Hekaheka za Mikundeni, CHADEMA na Limbu

Hekaheka za Mikundeni, CHADEMA na Limbu

Dotto C. Rangimoto

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2012
Posts
1,985
Reaction score
1,286
HEKAHEKA ZA MIKUNDENI.

limbu.jpg

Haikuwa mikundeni,
Seuze michorokoni?
Siulize kulikoni,
Uliza kaanza nani?

Halikwisha moyoni,
Litakomaje machoni?
Donda lipone zamani,
Kovu labaki ngozini,

Haikufaa shambani,
Litafanaje kondeni?
Kiroboto na kunguni,
Wana undugu jamani.

Alia wako mwandani,
Mie nitafanya nini?
Mbichi zimekuwa kuni,
Kavu zitakuwa nini?

Ana wema hayawani,
Yule mlala bomani,
Nikuweke kundi gani?
Hufai hata bomani.

Njano5
0762845394 whatspp
0784845394
 
Sijui ubongo wangu unachagua vitu vya kuelewa,maana sijaewa kabisa
 
Unajinasibu kuandika mashairi hata kanuni za mashairi hujui, hakuna urari wa vina na mizani. Bull Shit!!!
 
Naona Limbu yupo na Mbowe na Slaa wanapanga mipango.
 
Kazi aliyotumwa Limbu imemshinda!!!!
 
Unajinasibu kuandika mashairi hata kanuni za mashairi hujui, hakuna urari wa vina na mizani. Bull Shit!!!

We Tatizo lako haujui aina za mashairi yaani mashairi ya kisasa (hamna ulazma wa kufuata kanuni za urari wa vina na mizani) na Yale ya kimapokeo ( huzingatia kanuni za urari wa vina na mizani). usijitape kukosoa vitu usivyovijuaa
 
Uko sahihi kabisa, hata hivyo shairi langu si la kisasa bali ni la kimapokeo na limefuata kanuni zote za kimapokeo. Vina na urari vyote viko sawa, kil a kipande cha mstari kina silabi nane, na mwisho wa kila kipande kumeishia sialabi "ni".

ila watu wanapenda kukokosoa sababu ujumbe haukumfurahisha.
 
Back
Top Bottom