Tutor B
JF-Expert Member
- Jun 11, 2011
- 9,025
- 6,614
HEKIMA NI NINI?
Hekima ni uwezo wa kutumia maarifa uliyonayo kwa ajili ya kuzalisha matokeo unayotamani maishani mwako. Unapotamani kuona matokeo fulani katika maisha yako jua kuwa kuna maarifa ambayo kwanza unayahitaji; ambayo hayo ndo utapata uwezo wa kuyatumia kwa ajili ya kuzalisha hayo matokeo kusudiwa.
Bibilia inasema: *“Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.” (YAK. 1:5 SUV).* Natamani uone kuwa hapa unachoweza kuomba toka kwa Mungu ni hekima, na kumbuka hekima ni uwezo wa kutumia maarifa kwa ajili ya kusababisha mabadiliko ambayo unatamani kuyaona katika maisha yako.
Huwezi ukamwomba Mungu maarifa. Maarifa Mungu ameshayatoa kupitia Neno Lake, watu, vitabu, CD, DVD nk. Ni wajibu wako kutafuta maarifa mahususi kwa ajili ya matokeo ambayo unatamani kuyaona maishani mwako. Lakini kumbuka kuwa maarifa hayatakupa matokeo lakini uwezo wa kuyatumia hayo maarifa ambayo ni hekima ndiyo itakayokupa matokeo maishani.
Ukishakuwa na maarifa ambayo unajua unahitaji kwa ajili ya kuzalisha matokeo fulani katika maisha yako ukiona hujui namna ya kutumia hayo maarifa kuzalisha hayo matokeo, sasa unaweza ukamwomba Mungu huo uwezo wa kuyatumia maarifa uliyo nayo kuzalisha hayo matokeo unayotamani.
Maandiko yanasema; *“Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa watoto wake wote.” (LK. 7:35 SUV).*
Sijui kama unaona ninachoona? Hazungumzii watoto wa maarifa wala watoto wa ufahamu anazungumzia watoto wa hekima. Hekima ndiye mwenye watoto. Au kwa maneno mengine hekima ndiyo inayozaa matokeo maishani mwetu. Usipokuwa na uwezo wa kujua jinsi ya kutumia maarifa kuzalisha matokeo maishani mwako hutakuwa na kitu cha kuonyesha. Sasa sio kwamba huna maarifa ni kwamba huna uwezo wa kuyatumia maarifa uliyo nayo kuzalisha matokeo maishani mwako. Hivi hujawahi kuona mtu amesoma degree kibao lakini hakuna ushahidi maishani mwake wa kuonyesha kuwa yeye ni msomi?
Maisha yake hayana tofauti kabisa na mtu ambaye hajaenda shule? Tena kuna watu ambao hawajaenda shule wana matokeo makubwa zaidi maishani mwao kuliko yeye aliyeenda? Nini kimepungua? - Hekima.
Uwezo wa kuyatumia hayo maarifa kuzalisha matokeo maishani mwake. Hiyo hekima anaitoa Mungu na amesema ukiihitaji umwombe Naye atakupa kwa ukarimu pasipo kukukemea. Suleiman alikuwa na maarifa maana kama mtoto wa Mfalme alikuwa amesomeshwa vizuri mno. Ila alijua ili afanikiwe katika utawala wake atahitaji hekima, yaani uwezo wa kutumia hayo maarifa kiusahihi. Akamwomba Mungu hekima na Mungu akampa hekima kama mchanga wa bahari.
