa nakitumia sparingly (kwa nadra) maana kinaweza kuwa na madhara makubwa kwa watoto wa kike. Na hapa nilikitumia kwa kusudi, nione matokeo yake kwa Hellen. Nachompendea Hellen, ni wa kishua sana. Unajua utofauti wa mtoto wa kishua na mtoto wa kiswazi ni ile openness(uwazi). Mtoto wa kishua yupo huru sana kujielezea hisia zake. Na huwa wanafanya hivyo without second-guessing (bila kujiuliza-uliza). Kwa hivyo nilipomaliza tu kukitoa kicheko laini, nilijua kama amevutiwa nacho lazima atasema. Kweli bwana, nikasikia.

'Oh oh Derick, napenda vile unacheka. You sure are blessed with many things. By the way hakuna dress code wala cha nini. Just wear casually, ukiwa comfortable ni muhimu zaidi, so vaa vile utajisikia peace.' alinambia akimaanisha nimebarikiwa vingi, na akanisisitiza kuvaa vile nitaona niko poa.

'Right, basi sawa.' nikatamka halafu nikasikia tena.

'So, umeamua utavaaje D?'

'Ah, niko na suruali ya jinzi la bluu, na juu nitaning'iniza fulana ya kijivu. Kama kawaida yangu, sichomekeagi.'

'Anhaa, great. Don't forget ni saa nne hadi nane so ukianza safari saa tatu itakuwa vizuri tusijekwama kwenye foleni.'

'Yeah right, baadaye!'

'See you!'


Saa tatu na ishirini hivi, nilikuwa kwenye ATM machine za NBC maeneo ya cafeteria nimetulia nasikilizia motivation speech kutoka kwa mwanagenzi Joel Nanauka. Huyu ni mbongo mwenzetu ambaye niliamua kumsikiliza baada ya kusoma wasifu wake mahali, kuwa alikuwa Tanzania one kidato cha nne halafu chuo kikuu akabamiza gpa ya 5. Imagine. Hizi ni mambo zangu kabisa. Kubamiza ma-gpa mazito mazito. Kwa mfano, last year niligonga gpa ya 4.8 kuingia mwaka wa tatu, na huyu mwana ikaonekana sijamfikia bado. So nilitaka nimsikilize nigundue genius yake. Yap, mwana yuko vizuri sana.

Wakati naendelea kusikiliza madini anayomwaga mkali, nikahisi mtu ananigusa begani, maana nilikuwa nimekaa kwenye ukingo wa barabara inayoshuka kuelekea cafeteria. Nikanyanyua macho juu na kumuona Hellen. Wow, mtoto alikuwa mpya. Alikuwa kamechisha nguo zake na zangu. Skirt ya Jeans bluu na fulana ya kijivu. Alipendezaje?

'Oh Hellen you look mwaa!' nilimweleza.

'Hiyo mwaa ndio gani Derick?' akaniuliza kwa sauti fulani hivi. Mtoto ana sauti huyu! We acha tu.

'Namaanisha you look delicious, edible na makila kitu.' nilimtania nikiwa na maana kuwa alipendeza na kuwa mtamu.

'Haha, acha mambo zako Derick. Twende zetu.' alitamka huku ananishika mkono na kunivuta taratibu. Wallah kidogo niruke, maana nilihisi kitu kama shoti hivi. Wee, Ni noma wazee. Basi mdogo mdogo nikawa nashuka na mtoto wa kishua hand in hand. Sometimes ile kutembea na mtoto mkali barabarani na wana wakaona na kuwatumbulia mijicho, hua ni ufahari sana. Sure, maana kuna wana wanaishiaga kuwaona watoto wa kishua kwa mbali. Nikiwa nipo mdogo mdogo tukielekea kwenye barabara ili kupata usafiri mara nikasikia sauti nayoijua vema. Ah kudadeki! Nikajikuta nafyumu kishenzi. Hakawii kuniharibia mtoko huyu mwana.

'Oya Derrick, vipi mwanangu nimetuma maesemues (sms) kibao hureply, kulikoni?' ilikuwa sauti ya Issa.

'Oy niaje, dah itakuwa nilikuwa mbali na simu.' nikaongea naye huku nikimpa ishara kwamba aniache kidogo maana nina mtoko na mtoto mkali wa kishua. Jamaa aliona, lakini huyu mwamba anakuwaga na mambo ya ajabu sana sometimes. Yaani ile kuzingua kwa makusudi. Na hapa alitaka tu nimu-introduce kwa mrembo. Kwa hiyo alikusudia kujongea tulipo.

'Mambo vipi?' alimpa hai Hellen.

'Poa. Habari yako?' Hellen akajibu.

'Njema.' Jamaa akajibu. Nikaona hapa ndio pa kuweka mstari. Issa namfahamu. Ana ujinga mwingi sana.

'Mpendwa Hellen, huyu ni my best friend anaitwa Issa. Issa, this is Hellen. Mtu wangu wa nguvu'

Niliongea kuwatambulisha.

'Oh nice to meet you!' Hellen Alizungumza.

'Oh mtoto anazungumza kinge!!. Wow, nice to meet you too.' lijamaa likanyoosha na mkono. Dah nilitaka niupangue lakini nikaona itakuwa Soo, so nikavunga.

'Kwa hiyo ni mtu wa nguvu siyo, hebu nyoosheni maelezo bwana.' Issa akaongea huku anatutazama kwa zamu. Nikaona huyu mpuuzi anakusudia kukitia mchanga kitumbua changu. Nikaona nimuondolee uvivu.

'Ah we jamaa, baadaye kwanza. Tunahitaji kuwa mahali mida hii.' niliongea kwa msisitizo.

'Wapi tena?' Jamaa akauliza kwa lafudhi ya kimwera, watu wa kusini huko.

ITAENDELEA..
FB_IMG_1613619817199.jpg
 

Attachments

  • FB_IMG_1613619797151.jpg
    FB_IMG_1613619797151.jpg
    27.9 KB · Views: 12
HELENA SIMULIZI YA HUBA 09
DAVID NGOCHO SAMSON
0629077792

9

'Tunaenda semina Issa. Are you interested?' Hellen akaongea. Ah, nikaona jamaa ametibua mchongo. Nikamkazia macho kuonesha kwamba nataka atoe udhuru. Lakini jamaa kama kawaida yake kuharibu mipango, si akakubali bwana!! La la la! Nilifyumu kishenzi yaani. Yaani nilijikuta naishiwa pozi kabisa. Basi tukachukuwa bajaji hadi mlimani city, jamaa akiwa ametawala mazungumzo. Mimi kimya, na nikagundua Hellen pia alikuwa anafanya kuitikia tu almradi. Issa ni aina ya watu ambao, anaongea non stop, yaani mfululizo na bila kuchoka. Wale ambao anataka anapoongea uwe msikilizaji tu, yaani akiona kama unawaza kingine basi aidha ataendelea kuongea huku anakugusa gusa au hata kukufinya. Unaweza ulale usingizi wa nusu saa yeye akiwa anasimulia ukaamka jamaa bado anaendelea kuongea hadi midomo imkauke na povu pambizoni mwa midomo lionekane na wala asichoke. Cha muhimu wewe uoneshe kuitikia. Na mara moja moja uchomekee maneno mawili ya kumchaji, basi mtakesha usiku kucha na mshinde mchana kutwa jamaa akiwa bado anasimulia. Basi namna hiyo mshikaji akawa amezingua na kuharibu kabisa siku yangu.


****


Tulifika Millennium Tower mapema kabla ya ratiba kuanza. Tukakutana na wanasemina kibao, tukawa tunapeana hai na kuzungumzia mafanikio. Sijawahi kuona watu wenye mitazamo chanya kama wale ndugu. Ukiwasikiliza, hakika unayaona mafanikio 'haya hapa'. Ni watu fulani wenye utamaduni tofauti na ule wa mwananchi wa kawaida. Hawa jamaa naamini hata mbinguni wataingia. Wana imani thabiti sana. Ilikuwa ni semina ya biashara za network marketing.


Utaratibu wake sasa, kadri unavyoingiza watu na kutengeneza mlolongo mrefu wa minyororo ya watu chini yako, ndivyo unavyojikusanyia ukwasi. Kwa kusikiliza, inavutia mno. Kiujumla wanasisitiza zaidi utengenezaji wa mitandao ya watu kuliko uuzaji wa bidhaa. Kwa nini? Ukishakubali kuwa sehemu ya mtandao tayari ni bidhaa zinakuwa zimeuzwa. Shida ni kuwa bidhaa zao ni ghali mno. Halafu incentive nyingine hamasishi, wanakupa fursa ya kutalii dunia na kujumuika na watu kutoka mataifa mbalimbali ukiwa ngazi ya manager. Ni maisha fulani hivi yenye mvuto hasa kwa vijana dreamers(waotaji). Yaani watu wenye ndoto kubwa kubwa. Hawa jamaa, wanatengeneza fedha, hasa ukiwa kwenye ngazi za juu. Wana maisha fulani hivi ambayo wakikusimulia, utataka usichelewe kabisa. Utatamani ujiunge haraka ili uanze kuijongea ndoto yako ya kumiliki magari, majumba, safari nk.


