Hekima na busara

Martin BM

Member
Joined
Jul 2, 2020
Posts
16
Reaction score
22
‎1.‎ Watu wenye Mafanikio na Ufanisi huwa na sifa mbili ‎midomoni mwao: Tabasamu na Ukimya. Tabasamu ‎husaidia kutanzua matatizo, vile Ukimya husaidia ‎kuepuka matatizo.‎

‎2.‎ Unaweza kuchanganya Sukari na Chumvi pamoja. Ila ‎sisimizi huchkua Sukari tu, na kuondoka nayo, na ‎kuacha Chumvi. Chagua marafiki wema, katika ‎maisha yako, ili uyaboreshe na kuyaona kuwa ni ‎matamu.‎

‎3.‎ Ukishindwa kufanikisha ndoto zako, badilisha mbinu, ‎usibadilishe Mola wako.‎

‎4.‎ Kumbuka daima! Miti hupukutisha majani yake, ili ‎istawi zaidi. Haibadilishi mizizi yake!‎

‎5.‎ Hutafika uendako, iwapo utakatisha safari ili ‎umrushie jiwe kila mbwa anayekubwekea njiani!‎

‎6.‎ Wenye kukuchukia, hawatakosa la kusema! Hata ‎wakuone unatembea juu ya bahari, watasema ni kwa ‎sababu hujui kuogelea! Hata kama utacheza ngoma ‎juu ya Bahari, basi watakushutumu kuwa ‎unawarushia vumbi!‎

‎7.‎ Panga kuishi kwa Amani na Utulivu; kwa ‎kushughulikia mambo yako, kwa nguvu zako ‎mwenyewe; hutakuwa mtumwa wa mtu!‎

‎8.‎ Kumbuka daima! Usitiane miereka na nguruwe; ‎mtachafuka nyote wawili. Ila nguruwe atafurahi na ‎kuona raha!‎

‎9.‎ Kumbuka, daima usibishane na mjinga! Hata werevu ‎watashindwa kutofautisha nani ni mjinga kati yenu!‎
 

Haya maneno nimeyapenda sana, ila namba 8 mmmmmmmmhhhhhhhhhh. Imenivutia zaidi.
 
‎1.‎ Watu wenye Mafanikio na Ufanisi huwa na sifa mbili ‎midomoni mwao: Tabasamu na Ukimya. Tabasamu ‎husaidia kutanzua matatizo, vile Ukimya husaidia ‎kuepuka matatizo.‎
nakumbuka jana katika kupata ulabu huku naangalia game ya Man U, ile sehem baamedi huwa hawapendi kutumwa madukani, nikamuita mmoja akaninunulie vocha, alinuna ila alivyoniangalia usoni akakuta natabasamu na ye bana si akatabasamu, mdogomdogo akasogea dukani na vocha ikaja. tabasam bana ni silaha mda mwingine.
‎8.‎ Kumbuka daima! Usitiane miereka na nguruwe; ‎mtachafuka nyote wawili. Ila nguruwe atafurahi na ‎kuona raha!‎
hii namba nane nimeipenda chief
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…