chamilo nicolous
JF-Expert Member
- Mar 10, 2016
- 2,110
- 1,492
HEKIMA, AKILI na Ujanja/Hila.
Leo 17/8/2025, KKKT imetafakari juu ya kuongozwa na HEKIMA ya Mungu. Mtume Paulo anasema, “Hata hivyo, sisi tunatumia lugha ya hekima kwa wale waliokomaa kiroho; lakini hekima hiyo si ya hapa duniani, wala si ya watawala wa dunia hii ambao wako katika mkumbo wa kupotea” (1 Wakorintho 2:6-9).
Hekima, Akili na Ujanja/Hila vinachanganywa sana katika taifa letu. Ukiona matumizi ya nguvu yanazidi ujue hekima iko likizo, akili iko kifungoni na Ujanja/Hila uko zamu. Nimetafakari:
1. Matajiri na wageni kuchangia CCM isiwe taabu. Maskini wawe huru kuchangia tone tone wanakopenda. Mshikamano wa maskini usiwe nongwa wakati mshikamano wa matajiri umeruhusiwa. Hiyo ni hekima.
2. Matajiri kuchangia upinzani kwa kificho huku wakichangia CCM hadharani ni zaidi ya kasoro. Hekima itumike kuondoa hii aibu.
3. Mahakama imekuwepo kabla na baada ya uhuru. Haijawahi kuhojiwa na umma kama sasa. Hili si tatizo la umma wala la serikali. Ukikubali kuingiliwa, si tatizo la anayeingilia. Ni tatizo la mahakama. Akili na hekima vinahitajika.
4. Kuna wakati tutahitaji taifa moja lililoungana ili kuomboleza, kushangilia au kulilinda likiwa vitani. Kupigana sisi kwa sisi wakati tuko vitani ni janga. HAKI inaunganisha taifa. DHULUMA inaligawa. Tuna uchuro kitaifa. Tumegawanyika. Kukubaliana na ukweli huu ni HEKIMA.
5. “Wananchi wanataka mabadiliko”, alisema Baba wa Taifa. Kuwa na tumaini kuwa “mabadiliko yanakuja” ni nyenzo ya kutunza amani. Waliotugawa hawawezi kutuunganisha. Kama wanaweza watuambie tusiyoyajua ili tuamini. Hata wanaokataa mabadiliko wanataka mabadiliko. Tutumie hekima siyo nguvu, kukataa mabadiliko.
6. Yanayohitaji mabadiliko ni mengi lakini manne yako juu kabisa: Vita ya rushwa, utetezi wa watu maskini, utawala wa sheria na Demokrasia. Bunge na mahakama vimekwama. Serikali yetu inaogopwa na kila mtu/taasisi, na sasa INAJIOGOPA. Tutokeje hapa? Hekima na siyo hila inatakiwa.
7. Uchaguzi Mkuu huwa ni fursa ya kuinua matumaini na kuondoa kukata tamaa. Kila mtu alijifanya analaumu chaguzi za 2019 na 2020. Waliozilaumu, wakaharibu uchaguzi wa 2024 kuliko hata zile! Sasa hakuna anayeuamini wa 2025 ambao “kimsingi” umekwisha. Ndani ya vyama vyote, tunashindana kufanyiana hila. Waadilifu wanateseka sana.
8. Tumechanganya mambo. Tunadhani wingi ndiyo UKWELI na uchache ni UWONGO. Daraja linalounganisha wingi na ukweli linaitwa HILA. Daraja linslounganisha uchache na uwongo linaitwa UBABE. Tunastawisha kizazi cha kutumia ubabe kutatua matatizo. Kutumia hila na nguvu kutawala watu ni kuwachokoza watu. “Enyi wazazi msiwachokoze watoto wenu wasije wakakata tamaa” ( Kolosai 3:21). Ni hekima.
9. Kutumia nguvu na hila ili kuvuka mkwamo huu kwa tumaini la kufanya maridhiano baadaye ni kukwamisha maridhiano hayo. Ahadi ya katiba mpya ni tamu ikiwa wote wameshiriki katika uchaguzi wa kuielekea. Kupiga kura ni haki, wajibu na hiari pia. Kutopiga kura kwa kukosa imani na mfumo ni sawa na KUZUIWA kupiga kura. Rudisha imani, watu watapiga kura za kutosha. Ni hekima.
10. Giza la rushwa, ufisadi na dhuluma limetanda kote nchini. CCM inahitaji wapinzani halisi, Media halisi, Asasi za kiraia halisi, mashirika ya dini halisi, bunge halisi, mabaraza ya madiwani halisi, mahakama halisi na wazalendo halisi ili kusafisha nchi. Dola isitengeneze wapinzani. Dola isijigeuze wapinzani. Taifa linahitaji HAKI siyo HISANI. Anayekataa hili hatutakii mema.
TURUDI MEZANI
TEC TUNATAKIA NOVENA YENYE MAJIBU
MSIOJUA KUOMBA, JIFUNZENI.
Mungu, Taifa, sina chama, familia.