Hata wewe unaweza kumwomba Mungu hekima. Akupe uwezo wa kutumia maarifa uliyo nayo kuzalisha matokeo unayotamani maishani mwako. Ukiangalia maandiko yanasema; “Nyumba hujengwa kwa hekima, Na kwa ufahamu huthibitika, Na kwa maarifa vyumba vyake hujazwa Vitu vyote vya thamani na vya kupendeza. Mtu mwenye hekima ana nguvu; Naam, mtu wa maarifa huongeza uwezo;” (MIT. 24:3-5 SUV).*
Unaona hapo? Nyumba hujengwa kwa hekima. Hamna kitu unaweza ukakijenga bila hekima. Iwe biashara, iwe huduma, iwe chochote! Unahitaji hekima, yaani uwezo wa kutumia maarifa kiusahihi ili kuzalisha matokeo. Anasema kwa ufahamu itathibitika. Ili uwe na kitu kisichoyumbishwa yumbishwa unahitaji ufahamu ambao ni uwezo wa kuelewa maarifa uliyo nayo.
Wengi tumefikia hatua hii ya ufahamu; tuna maarifa sahihi na tunao uwezo wa kuelewa na kutafsiri hayo maarifa na ndiyo maana tunaweza kuelezea vizuri sana vitu. Lakini kama tukitaka matokeo yanayoshikika lazima tuwe na uwezo wa kuyatumia hayo maarifa tuliyoyaelewa kuzalisha matokeo.
Alafu anasema kwa maarifa hiyo nyumba ambayo imejengwa kwa hekima ikathibitika kwa ufahamu hujazwa vitu vyote vyema na vya thamani. Maarifa ni uwezo wa kukusanya taarifa sahihi kuhusu jambo husika. Mtu mwenye taarifa sahihi kuhusu jambo anayo maarifa. Akizielewa hizo taarifa anao ufahamu. Akiweza kutumia hizo taarifa alizoelewa kuzalisha matokeo huyo ana hekima.
Watu walipoyaona matendo makuu ya Mungu katika maisha ya Yesu moja kwa moja walijua kuwa yale matendo makuu ni matokeo ya hekima yaani uwezo wa kutumia maarifa kuzalisha matokeo.
Embu tuangalie maandiko: - *“Na ilipokuwa sabato, alianza kufundisha katika sinagogi; wengi waliposikia wakashangaa, wakisema, Huyu ameyapata wapi haya? Na, Ni hekima gani hii aliyopewa huyu? Na, Ni nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake?” (MK. 6:2 SUV).*
Walipokuwa wanamsikiliza Yesu akifundisha na miujiza ambayo alikuwa anaifanya walishangazwa mno na kwanza amepata wapi hayo anayoyafundisha? Pili hiyo hekima ameitoa wapi hata miujiza mikubwa ilikuwa ikifanyika kwa mikono Yake? Yesu alikuwa na uwezo wa kutumia maarifa aliyo nayo kuzalisha matokeo kusudiwa katika maisha na huduma Yake? Miujiza iliyoambatana na maisha ya Yesu ilikuwa matokeo ya hekima yaani uwezo aliyokuwa nao wa kutumia maarifa kiusahihi kuzalisha matokeo.
Kinyume cha hekima ni upumbavu na upumbavu ni kutokuwa na uwezo wa kutumia maarifa kuzalisha matokeo maishani mwako. Maandiko yanasema: - *“Kazi yao wapumbavu huwachosha kila mmoja, Maana hajui hata njia ya kuuendea mji.” (MHU. 10:15 SUV).*
Umeona kitu maandiko yanachosema? Kazi ya mpumbavu humchosha kila mmoja. Kwanini? Hajui njia (namna ya kufanya) ili aweze kuingia mjini. Njia ni mkakati, mpango. Hekima itakupa cha kufanya ili uweze kuzalisha matokeo kusudiwa. Haijalishi nini unafanya. Hekima itakupa uwezo kutumia maarifa uliyo nayo katika uhalisia wa hali na changamoto unazokabiliana nazo ili kuzalisha matokeo tamaniwa na kusudiwa.