Basi bwana, tulivutiwa kweli kweli na shuhuda na shawishi za wajasiriamali hawa. Na kwa vile tulialikwa na mtoto mzuri Hellen, ah mimi binafsi nikaona wacha niongezeke kwenye mnyororo wa watu wake. Nikajiunga chini yake. Nikitumia kabalance kote ka fedha za kujikimu nilikokuwa nalinda kama Roho yangu. Ilinibidi kutunga simulizi ya uongo ili kumpiga mzinga wa hela mamangu. Hata sijui nini kilinikumba aisee. Imagine nachomoa vijisenti vyangu na kuweka kwenye biashara ngeni bila kujihoji mara mbili? Nahisi mama anajuaga blanda zangu lakini daima hajawai kuniangusha. She is very understanding. Alinitumia fedha na maisha yakaendelea kama kawaida. Hiyo ilikuwa jumamosi. Na kusema kweli kwa uwepo wa Issa kati yetu, hatukuzungumza sana siku hiyo mimi na Hellen. Tulipiga lunch hotelini kama walivyoandaa wajasiriamali wa network marketing. Halafu baadaye tukageuza. Issa alivutiwa sana na ule mfumo wa biashara. Nadhani kutoka moyoni alidhamiria hiyo ndio ingekuwa njia yake ya maisha hata baada ya chuo. Nasema hivyo kwa sababu hata baada ya kumaliza chuo, yeye hakujihangaisha kabisa na mambo ya kutafuta ajira. Aliingia jumla kwenye biashara ile.


Usiku kama kawaida, Hellen alianzisha chat na mimi, tukazungumzia siku ilivyokuwa. Akanishukuru kwa kukubali kujiunga na network yake. Basi ikawa ni mwanzo mzuri wa kufanya biashara kati yangu na yeye, lakini pia kufahamiana zaidi.


10


Kesho yake ilikuwa jumapili, nikiwa nimeamka asubuhi mapema nilikuwa nimejitengenezea chai naendelea kunywa taratibu huku namsikikiza Robert Kiyosaki kutokea kwenye sub-woofer langu. Ilikuwa saa mbili. Nikaona ujumbe kutoka kwa Hellen.

'Mambo Derick?'

'Poa, Hellen nambie mpendwa. Hapo utakuwa unaelekea zako church bila shaka?.' nilimjibu na kuhoji.

'Ah hapana. Leo sipo vizuri kabisa.'

'Oh, unaumwa Mpendwa?'

'Hapana Derick, basi tu nina mawazo sana'

'Dah mpendwa, pole kwa yote. Kama unahitaji mtu wa kuzungumza naye, talk to me!' nilimweleza.

'Uko wapi Derick?

'Niko Changanyikeni dear friend. Karibu ukitoka church tuongee. Wanasema kuongea na mtu inasaidia kupunguza stress.'

'Kwa kweli sidhani kama nitaenda church leo. Kama uko free basi nakuja!'

'Yeah, nipo free Hellen na kwa kuwa ni wewe, there is always a room for you!' nilimweleza.

'Ok. Basi nachukua bajaji, utamuelekeza dereva.'

'Haina taabu. Ukishampata mpe simu niongee naye.' baada ya kuongea na Hellen na kujua anakuja, mwanaume nikasimama fasta na kuanza kudeki chumba. Nikaondoa shuka na kutandika safi, nikafuta futa vumbi maeneo eneo, halafu fasta sana nikamwagiza mtoto wa jirani tunamuita Justine akanichukulie kilo moja ya nyama, maziwa na chapati kadhaa na matunda na nikamsisitiza arudi na chenji. Nilikadiria kwamba Hellen atapata kifungua kinywa hapa, kwa hiyo nilikusudia kuandaa chai ya maziwa. Halafu mchana tungekula wali nyama. Nilijua jioni hatakuwepo hapo ghetoni kwangu. Nikazama bafuni na kuoga. Ile narudi ndani kutoka bafuni, nikaona simu inaita.

'Yeah, nambie mpendwa.'

'Huyu hapa dereva.' Hellen akaongea akimkabidhi dereva wa bajaji simu yake.

'Tupo hapa Changanyikeni sokoni' Alizungumza dereva. Basi mie nikamwelekeza vizuri nikawa nawasubiri.

Inavyoonekana, dereva maelekezo yangu hakuyapata vizuri, ikabidi aulizie jina la mwenye nyumba wangu kama nilivyomweleza. Uzuri akamuuliza Justine ambaye tayari alikuwa keshafanya manunuzi niliyomuagiza. Dogo janja Justine akawaambia twende niwapeleke. Akazama kwenye bajaji akawaleta hadi mlangoni. Akanikabidhi bidhaa na mgeni wangu.

'Oh, kumbe unaishi hapa?' Hellen akamuuliza Justine kwa mshangao.

'Ndiyo' Justine akajibu huku anatabasamu mwenyewe.

'Oy, chenji yangu?' nikamshitua Justine wakati anataka kusepa.

'Ah nilikuwa nimesahau kaka.' akasema huku anaingiza mkono mfukoni. Akajifanya anaitafuta wee.

'Ah, kaka sijui nimedondosha? Niliweka humu.' nikajua dogo analeta usanii.

'Dogo, jero kubwa hiyo!' nikamwambia.

'Ah, hii hapa, ilikuwa imebana kwenye kona.'

'Haya basi, hiyo itakufaa mdogo wangu. Asante kwa kuniendea sokoni.' nikamwambia Justine nikimwachia ile mia tano.

'Asante kaka.' Justine akaongea huku anaachia tabasamu na kupotea.

'Derick, umemhangaisha hivyo na ulikusudia kumwachia?' Hellen aliniuliza.

'Ee, ndio namfundisha kwamba uaminifu ni muhimu. Sasa hivi ataitumia hiyo pesa kwa amani bila hofu kwamba ataulizwa ameitoa wapi. Atakuwa na ujasiri wa kusema kaka aliniagiza halafu akanipa hii kama shukrani.' nilimweleza Hellen halafu nikamkaribisha ndani.

'Karibu sana Hellen. Nimefurahi sana kukuona.'

'Mimi pia Derick. Asante sana.'

'Ah utanisamehe, ghetto langu sio kama la mangwea, lipo kishikaji tu, kusaidia kusukuma siku mbele tumalize chuo.'

'Mangwea ndio nani tena Derick?'

'Ah, huyo alikuwa ni msanii wa bongo fleva enzi za uhai wake. Kuna ngoma alitoaga inaitwa gheto, analisifia gheto lake lilivyo bomba. Na ambavyo linampatia mademu wakali sampuli yako.'

'Mh, haya bwana. Mimi na bongo fleva wapi na wapi?'

'I understand, wewe na Rose Mhando sawa, kwenye utamu wa Yesu ndio unaelewa zaidi sivyo?'

'Haha Derick uko na utani mwingi sana. Umeona kwenye utamu tu? Actually mimi napendelea zaidi nyimbo za kuabudu kama zile za Upendo Nkone na Upendo Kilahiro. Na zilizochangamka, napendelea za Angel Bernard. Otherwise, napenda zaidi gospel za nje. Za kina Don Moen, na wengineo.'

FB_IMG_1613619797151.jpg
 
HELENA SIMULIZI YA HUBA 11
DAVID NGOCHO SAMSON
0629077792

11

'Wow? Kwa hiyo hawa wakina Martha Baraka huwapendi kivile?'

'Nawapenda wote, ila ladha ya miziki nayopenda mimi siyo wanayofanya wao.'

