Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,885
Kuna hisia zinajengwa kwamba Makontena ya mchanga wa dhahabu (copper concentrate) au makinikia ya shamba yaliyokua yanasafirishwa nje ya nchi, yanasafirishwa kwa wizi au kwa njia za kificho. hii ni siasa ya kujitafutia umaarufu usio na msingi.
Ni kweli kwamba usafirishaji huu umesababishia taifa letu hasara kubwa sana, lakini siku zote makontena yamesafirishwa kihalali na kwa mujibu wa sheria na mikataba ambayo taifa letu limesaini, kwahiyo kusahihisha hilo sio kutoa tamko bali kuleta bungeni mikataba hiyo ili ipitiwe upya.
Michanga hii imepigiwa kelele mda mrefu na wabunge wetu lakini kwasababu ya uchache wao walipuuzwa. Sheria zililetwa na kupitishwa kwa hati ya dharura, kuzuia kwa ghafla tu vitu vilivyo kwenye mikataba ni kusababishia nchi hasara kubwa zaidi.
tayari Accacia wametangaza kwamba wanapata hasara ya 1m USD kila siku tangu kutolewa tamko la kuzuia usafirishaji huo. Sababu za wao kusafiri mchanga huu ni kwamba Tanzania hakuna tanuri au (smelter) ya kuchomea kiwango cha dhahabu kinachobaki kwenye mchanga kiasi cha 20% baada ya kusafisha kwenye migodi yao ambayo kwa Tanzania ni Buzwagi na Bulyahuru.
Ukisoma sera ya madini 2009 kifungu cha 5.11 kinaeleza wajibu wa serikali katika kuhamasisha uongezaji wa thamani ya madini nchini.
Lakini kutoa tamko overnight na kuonesha kwamba kuna kitu cha wizi kimekamtwa ambacho kilikua hakijulikani sio kweli kwasababu michanga hii inabebwa migodini na huko kuna watu wa serikali kuanzia TMAA,TRA na hata watu wa usalama, kuna wakuu wa wilaya, wakuu wa Mikoa na pia hii michanga inasafirishwa mchana kwenye barabra zetu.
My take:
Serikali ilete hiyo mikataba na sheria hizo zilizopitishwa kipindi hicho bungeni tuzifanyie marekebisho kuzia tu kwa tamko kutasababisha hasara kubwa kwa nchi maana tutashitakiwa kwenye mahakama za kimataifa.
Hii pia itukumbushe sheria ya mafuta ilivyopitishwa kishabiki na wabunge wa ccm tena kwa hati ya dharura nategemea nayo itatoa mwanya wa kuibiwa kama huu wa madini kama isipoangaliwa upya.