Maandiko yanasema: *“Mwanangu, ule asali, kwa maana ni njema, Na sega la asali lililo tamu ulionjapo. Basi utaijua hekima kuwa tamu kwa nafsi yako; Ikiwa umekwisha kuiona; Ndipo itakapofuata thawabu; Wala tumaini lako halitabatilika.” (MIT. 24:13-14 SUV).*
Ulaji wa asali na sega la asali ndo ukusanywaji wenyewe wa taarifa sahihi yaani maarifa. Ndo kusoma na kujisomea kwenyewe. Ila taarifa hizi haziwezi kukuzalia matokeo kama usipopewa uwezo wa kuona au kujua unatakiwa kufanya nini na hizo taarifa ili kujizalia matokeo maishani mwako. Ukishaona hekima, yaani ukajua unapaswa kufanya nini na hayo maarifa ndipo inapofuata thawabu au kwa maneno mengine matokeo.
Maisha hayampi matokeo yeye mwenye maarifa bali yeye anayejua jinsi ya kuyatumia hayo maarifa kiusahihi ili kuzalisha matokeo.Tumaini, ndoto, maono na malengo ya watu wengi yanabatilika kwa sababu ya kutokuwa na hekima yaani uwezo wa kutumia maarifa kwa ajili ya kuzalisha matokeo.
Ukiwa na hekima unakuwa na nguvu ya kufanya kitu. Maarifa yanakuongezea uwezo (capacity) ya kufanya kitu. Kila mtu anayo capacity yaani uwezo wa kufanya kitu fulani lakini ili akifanye atahitaji hekima yaani uwezo wa kugeuza huo uwezo wa kufanya kuwa kitu halisi. Mungu tunamwomba hekima ila sisi kazi yetu ni kutafuta maarifa.
Paulo alipowaombea Waefeso aliwaombea Waefeso vitu viwili vikubwa: *“Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye; macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue…..” (EFE. 1:17-18 SUV).* Mtu wa Mungu roho ya ufunuo itakusaidia kuyaelewa maarifa uliyo nayo na roho ya hekima itakupa uwezo wa kuyatumia maarifa hayo ambayo umeyaelewa kuzalisha matokeo maishani mwako.
Paulo aliwaombea pia Wakolosai maombi yanayofanana na haya: *“Kwa sababu hiyo sisi nasi, tangu siku ile tuliposikia, hatuachi kufanya maombi na dua kwa ajili yenu, ili mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni;” (KOL. 1:9 SUV).*
Paulo alijua kuwa hata Wakolosai wajazwe maarifa kiasi gani haitawasaidia kama wasipopata na uelewa ambao utawapa ufahamu na hekima ambayo itawapa uwezo wa kutumia hayo maarifa kiusahihi. Kama unajiona unajua vitu vingi lakini unachojua hakikusaidii kukwamuka maishani basi ulichopungukiwa ni hekima, yaani uwezo wa kutumia unachojua kujizalishia matokeo maishani. Mungu amekuruhusu umwombe na ameahidi ukimwomba atakupa kwa ukarimu yaani kwa uwingi pasipo kukemea. Unaweza kukwamuka hapo ulipo.
Nikupe andiko moja hapa alafu nikuache. *“Walakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilika; bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu;” (1 KOR. 2:6-7 SUV).*
Paulo anasema kuwa ipo hekima waisemayo kati ya wakamilifu na anaisema hiyo hekima imefichwa ndiyo maana shurti tuiombe kwa Mungu, na anasema hiyo hekima Mungu aliiazimu tangia milele kwa utukufu wetu. Ipo hekima ya Mungu ambayo itakutoa hapo ulipo na kukuleta mahali patukufu na pa heshima.
Mwombe na usiache kuendelea kumwomba Naye atakupa. Ila kumbuka tu kuwa hekima ni uwezo wa kutumia maarifa kuzalisha matokeo. Kama wewe sio mtafutaji wa maarifa utaiwekea mipaka hekima maishani mwako. Tafuta maarifa maana hekima huja maishani mwako kukuwezesha kuyatumia hayo maarifa kuzalisha matokeo.
Ukiijua kweli itakuweka huru - nawe utakuwa huru kweli kweli.