'Yeah I got you. Wacha nikuandalie chai kwanza mpendwa halafu utanifundisha namna ya kutambua ladha ya muziki!' niliongea huku natabasamu. Hellen akajikuta anacheka na kunipigapiga ngumi dhaifu mgongoni. Nilikusudia kumsahaulisha kabisa ishu yake hiyo iliyokuwa inamtia stress na wala sikutaka kabisa tuizungumzie. Nilishaga jifunza, kwamba kitu kinapokusumbua, kadri unapokipatia makini yako, kwa kukiwazia au kukizungumza, ndio unakipa nafasi ya kukuvuruga zaidi. So, mara nyingi janja yangu ya kudili na stress ni kuzipuuza na kuendeleza mambo yanayonipatia furaha zaidi. Nilishajifunza kwamba, sio rahisi kupendeza kila kitu au kumfurahisha kila mtu. Kuna watu kwa mfano, unapotafuta sana kuwafurahisha ili wakupe umakini wao, ndivyo unavyowakera zaidi. Kuna wengine kadri unavyoonekana kuwepo sana kwenye upeo wao, ndivyo wanavyokuchukulia poa na kupoteza thamani yako. Hivyo, kuna wakati unatakiwa usome mazingira, unapotea kwenye upeo wao kwa muda fulani hadi wajihisi kuna kitu kinakosekana kwenye maisha yao na wagundue kwamba uwepo wako ndio kitu kinachomisi ili watambue thamani yako. Halafu, kuna wakati wale uliowashobokea sana wakakudharau unatakiwa usitishe shobo na uwaoneshe kwamba ulikosea kuwapa thamani ile ambayo hawakuiona. Hapo ndipo watakapogundua kuwa kumbe kuringa kwao na kujipandisha hadhi, ilitokana na wewe kuwashobokea sana, hadi watamani kukuona ukiwapa ile hadhi na wao wakikupa thamani unayoistahili.


Ujio wa Hellen jumapili hii ulinipa fursa ya kumfahamu vema. Na nilijitahidi sana kupunguza ule utani wangu wa kimapenzi ili nisije kumtia kwenye vishawishi potofu mtoto wa watu. Pamoja na kuwa nina madhaifu yangu, lakini sipendi kabisa kujaribu kutikisa imani ya mtu. Na hivyo, nilikuwa mtoto mzuri sana jumapili hii. Tukawa tunazungumza habari njema za injili. Hellen yupo vizuri sana kwenye imani. Kabisa. Lakini, kwenye suala la mapenzi, hata mwenye Imani huanguka. Nadhani hicho ndicho kilichotokea. Tulipika, tukala, Tukapiga story na kucheki movie, muda nao ulikuwa unasogea. Ikafikia kwenye saa kumi na mbili jioni hivi, tukawa tumechoka. Basi ikabidi tujipumzishe kidogo na kuruhusu usingizi utupitie kiasi. Nilijaribu kuweka nafasi kati yangu na yeye, na uzuri kitanda changu cha sita kwa sita kilitoa mwanya wa kuwepo nafasi ya kutosha. Wakati kausingizi kananibeba nikahisi kama Hellen amenisogelea zaidi. Nikaamua nijisogeze taratibu bila kumshitua usingizini na jinsi alivyolala, kwa kweli sikutaka niendelee kumwangalia kwa sababu nilihisi kabisa nitajikuta kwenye dhambi. Basi ile kwamba nijisogeze, Hellen alivyogundua nataka kumhepa, basi ndio kabisa akafanya makusudi ya kunikumbatia kwa mkono wake. Oh Lolo yaye! Mwili ulinisisimuka vibaya mno. Lakini nikajikaza na kutulia tuli. Mara, nikahisi mkono wa Hellen unanitembea kifuani taratibu. Loo! Hali ikawa si hali. Mnara wa babeli ulikuwa unanyanyuka na kuvuruga kabisa lugha ya maelewano. Mwishowe nikaona ah, isiwe tabu. Nikauruhusu upande hewani kwa kadri ulivyotaka.

Mkono ule uliendelea kutalii mwilini mwangu na kunipa wakati mgumu, maana Mimi mwenyewe nilikuwa nasita sana kufanya kitu chochote. 'Ah kudadeki wallahi, huu si ubwege huu!' nilijiambia nafsini. Mtoto anataka na ameonesha njia bado naendelea kujifanya sielewi? Ah, nikaona isiwe tabu. Wakati huo mkono wa Hellen ulikuwa umeufikia mnara wa babeli na kuanza kuupapasa kwa uchu. Nikasema wacha nijibu mashambulizi.

Nikanyoosha mkono kifuani kwake na kuanza kuzipapasa taratibu embe dodo. 'Ah haa' nikasikia Hellen anatoa sauti ya mahaba, miguno ikamkolea zaidi nilipofanya matembezi kwenye kisima cha malkia. Dah, haya mambo buana nadhani hayana mjanja. Hatua moja hupelekea nyingine, shika hapa nishike pale, tomasa huku nitomase hapo. Mihemo ikabadili spidi. Mabusu yakatawala uwanja, Mizuka ilipozidi, nikataka kupima kina cha maji kwa mtarimbo. Wala malkia hakuweka pingamizi, aliniruhusu niuchomeke mtarimbo kisimani, lakini kabla sijafika kwenye kina chake, naona akabadili mawazo. Haraka sana akasimama na kutoa mtarimbo kisimani akajiweka sawa haraka haraka, huyo akatoka bila hata kuniaga. Nilijisikia vibaya sana. Mbaya zaidi, aliamua kuzima simu usiku wote. Loh!

12

Kitendo cha yeye kuamua kuondoka vile, kwa kweli kilinitia hatiani mno. Nilibaki najilaumu na kusikitika sana kwa kitendo kile. Nikajiona mwenye dhambi mno kumweka binti yule kwenye majaribu kiasi kile. Kitu pekee nilichokuwa nahitaji muda huo, ilikuwa ni msamaha tu. Lakini ndio hivyo, hakunipa nafasi ya kulifanya hilo, na akanichanganya zaidi alipoamua kuzima simu nisimpate hewani. Aisee nilijutia sana kitendo kile. Ajabu kuwa nilikuwa pia najiweka kwenye hatari ya usaliti. Ilikuwa nimemsaliti mpenzi wangu Welu kwa mara ya kwanza ingawa kwa kiasi kidogo maana ni kama tulifikia mlangoni na ilikuwa kidogo tu tuingie chumba cha usaliti.

Hofu yangu kubwa pia ikawa kwamba, kwa jinsi Hellen alivyokuwa mtu wa dini, asije akafunga na kuomba akinishitakia kwa Mungu kwa kuruhusu shetani atupitie. Kwa kweli nilikuwa katika hali mbaya sana kisaikolojia. Nilijikuta naanza kutubu madhambi yangu, nikawa namuomba Mungu ampe Hellen roho ya kusamehe.


Hofu nyingine iliyonikumba ni kwamba sikujua Hellen amelichukuliaje suala lile. Na haya mambo ya haki za wanawake duniani, na jinsi wanavyopewa kipaumbele kwenye sheria, nikawa nawaza, hivi akisema nilimrubuni na kujaribu kumbaka nitajiteteaje? Ah! Sikulala vizuri kabisa siku hiyo. Nilimlaani shetani na ukoo wake wote kwa kuniweka kwenye kona mbaya kiasi kile. Nilihitaji mtu wa kunipa neno la tumaini na kuniondolea hatia. Kwa kawaida, Welu alilibeba vema jukumu hilo, lakini hapa naanzaje kumpigia simu kumweleza haya yaliyonisibu bila kumkosea?

Ah acha aisee. Hapa ndio pale unapotamani umwambie mpenzi wako jinsi mchepuko unavyokunyanyasa. Lakini hapa wala hapakuwa na mchepuko. Hatukuwa tumekubaliana chochote cha vile na Hellen. Jambo lile lilitaka kutokea kwa kutokea tu bila ruhusa yetu wawili. Au tuliruhusu bila kujua? Sasa kwa nini akimbie? Au alijikuta anakumbuka ghafla kwamba ni dhambi ikabidi akimbie? Kufikia hapo nikajikuta naukumbuka mstari kwenye vitabu vya dini usemao, kuna dhambi zingine hukemei tu, bali unazikimbia kwa miguu kama alivyofanya Yusuf dhidi ya mke wa Potifa. Loh! Hapo ndio nikapata mwangaza. Kilichotokea, ni kwamba, Hellen aliamua kuikimbia dhambi. Oh! Nikaona afadhali hapo. Kama aliondoka kwa kusudi la kuikimbia dhambi, nikamuona ni mwanamke shujaa! Hellen alikuwa mtu wa Imani. Kuwa na imani haimanishi huwezi kujaribiwa. Infact ukiwa na imani ndio unajaribiwa zaidi. Kulishinda jaribu ndio kitu kinakufanya shujaa, sio kutokujaribiwa. Nilijikuta namheshimu sana Hellen. Hapo ndio nikapata na usingizi. Ilikuwa yapata saa nane za usiku nilipolala usingizi.


Kesho ya kuamkia usiku huo, Ilikuwa jumatatu na nilipaswa kuhudhuria mihadhara( lectures) chuoni kama kawaida. Niliamka mapema saa kumi na mbili asubuhi ili nioge kuwahi lecture ya saa moja asubuhi. Baada ya kujiweka safi na kupata kifungua kinywa. Nikiwa najiandaa kutoka, mara anaingia mtu ndani. Mlango ulikuwa wazi. Hey! Alikuwa Hellen!. Nikapigwa na butwaa. Sikutarajia hili na kama kuna kitu nilikuwa nawaza, basi ilikuwa ni baada ya lecture nimtafute kwa ajili ya kumuomba msamaha. Hapa nilibaki nimeduwaa sijui niseme nini. Nadhani yeye pia aligundua kwamba huyu ndugu ameduwazwa na ujio wake. Alinitazama usoni. Nikajaribu kutoa neno.

