PostGE2025 Heche: Vyombo vya kimataifa vifanye uchunguzi kilichotokea Oktoba 29

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Makamu Mwenyekiti Bara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) John Heche ametaka uchunguzi ufanyike na vyombo vya kimataifa kuhusu kilichotokea nchini tarehe 29 Oktoba 2025 siku ya uchaguzi Mkuu na sio vyombo kutoka ndani ya nchi kwa kuwa ndivyo vinavyotuhumiwa.

Heche ameyasema hayo hii leo tarehe 12 Novemba 2025, kwenye viunga vya Mahakama Kuu masjala ndogo ya Dar es Salaam, mara baada ya kuahirishwa kwa shauri la uhaini linalomkabili mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu.
Your browser is not able to display this video.
 
Na pia wasisahau kukusanya taarifa ya watu waliopotea/walioawa/Waliojeruhiwa kuanzia Oct 29 mpaka tar 3 Nov 2025.
 
"Tunapokea ushauri wenu ila mstuelekeze la kufanya".......mtu moja kasema hivo
 
Kama watafunguliwa milango na by the time wanafunguliwa milango kila kitu kitakuwa kimeshasafishwa na witnesses kupangwa usishangae wakawa another rubber stamp kwamba hali ilikuwa sawa sawia apart from few mishaps...
 
Kama watafunguliwa milango na by the time wanafunguliwa milango kila kitu kitakuwa kimeshasafishwa na witnesses kupangwa usishangae wakawa another rubber stamp kwamba hali ilikuwa sawa sawia apart from few mishaps...
Unadhani huo uchunguzi wa kimataifa ni kama huu wa kina murilo wa kusema nilisikia maneno ya Lissu nikahamasika?

We undhani kwa nini wanaogopa vyombo vya nje kuja kuchunguza?

Waombe tu waruhusu hao wachunguzi wa nje waje wafanye uchugunzi wa mdude au Polepole uone watu watakavyoumbuliwa

Wale ni Next level
 
Wa wapi Scotland Yard - Kifo cha Auko mwisho wa siku walipata mtu without reasonable doubt au waliongezea sintofahamu

Je waliopeleleza ni nani aliangusha ndege ya Juvénal Habyarimana wafaransa wakasema huenda ni Kagame na wengine wakasema haiwezekani na sio Kagame huenda ni mke wake

Moral of the Story uchunguzi unategemea sana msaada na leeway mtakayopewa ingawa ni muhimu sana kwa kuleta watu kutoka nje kuchunguza sababu waliopo hawaaminiki ili hitimisho lifikiwe watu wafungwe na imani katika vyombo za usalama irudi na sio tarehe 29 tu, bali vifo vyote visivyoelezeka na watu kutekwa hata kama evidence itakua ni siku zimepita watu wafungwe na kufukuzwa kwa kutokuwajibika...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…