'I'm very sorry..,.' nilijaribu kutamka lakini sikuweza kumaliza. Maneno yangu yalikatikia njiani kwa sababu midomo ya Hellen ilikuwa sambamba na midomo yangu. Akili yangu iliyokuwa na majuto chungu nzima, kwa muda ilisimama, lakini kama kuna muda ilizinduka, basi ilikuwa imesahau yale majuto na sasa ilikuwa imeuamrisha mwili kufanya yale aliyotaka Hellen. Kwa maana sasa ulimi na midomo yangu vilionesha ushirikiano na alichotaka Hellen. Ile safari iliyokuwa imeishia njiani ile jana, ilianzishwa rasmi. Safari hii, ilianza kiprofesheni kabisa. Mimi nilikuwa nafuatisha kule alikokuwa ananipeleka Hellen. Ningekusimulia kilichofanyika lakini ikutoshee kujua kwamba pamoja na kuwa na mpenzi, lakini kwa Hellen nilikuwa nimeanza rasmi safari ya kujifunza mapenzi. Huyu alikuwa ni mwalimu wa mapenzi. Sikuhitaji tena mihadhara ya chuoni kwa siku hiyo. Niliamua mihadhara ya vitendo kutoka kwa Hellen Ilikuwa inanitosha kwa siku hiyo. Na si siku hiyo pekee. Kesho yake, keshokutwa yake, na hatimaye wiki nzima ilipita hatuendi chuoni kwenye mihadhara. Shetani mbaya nyie!! Mmsikiage tu

Itaendelea...
FB_IMG_1614266708456.jpg
 
HELENA SIMULIZI YA HUBA 13
DAVID NGOCHO SAMSON
0629077792

13


Sasa nikurejeshe Tena kwenye mawasiliano yangu na Hellen baada ya kurudi nchini. Kama nilivyokueleza mwanzoni mwa simulizi hii, kutoona ujumbe wa hr 301, kulimaaanisha Hellen anataka mimi ndio nimfuate, kwa hiyo nikawa nimeelekea zangu chuoni. Nilijua ni wapi pa kumkuta Hellen. Kwenye viunga vya hall 3 kwenye eneo ambalo mimi na yeye tulikutana mara kadhaa.

Nilimkuta Hellen ametandika kitenge chini amekaa anachezea tablet yake wakati akiendelea kuningojea. Oh, kwa wiki mbili nilizokuwa nje ya nchi bila Hellen, nilikuwa nimem-misi sana. Sana yaani. So nilipomuona pale chini, miguu iliongeza spidi sana kumwahi, midomo yangu ikiimba

'Waooo waoo!' Nikaona Hellen pia anashindwa kuvunga, akajinyanyua na kunikimbilia. Tulipokuwa hatua moja kabla ya kufikiana, tukaanza kucheza step yetu fulani' halafu nikamnyanyua juu Hellen wangu na kumkumbatia kwa nguvu sana. Ah, nilijisikia vizuri sana. Aisee, kukumbatiana kuna raha sana. Amini nachokuambia, kama wewe na mpenzi wako hamkumbatiani mara kwa mara, kuna mambo ya msingi mnayakosa kwenye penzi lenu. Anza mara moja kuwa unamkumbatia mwenzako. Angalau udumu kwenye kumbato lake kwa dakika moja. Ni nzuri sana kiafya.

Basi tulikumbatiana bila kusemeshana kitu kwa dakika moja na ushei hivi. Raha sana yaani. Halafu baada ya hapo tukatazamana usoni na kugusanisha pua zetu kwa mtindo wa kusigishana. Huu ni utaratibu wetu mimi na Hellen.

'Mambo mpenzi, nilikumisi sana laazizi, oh I real missed you.' nilimtamkia Hellen na kumkumbatia kwa mara nyingine tena.

Hellen akaibinya pua yangu na kuitikisa.

'Kama ungenimisi ungenitafuta first thing baada ya kurudi. Yaani kweli Derick urudi toka Kenya kwa ndege, upite airport, uende nyumbani na baadaye Changanyikeni, usubirie nikutafute ndio uanze kunambia ulikuwa unataka kunipigia? Nina mashaka na penzi lako. Au umepata mrembo mwingine huko Nairobi akakufanya unisahau?'

Alipomalizia kuongea hivyo akaibinya pua yangu kwa nguvu hadi nikahisi maumivu. Aliamua kuniadhibu nadhani.

'Hapana mpenzi, niamini. Simu ilizingua na hata hii ya kitochi nimeifufua baada ya kufika Changanyikeni.' nilijitetea.

'Mh, sa ntafanyaje? Nashindwa hata kukununia kwa jinsi nilivyokumisi Derick wangu. I'm happy to see you'

'Thanks darling. I'm happy to see you too. Nimekuletea bonge la zawadi. But hapa sijaja nayo. Ipo ghetto.!'

'Wow darling, Asante Sana mpenzi, can't wait to see it'

'You'll definitely see it babe. But why nilikusikia kama mwenye huzuni kwenye simu mpenzi?' nilimtupia swali.

'Siku hazilingani mpenzi! But let's forget about that for a moment now. I want to make love to you mpenzi. I'm all wet!' Hellen alitamka kwa sauti ile ya mahaba nikahisi kama imeamsha vitu fulani mwilini mwangu.

Alinivuta taratibu nami nikalazimika kumfuata. Tukaelekea chumbani kwao Hall 3. Haikuwa mara ya kwanza kufanyia mambo yetu room kwao. Ilipotokea hivyo ma-roommates wake waliachia chumba kwa muda. Walipigwa exile kwa muda hadi pale ambapo tungemaliza mambo yetu.

Tuliingia chumbani tukiwa tayari tumevurugwa. Nakumbuka hata kabla hatujaingia chumbani mle, tayari huku kwenye makorido tukikuwa tumeshaanza romance, na hata tulivyoingia ndani basi kazi ilianza mara moja. Wiki mbili za kuwa mbali mbali zilichangia kuwa na hali ile nadhani.

Hatukuridhika na hali hiyo. Tulipomaliza tu mzunguko wa pili, Hellen alinitaka twende sote changanyikeni.

***

Alimpigia simu mtu wa bajaji. Bajaji ikatuchukua mimi na Hellen wangu hadi ghettoni Changanyikeni. Nilimlipa jamaa wa Bajaj halafu sie tukaingia ndani.

Tulivyoingia tu, Hellen alitaka kuona zawadi niliyokuwa nimemletea. Sikutaka kupoteza muda, haraka sana nilivuta bag nikachomoa zawadi zangu kwa Hellen. Nilikuwa nimemletea zawadi aina tatu tofauti. Ya kwanza ilikuwa ni bracelet (kidani cha kuvaa mkononi), ya pili ilikuwa necklace (mkufu)wenye kidani cha madini ambayo muuzaji alinambia yanaongeza mvuto wa mapenzi, Sikumbuki jina la madini) na zawadi ya mwisho ilikuwa ni nguo za ndani zenye mvuto wa kimahaba yaani lingerie. Hizi nguo kawaida zinakuwa zinavaliwa chumbani kunogesha mahanjamu ya mapenzi.

Hellen alizifurahia sana zawadi hizo. Nikaona machozi yanamshuka bila hodi.

'Oh mpenzi, you are very sentimental (una hisia kali Sana)' nilimwambia. Nilihisi alikuwa analia kwa furaha. Ni kweli alilia kwa furaha, lakini kumbe kulikuwa mchanganyiko wa huzuni ndani yake.

Walisema waswahili usilolijua ni kama usiku wa kiza. Nilimsogelea karibu na kumkumbatia Hellen. Nadhani huzuni ilimzidia. Maana nilimsikia akitoa sauti ya kilio cha kwikwi. Taratibu nikaunyanyua uso wake na kumtazama usoni. Ajabu! Hellen leo ananionea aibu? Ama kwa hakika mapenzi ni mtihani sometimes. Nilimfuta michirizi ya machozi yake kwa kutumia kiganja cha mkono wangu. Uso mlaini, macho makubwa kiasi yenye mvuto, midomo minene laini inayovutia kimahaba. Ah, sijui hata ni muda gani tulianza kubusiana kwa hisia nzito. Kulikuwa na energy kubwa sana safari hii. Miili yetu Ilikuwa kama imechajiwa na nguvu ya umeme. Tulipoingia kwenye tendo, ilikuwa tofauti na siku zote. Ilikuwa na upekee. Wote tulikuwa na hamu na nguvu za ajabu ni kama mtu mwenye njaa anavyopewa chakula anavyokishambulia. Ilikuwa kama uwanja wa vita. Hatimaye tukapumzika.

Baadaye nikahisi mguso wa Hellen kifuani mwangu. Mguso huo ulifuatiwa na sauti yake nzuri na tulivu. Alitamka jina langu.

'Derick!'

'Naam mpenzi. Niko hapa kwa ajili yako sasa na hata milele' nilitamka

'Sitaki kuwa mbali na wewe. Sitaki kukuacha Derick' aliongea. Kidogo nilitafakari. Kwani alikuwa amepanga kuniacha?

'I'm not going anywhere darling. Kama unamhofia Welu, well don't. Hana shida na wewe na hatakaa ajue.' Uzuri ni kuwa nilikuwa nimeshamweleza Hellen uwepo wa Welu. Ndiyo, kwa sababu mapenzi yangu na Hellen yalivyoanza hayakutupatia muda wa kuelezana Historia na status zetu za wakati huo. So, baadaye niliona inaweza kuwa shida kama nisipomwambia kwamba kuna mtu alikuwa ananimiliki na yeye ameingia anga zake. Of course nilikuwa sina namna kwa vile sikuwa tayari pia kuachana na Welu wangu. Pia Sikujua kwa wakati ule kama kilichokuwa kinaendelea kati yangu na Hellen kina future gani. Sikutaka kurisk.

Nilijaribu kumtuliza.

'Kuna kitu sikukuambia Derick. Lakini naona ni muhimu nikuambie kwa sababu Niko tayari kubadili maamuzi kwa ajili yako.'

'Ok dear, I'm all ears (nakusikiliza)'

'My wedding day is due in a month time (tarehe ya harusi yangu ni mwezi mmoja tangu leo), lakini niko tayari kuachana nayo kama utaniambia kufanya hivyo'


Itaendelea...

14

'WHAT?' nilihamaki vibaya mno. Actually, nilichanganywa sana na kauli yake. Eti harusi yake inafanyika mwezi mmoja tokea leo? Sijui hasa ni nini kilikuwa kinaendelea kwenye hisia zangu.

Unajua, ukweli ni kwamba sikuwahi kumuuliza Hellen juu ya mahusiano yake kabla yangu. Hivyo, nilikisia kuwa alikuwa free, yaani single lady kabla ya kukutana nami. Sijui kwa nini hakunijulisha kama ana mtu hasa wakati mimi nilipokuwa namjulisha habari za Welu wangu. Tena wakati akijua sio mtu tu, eti mtu wake ni bwana harusi mtarajiwa!? Pata picha nilivyojisikia ndugu yangu msomaji. Nilihisi amenifanyia kitu kibaya sana. Ukweli ni kwamba, nilishaanza kumzoea na kujidai kwamba mie na yeye forever. Unapata picha?

'Unaongea nini wewe?' nilihoji. Uso wangu haukuwa ule wa mahaba tena. Nilikuwa nimefura kama nyoka aina ya cobra. Hasira zilikuwa zimenijaa kwa ghadhabu kubwa.

'Please darling, nisikilize babe' Hellen alinisisitiza kwa upole

'Nisikilize nini? Nisikilize upuuzi kwamba kwa muda wote huu ulikusudia kuchezea hisia zangu? Kwamba unaolewa na jamaa mwingine? What nonsense is that Hellen? Mbona hukunambia wakati mimi naropoka habari za Welu wangu?'

Kusema kweli. Nilikuwa nimeumia sana kihisia.

'How could I, babe?(Ningeanzaje mpenzi). How could I tell you about another man when I needed you badly?(Ningeanzaje kukueleza kuhusu Mwanaume mwingine wakati nilipokuhitaji zaidi?. Nisamehe mpenzi, nisingeweza. Sikutaka kukupoteza hata kabla ya kukupata. Sikutaka kukupoteza asilani. Niamini. Hata sasa sitaki kukuacha Derick. How can I be without you?(nitakuaje bila wewe). I can't fathom my love life without you!!' (sipati picha maisha yangu kimapenzi bila wewe)' Hellen alizungumza. Maneno yake yakazidi kunichanganya akili. Anataka nini? Nilijiuliza.

'What are you saying Hellen?'(unasema nini Hellen) niliuliza. Safari hii nikiwa nimepoa kabisa. Sikuwa na ujanja. Lakini pia nikitaka kufahamu nini hasa alikusudia kusema.

'Darling, my life, has always been a dictation. I want to own it now. (Maisha yangu yamekuwa ya kiimla kwa muda wote. Nataka sasa nishike usukani wake mwenyewe.) Ni story ndefu sana. Babe, nitakusimulia yote.' Alitamka akionekana kutopea kwenye kumbukizi nzito bila shaka.

'Nakusikiliza!' nilitamka kwa mkato, lakini ukweli ni kuwa nilikuwa nimenywea kabisa. Kwa mara ya kwanza, nilihisi wivu sana na sikutaka kabisa kumpoteza Hellen. Niliamua kumpa nafasi ya kuniweka sawa kama angeweza.

***

Wakati Hellen ananisimulia, nikakumbuka ile siku tuliyopaswa kukutana kwa ajili ya discussion. Siku ambayo hakuna mwanakikundi hata mmoja aliyetokea. Siku niliyojipatia kazi ya kuwabeba wenzangu kwa kuandaa kazi ile ya kikundi. Unakumbuka alinambia hakufika siku hiyo kwa sababu alikuwa kwenye kikao cha harusi? Basi ndugu yangu, kikao chenyewe kilikuwa cha harusi yake yeye mwenyewe. Kikao cha maandalizi ya send-off yake.

Simulizi yake Ilikuwa hivi.


Nachokumbuka ni kwamba hadi nafikisha umri wa miaka nane, sikuwahi kujua tabasamu wala kicheko. Ilikuwa kama niko jeshini nasomea ukomando. Kazi baada ya kazi ndio ulikuwa utaratibu wa maisha yangu. Kosa dogo kabisa lingeweza kunisababishia kulazwa kwenye godoro lenye maji kwa wiki nzima. Hizo bakora je? Ilifika mahali nikawa najiuliza huyu kweli ni mama yangu mzazi? Sikuwahi kupata jibu. Nilipokuwa nafikisha miaka nane, nikaamua kutoroka nyumbani. Nilijificha ndani ya gari la taka lililofika pale mtaani kukusanya taka kwa ajili ya kwenda kuzihifadhi mwenye dampo nje ya jiji. Inaonekana nilikuwa na kismati siku hiyo. Kulikuwa na msamaria mwema akikusanya watoto wa mtaani kwa ajili ya kuwahifadhi kwenye kituo chake cha kusaidia watoto wa mtaani. Nikajikuta nimebahatika kuokotwa. Tangu siku hiyo maisha yakabadilika. Angalau niliishi kama mtoto wa umri wangu. Kulikuwa na muda wa michezo, tulikula vizuri na maisha yalikuwa na maana. Angalau naweza kukiri hilo. Mwaka huo huo nilianzishwa shule.

Nadhani Mungu alikuwa na mpango na maisha yangu. Kwa sababu alinijaalia akili za darasani. Lakini pia, alinijaalia kukutana na watu wenye mapenzi mema na mimi tangia hapo. Baada ya kufanya vizuri mitihani' ya darasa la pili, nilirushwa darasa na kuingia darasa la nne. Nikafanya mtihani wa kitaifa na kuongoza kwa kata yetu. Nikaingia darasa la tano. Kutokana na uwezo wangu kuwa mzuri, baadaye nilirushwa na kuingia la Saba bila kusoma la Sita kama wenzangu, hii ikiwa ni mara ya pili kurushwa darasa. Walau sasa nilikuwa darasa moja na watu wa rika langu.

Wamiliki wa kituo chetu walipendezwa Sana na juhudi zangu kimasomo, wakanipenda Sana na hata kuamua kuniasili (adopt)wao wenyewe. Nilikuwa nimeangukia kwenye mikono iliyo salama.

Kutokana na wema wao kwangu, nilijiapiza moyoni. 'Nitafanya kwa ukamilifu kila watakachoniagiza.' Hao watu, ndio wazazi wangu hata leo. Walionizaa hawakuona umuhimu wangu kwao, hawa walioniokota waliona thamani yangu. Wakayabadili maisha yangu kabisa na ndio maana sikuona shida kabisa kujiapiza kuwapenda na kuwatii hadi nakufa.'

ITAENDELEA..
FB_IMG_1614266980417.jpg
 
HELENA SIMULIZI YA HUBA 15
DAVID NGOCHO SAMSON
0629077792

15

Simulizi ya Hellen inaendelea..

…. Derick mpenzi. Sio kwamba nilikusudia kukuficha, hapana. Haikuwa kusudi langu kukuficha kuwa nina mchumba. La hasha sweetie. Ni kwamba sikuwahi kudhani tungefikia hapa tulipo. Wakati naingia mwaka wa pili hapa chuoni, wazazi wangu walezi walinijulisha kuwa walikuwa na pendekezo la nani awe mchumba wangu. Walinishawishi kwamba Allan, ambaye ni mfanyabiashara mwenye kumiliki kampuni inayofanya vizuri katika ulimwengu wa teknolojia ya mawasiliano, ni mtu sahihi kwangu. Kwanza, kwa sababu wao wazazi wangependa niolewe na mtu ambaye licha ya kuwa na uchumi mzuri, ni mcha Mungu. Pili, Allan ni kama mtoto wao, kijana ambaye amekulia kwenye mikono yao kama ilivyokuwa kwangu. Wanamfahamu vizuri. Isipokuwa tu, yeye aliasiliwa(adopted) na familia nyingine akitokea mikononi mwao alipokuwa na miaka 8. Wao walimpata Allan akiwa kichanga cha siku kadhaa. Familia iliyomchukua Allan mikononi mwa wazazi wangu ilikuwa familia yenye maadili. Familia yenye kuzingatia uchaji Mungu. Kwa maoni yao, ndoa yetu ingekuwa ndoa iliyoundwa mbinguni kwa kuzingatia Historia zetu mimi na Allan.

Kwa hiyo, walipoamua kunikutanisha na Allan, sikuweka kipingamizi. Nilikwisha jiapiza kuwatii.

Sijui. Labda sijui tu maana ya mapenzi. Nilipokutana na Allan, niligundua kuwa ni kweli ana sifa zote za kunimiliki. Lakini moyo wangu haukuridhika kama ambavyo nilitarajia kabla ya kukutanishwa naye. Nilimuona kama kaka mwenye mafanikio na nilimpenda kwa sababu hiyo, lakini mwili wangu haukusisimka kama ambavyo nilitamani itokee. Labda nikueleleze hivi, kabla ya kukutanishwa naye, nilikuwa nikikaa mwenyewe natafakari itakavyokuwa nikikutana naye. Ajabu haikitokea hivyo nilipokutana naye. Hisia zangu hizo ni kama zilijificha kabisa zisitokee kamwe mbele yake. Hisia hizo, ziliendelea kubaki mafichoni hadi pale nilipokushuhudia kwa mara ya kwanza ukifanya wasilisho la Hr301. Kila kitu nilichokuwa nawazia siku ya kukutana na mpenzi kingetokea, kilitokea nilipokutia machoni wewe Derrick. Ndio maana sikuona tashwishi kukutunuku busu siku ya kwanza. Nakupenda sana Derick na niko tayari kuvunja uchumba na Allan ili nibaki na wewe.'

Ilikuwa simulizi ya Hellen. Wow! Nilijihisi mwenye bahati kuangukiwa na zali hili la kukutana na Hellen. Nikamshukuru Mungu kwa ajili ya Hellen na nikashukuru kwa kozi ya Hr301 iliyotukutanisha. Lakini nilipotafakari kwa kina, nikaona ugumu mbele yetu. Namna gani ningeendelea kubaki na Hellen? Nikajiuliza, je ninao ujasiri wa kuvunja uchumba huo ambao vikao vya harusi vilikuwa vikiendelea? Kusema kweli sikuwa na ujasiri huo. Nilijaribu kuvaa viatu vya Allan, nikaona vinanipwaya kabisa. Mbaya zaidi, Hellen alinijulisha kuwa tangazo la ndoa kanisani ilikuwa imesalia jumapili moja tu wahesabu kuwa hakuna pingamizi. Nisingeweza kumfanya mpenzi wangu Hellen avunje kiapo chake cha utii kwa watu waliomaanisha furaha na maisha kwake. Watu aliohiyari kwa dhati ya moyo wake kuwatunuku nafasi ya wazazi maishani mwake baada ya wale halisi kumkataa. Ingawa alikimbia mwenyewe nyumbani utotoni, ni dhahiri, alikimbia mateso. Waswahili husema, akufukuzaye hakuambii toka. Vipi ningeweza kuwa chanzo cha huzuni ya mwanaume mwenzangu ili tu niwe na furaha mimi.? Ingawa Hellen alikuwa tayari kusaliti penzi la Allan kama ningemtaka kufanya hivyo, sikuwa na ujasiri wa kumruhusu afanye hivyo. Nilimuomba aendelee na taratibu za ndoa. Akakubali kwa sharti moja tu, kwamba tungeendeleza mapenzi yetu kwa siri. Ah, ni ngumu sana. Nilikubali almradi, lakini moyoni mwangu nilikusudia kutoroka jiji la Dar na kurudi kwetu Mbalizi mkoani Mbeya, kwenye bonde lenye joto majira yote ya mwaka kulinganisha na sehemu nyinginezo kwa mkoa huo. Hicho ndio kitu nilichofanya. Lakini kabla ya kufanya hivyo nilimpigia simu Welu tukakutana naye.

16

Tulikuwa sote watatu tumemaliza mitihani ya kumaliza elimu zetu za chuo na tayari wenzetu wengi walikuwa wameshasambaa kila mtu akisaka maisha kivyake. Hellen alikuwa keshafunga ndoa na mchumbaake Allan. Tulipokutana Mimi na Welu lengo langu lilikuwa kumuomba Welu, twende zetu Mbeya.

'Dear, now that we are through with our undergraduate program, what's your plan? (Mpenzi, hivi sasa tumeshaua chuo, una mpango gani?) Nilimuuliza Welu.

'Kwa maana ya mapenzi yetu au kazi?' Welu aliniuliza kwa namna ambayo niliitafsiri kwamba ana jambo hataki kuniweka wazi. Najua kwa muda fulani nilikuwa nimejikita sana kwa Hellen na kumkwepa kwepa Welu, hivyo nikahisi labda anataka kunionesha kwamba hakupenda hali hiyo. Sikutaka kuingia ndani sana kutaka kuulizia kulikoni kwa kuhofia kutibua mambo zaidi. Kwa kifupi Welu wangu alionekana kuwa na kisirani kingi.

'Lets say both' (ok, tufanye naulizia kwa pande zote)

'Ah, sijui kwa upande wa mapenzi, maana hilo ni jambo linalohitaji watu wawili, so, inategemea pia wewe una mpango gani. Kuhusu kazi, I'm fighting to get one (napambana kutafuta)'. Kama mwanzo, Welu aliendelea kunijibu kavu. Nikajikuta sipendezewi na hali hiyo. Hivyo nilijipata nimeropoka.

'Kwani una shida gani we mwanamke, mbona kama sikuelewi? Majibu unayonipa, ni kama umejisahau kwamba Mimi ni nani kwako au?' niliongea kwa hamaki.

'Ey hey!' Welu alinipayukia huku akinisonta kwa kidole cha pili baada ya gumba lake la kulia. Halafu akaendelea kuongea;

'Tena unyamaze hivyo hivyo. Usidhani miye bwege? Taarifa zako zote nnazo. Shukuru nimekupa na nafasi hii. Mwanahizaya wewe, eti "oh Welu wangu nakupenda sana" unampenda nani? Na yule unayeshinda naye mahotelini ni nani? Toka ulivyorudi toka Nairobi, ulikumbuka kuwa kuna Welu? Huna hata aibu kujidai kunifokea? Kama huna la maana lingine, mie naondoka zangu.' Welu alizungumza kwa ukali sana na kusema kweli nilikosa pozi kabisa. Nilijikuta sina hata cha kusema. Sikudhani kama Welu angeshitukia ishu yangu na Hellen. Ni kama sasa nilikuwa nimebambwa laivu. Nilijisikia aibu sana.

'Samahani mpenzi.' nilitamka kwa upole nikikusudia kunyenyekea na kumtaka msamaha.

'Samahani mpenzi' Welu alitamka maneno yangu kwa kuyarudia huku akibinya pua yake kama vile ameona kinyaa, midomo yake akiibenua kwa dharau. Lo! Nilijipata njia panda. Leo hii, Welu wangu wa kuning'on'ga miye? Sikuamini vile nilikuwa najikuta njia panda. Kule Hellen kawekwa ndani na kidume mwingine, huku, mpenzi wangu wa siku nyingi, tena aliyekuwa akiniheshimu sana sasa ananionesha dharau waziwazi. Sikuona kama kulikuwa na future tena ya Mimi na Welu. Hata hivyo, kwa vile makosa yalikuwa yangu, nilikusudia kumuomba msamaha.

'Najua umesikia mengi kuhusu….'

'Sio tu kusikia, Nimesikia mengi na kuona mengi. Siamini kabisa Derick kuwa pamoja na yote tuliyokuwa tumepanga na kuahidiana, ulithubutu kuyakanyagia chini kiasi hiki... ' Welu alinikatisha na kuchomekea lawama zake.

'Hata, hivyo Derick, nahisi kabisa we were never meant to be. I'm sorry but I have moved on. I think you should move on too. And before I forget, I thought I should bring you this.' ( nahisi kabisa haikupangwa tuwe, nimeamua kuendelea kivyangu, na nakushauri na wewe pia uendelee kivyako. Kabla sijasahau, nilifikiri ni vema nikuletee hii) Welu aliongea akiwa anaivua Pete ambayo nilimvalisha siku ya birthday yake mbele ya marafiki zake mwaka Jana tu. Dah! Niliumia sana. Sijui hata ilikuwaje, nilijikuta tayari nimeshapiga magoti na kuikumbatia miguu yake nikimsihi asiniache. Sikuwa tayari kubaki bachelor. Isitoshe,mapenzi na Hellen ndio kama hivyo, nilihesabu yamekwisha kwa vile, katu katu, nisingethubutu kuendelea naye akiwa ni mke tena aliyehalalishwa kwa ndoa takatifu. Tayari alikuwa ni mke wa Allan.

'Baby, please forgive me. Please darling. Let's get married right away. I want to prove to you that I real love you and am not going anywhere. Please Hellen, forgive me?' (Baby, tafadhali nisamehe. Tafadhali mpenzi. Nataka tufunge ndoa haraka iwezekanavyo. Nakuomba Hellen, nisamehe mpenzi)

'What did you call me?' (umeniita nani?) swali lake hilo likanirudiaha kwenye uhalisia. What? Ah I was in deep shit. Imagine nilijisahau na kumuita Welu Hellen. Nilipogundua hiyo mistake, nilikuwa too late(nshachelewa), Welu alinisukumia mbali na kuondoka huku analia. Nilijisikia vibaya mno. Dah, ama kwa hakika njia ya muongo ni fupi. Fupi sana. Nilijinyanyua na kuchomoka spidi sana kumfuata Welu, lakini wapi? alikuwa keshapanda gari na kuniacha. Nilimuungia tela kwa bodaboda. Alipofika gheto kwake na Mimi nikawa naingia. Sikutaka kupoteza muda. Nilimfuata na kumsihi sana. Lakini alikuwa ameamua kunifungia vyoo. Hata hivyo nilimfuata hadi ndani kwake.

'Baby, siondoki hapa kama hunisamehi. Please. I'm really sorry.' Niliendelea kubembeleza. Hakujibu kitu. Alinishika mkono, akaninyanyua juu.

'What do you want Derick?( Unataka nini Derick?)' Welu aliniuliza

'What else dear, I want you! I want us to make a home. Nataka nikakutambulishe kwa baba na mama Derick. Nataka nikuchumbie. Nataka nikuoe mpenzi' nilijikuta natiririka maneno. Ni kweli kabisa, nilikusudia kumuoa na kuishi naye.

'Derick, Asante sana. Najua ni maneno matamu sana. Kama nisingekuwa na hali hii uliyonisababishia, hakika ningefurahia maneno yako. Lakini, kama unajali hisia zangu. Tafadhali sana Derick, nipe muda. Nipe muda wa kutafakari, nipe nafasi ya kuamua ama kuwa nawe au kungoja kwanza. Nahitaji muda wa kuwa peke yangu kwanza. Tafadhali heshimu ombi langu hili kama bado una chembechembe yoyote ya kujali na kuniheshimu uliyobakiwa nayo.' Sikuwa na jinsi. Maneno yake yalikuwa mazito mno na yalinielemea vilivyo. Nilijiondokea kimya kimya kwa aibu.. nilijisemea moyoni, 'acha nimwache kwanza, kesho nitamtafuta) Baada ya juhudi zangu kugonga mwamba nikasema, hewala bwana. Baada ya kurudi kwangu, nilimpigia simu nikimuomba akubali twen'zetu Mbalizi Mbeya. Nilimweleza juu ya biashara yangu ya mbao. Biashara ambayo nilikuwa naota kuwa itakuja kunipa maisha ya kututosheleza Mimi na yeye na familia ambayo tungeanzisha. Hakuwa tayari na ni kama alipuuza ndoto yangu ya biashara ya mbao. Baada ya siku nyingi kiasi, mambo yakiwa bila bila, nilifanya maamuzi. Nikajiondokea zangu jijini Dar kwa unyonge. Nikawa Sasa nimebaki single boy. Hasira zangu nikaamua kuzielekeza kwenye ndoto yangu kwa lengo la kumthibitishia Welu kuwa inawezekana ndoto kuwa kweli.

ITAENDELEA...
FB_IMG_1614267256126.jpg
 
HELENA SIMULIZI YA HUBA 17 (MWISHO)
DAVID NGOCHO SAMSON
0629077792

17

Mwaka mmoja baada ya ndoa ya Hellen na Allan, mimi nilikuwa nipo zangu Mbalizi nikifanya biashara ya kusafirisha na kuuza mbao. Mara nyingi tenda zangu zilikuwa kutokea Tunduma na Sumbawanga mjini. Mbao nilizichukua umalila, huko Mbeya vijijini. Maisha yalikuwa hayajanitupa mkono baada ya kumaliza chuo kama ambavyo wenzangu wengi niliyowasiliana nao walivyokuwa wanalalamikia ukosefu wa ajira. Hivyo, nilimudu kununua kagari kakutembea kwa safari za hapa na pale na nilikuwa namalizia kujenga kanyumba kangu ka kisasa maeneo ya Forrest mpya.

Jioni ya tarehe 17/09/2016, nilipokea simu, namba mpya ikisomeka kwenye kioo Cha simu yangu ya kisasa.

'Derrick' Ilikuwa sauti ambayo haikuwa ngeni kwangu hata kidogo. Niliifahamu sauti ile. Ingawa mwaka mmoja ulishapita tangu tulipofanya mazungumzo na mtu huyu, kamwe sauti yake isingeweza kunipotea kabisa. Ilikuwa sauti ya Hellen.

'Hellen?' nilitamka kwa sauti ya ulizo.

'Nipo Mbeya Derick'

'Upo Mbeya?' nilihoji kwa mshangao nikijiuliza Hellen kafuata nini Mbeya na amejuaje namba yangu. Najua alifahamu nyumbani Ni Mbeya lakini kwa mwaka Sasa hatukua na mawasiliano.

'Ndio Derrick, tafadhali njoo unipokee' alitamka Hellen. Unajua Kuna vile unawezakutwa na kigugumizi cha ghafla usijue nini cha kusemaee, hiyo ndio hali iliyonikumba ghafla. Nilibaki kimya sijui niseme nini.

'Derick!' sauti ya Hellen ikanizindua kwenye gagaziko langu.

'Uko wapi Hellen?'

'Niko Mbeya stand kuu. Ndio nimeshuka kwenye basi muda si mrefu Derick!' Hellen aliongea na kunyamaza. Nadhani alitaka nimjulishe kama naenda kumfuata au atafute wapi pa kufikia.

'Nakuja Hellen, twenty minutes top' nilitamka, na wakati huo huo nikawa nalifuata gari langu aina ya Rav4.


Sikuamini macho yangu nilipofika stand kuu. Mbele yangu nilimshuhudi Hellen akiwa na katoto kadogo ka kike, kazuri kama malaika. Kalikuwa ni katoto keupe kuliko mama yake. Sikuhitaji DNA kufahamu kuwa ile ilikuwa ni damu yangu. Nasema hivyo kwa sababu, mimi ni mweupe, Hellen ni maji ya kunde, Allan ni ile ngozi kama ya watu wa sudani Kusini. Melanini halisi. Ule weusi unaong'ara.

Nilimkumbatia Hellen wangu na kumpokea mtoto na bag halafu mdogo mdogo tukaelekea nilikopaki gari langu. Tukaingia ndani, nikalitekenya likacheka, kisha hao tukaelekea zetu nyumbani. Ilikuwa furaha kubwa sana kuonana tena na Hellen. Baada ya Hellen kunisimulia kikichomleta kwangu, hatukuwa na muda wa kusubirisana. Tuliuwasha upya moto wa penzi letu.

Labda nikujulishe tu, hadi leo hii napokuandikia, naendelea kumshukuru Mungu kwa kumleta Hellen maishani mwangu. Amekuwa baraka katika maisha yangu. Sana yaani. Sana tu. Baada ya Angel, mtoto wetu wa kwanza, Hellen amenizalia watoto wengine watatu. Justine, Boke na Robin. Tunaishi kwa furaha sana. Kwa sasa tupo Sweden ambako tulikuja kwa ajili ya masomo ya juu zaidi lakini tulipomaliza tu, tukabahatika kupata kazi pia. Biashara yangu ya mbao, bado inaendelea vizuri kule nyumbani, nimemwajiri jamaa mmoja smart sana kuisimamia. Lakini pia, tulifungua biashara nyingine kadhaa.

Najua unajiuliza ilikuwaje tukaoana na Hellen na tumeanzaje kuishi Sweden. Nitakueleza kwa ufupi. Ukweli ni kwamba, Hellen ni mke wangu halali wa ndoa kabisa.

Ni kwamba, baada ya Hellen kujifungua Angel, Allan ambaye alikuwa mumewe, alihisi kachezewa rafu. Hakukubali kuwa Angel ni damu yake. Sababu kubwa Ilikuwa ule weupe aliozaliwa nao. Kwa siri, aliamua kupima DNA. Akabaini kuwa mtoto si wake. Kwake aliona ni kosa kubwa ambalo hangeweza kusamehe. Kwa vile dini inaruhusu kuachana kwa sababu ya uzinzi, aliitumia hiyo kumpa talaka Hellen. Kumbe, lile penzi letu la chuoni mwishoni mwishoni, siku ile tunayoachana baada ya kunijulisha uwepo wa mchumbaake, lilimleta Angel duniani. Baada ya Hellen kupewa talaka, akalazimika kunitafuta. Kwangu mimi na yeye, hiyo ilikuwa ni habari njema. Nilimpokea kwa mikono miwili. Kutokana na kwamba Hellen aliwahi kupata ufadhili wa masomo ya chuo kutoka kwa sponsor wake kutokea Sweden, mama yule wa kiswidish alimtafuta tena Hellen na kumpa ofa ya kusomea masters katika chuo kikuu cha Upsalla huku Sweden. Hata hivyo, Hellen alimjulisha kuhusu Mimi na mwanetu Angel. Akakubali kutufadhili sote. Mama huyu anaitwa Gratel Christos.

Mimi na mke wangu Hellen, kwa sasa ni waajiriwa katika taasisi ya mama huyu inayoshughulikia kutoa ufadhili kwa watoto na vijana waliokulia katika mazingira magumu katika nchi za ukanda wa kuzunguka ziwa Victoria, yaani nchi za maziwa makuu. Afrika ya mashariki.


Tamati.

Nini maoni yako kuhusu hii short story? Tiririka hapo chini.

David
FB_IMG_1614267518898.jpg
 
HELENA SIMULIZI YA HUBA 17 (MWISHO)
DAVID NGOCHO SAMSON
0629077792

17

Mwaka mmoja baada ya ndoa ya Hellen na Allan, mimi nilikuwa nipo zangu Mbalizi nikifanya biashara ya kusafirisha na kuuza mbao. Mara nyingi tenda zangu zilikuwa kutokea Tunduma na Sumbawanga mjini. Mbao nilizichukua umalila, huko Mbeya vijijini. Maisha yalikuwa hayajanitupa mkono baada ya kumaliza chuo kama ambavyo wenzangu wengi niliyowasiliana nao walivyokuwa wanalalamikia ukosefu wa ajira. Hivyo, nilimudu kununua kagari kakutembea kwa safari za hapa na pale na nilikuwa namalizia kujenga kanyumba kangu ka kisasa maeneo ya Forrest mpya.

Jioni ya tarehe 17/09/2016, nilipokea simu, namba mpya ikisomeka kwenye kioo Cha simu yangu ya kisasa.

'Derrick' Ilikuwa sauti ambayo haikuwa ngeni kwangu hata kidogo. Niliifahamu sauti ile. Ingawa mwaka mmoja ulishapita tangu tulipofanya mazungumzo na mtu huyu, kamwe sauti yake isingeweza kunipotea kabisa. Ilikuwa sauti ya Hellen.

'Hellen?' nilitamka kwa sauti ya ulizo.

'Nipo Mbeya Derick'

'Upo Mbeya?' nilihoji kwa mshangao nikijiuliza Hellen kafuata nini Mbeya na amejuaje namba yangu. Najua alifahamu nyumbani Ni Mbeya lakini kwa mwaka Sasa hatukua na mawasiliano.

'Ndio Derrick, tafadhali njoo unipokee' alitamka Hellen. Unajua Kuna vile unawezakutwa na kigugumizi cha ghafla usijue nini cha kusemaee, hiyo ndio hali iliyonikumba ghafla. Nilibaki kimya sijui niseme nini.

'Derick!' sauti ya Hellen ikanizindua kwenye gagaziko langu.

'Uko wapi Hellen?'

'Niko Mbeya stand kuu. Ndio nimeshuka kwenye basi muda si mrefu Derick!' Hellen aliongea na kunyamaza. Nadhani alitaka nimjulishe kama naenda kumfuata au atafute wapi pa kufikia.

'Nakuja Hellen, twenty minutes top' nilitamka, na wakati huo huo nikawa nalifuata gari langu aina ya Rav4.


Sikuamini macho yangu nilipofika stand kuu. Mbele yangu nilimshuhudi Hellen akiwa na katoto kadogo ka kike, kazuri kama malaika. Kalikuwa ni katoto keupe kuliko mama yake. Sikuhitaji DNA kufahamu kuwa ile ilikuwa ni damu yangu. Nasema hivyo kwa sababu, mimi ni mweupe, Hellen ni maji ya kunde, Allan ni ile ngozi kama ya watu wa sudani Kusini. Melanini halisi. Ule weusi unaong'ara.

Nilimkumbatia Hellen wangu na kumpokea mtoto na bag halafu mdogo mdogo tukaelekea nilikopaki gari langu. Tukaingia ndani, nikalitekenya likacheka, kisha hao tukaelekea zetu nyumbani. Ilikuwa furaha kubwa sana kuonana tena na Hellen. Baada ya Hellen kunisimulia kikichomleta kwangu, hatukuwa na muda wa kusubirisana. Tuliuwasha upya moto wa penzi letu.

Labda nikujulishe tu, hadi leo hii napokuandikia, naendelea kumshukuru Mungu kwa kumleta Hellen maishani mwangu. Amekuwa baraka katika maisha yangu. Sana yaani. Sana tu. Baada ya Angel, mtoto wetu wa kwanza, Hellen amenizalia watoto wengine watatu. Justine, Boke na Robin. Tunaishi kwa furaha sana. Kwa sasa tupo Sweden ambako tulikuja kwa ajili ya masomo ya juu zaidi lakini tulipomaliza tu, tukabahatika kupata kazi pia. Biashara yangu ya mbao, bado inaendelea vizuri kule nyumbani, nimemwajiri jamaa mmoja smart sana kuisimamia. Lakini pia, tulifungua biashara nyingine kadhaa.

Najua unajiuliza ilikuwaje tukaoana na Hellen na tumeanzaje kuishi Sweden. Nitakueleza kwa ufupi. Ukweli ni kwamba, Hellen ni mke wangu halali wa ndoa kabisa.

Ni kwamba, baada ya Hellen kujifungua Angel, Allan ambaye alikuwa mumewe, alihisi kachezewa rafu. Hakukubali kuwa Angel ni damu yake. Sababu kubwa Ilikuwa ule weupe aliozaliwa nao. Kwa siri, aliamua kupima DNA. Akabaini kuwa mtoto si wake. Kwake aliona ni kosa kubwa ambalo hangeweza kusamehe. Kwa vile dini inaruhusu kuachana kwa sababu ya uzinzi, aliitumia hiyo kumpa talaka Hellen. Kumbe, lile penzi letu la chuoni mwishoni mwishoni, siku ile tunayoachana baada ya kunijulisha uwepo wa mchumbaake, lilimleta Angel duniani. Baada ya Hellen kupewa talaka, akalazimika kunitafuta. Kwangu mimi na yeye, hiyo ilikuwa ni habari njema. Nilimpokea kwa mikono miwili. Kutokana na kwamba Hellen aliwahi kupata ufadhili wa masomo ya chuo kutoka kwa sponsor wake kutokea Sweden, mama yule wa kiswidish alimtafuta tena Hellen na kumpa ofa ya kusomea masters katika chuo kikuu cha Upsalla huku Sweden. Hata hivyo, Hellen alimjulisha kuhusu Mimi na mwanetu Angel. Akakubali kutufadhili sote. Mama huyu anaitwa Gratel Christos.

Mimi na mke wangu Hellen, kwa sasa ni waajiriwa katika taasisi ya mama huyu inayoshughulikia kutoa ufadhili kwa watoto na vijana waliokulia katika mazingira magumu katika nchi za ukanda wa kuzunguka ziwa Victoria, yaani nchi za maziwa makuu. Afrika ya mashariki.


Tamati.

Nini maoni yako kuhusu hii short story? Tiririka hapo chini.

DavidView attachment 1718982
story nzuri sana hongera
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom