Hebu huyu Eddo Kumwembe asiendelee kunichefua tafadhari

EngutanK

Member
May 3, 2021
99
244
Mwaka 1982 tarehe Fulani tulikuwa tunaangalia mpira Jamatini moja mjini Lindi, Ilikuwa ni mechi za kombe la dunia zilizofanyika nchini Hispania.

Tulikuwa tunaangalia mikanda ya mechi zilizokuwa zimeisha chezwa na matokeo yuke tulikuwa tunayajua. Mikanda hiyo ilikuwa inarekodiwa na television ya Zambia, mamikanda Fulani makubwa kama mikate.

Siku hiyo tulikuwa tunaangalia watu watatu mimi ambaye kitaaluma ni Medical doctor, Baba yake Eddo Kumwembe ambaye mimi nilikuwa namwita jina la taaluma yake Advocate Kumwembe jina halisi ni John Kumwembe na Sengwaji ambae alikuwa ni Mkandarasi wa ujenzi. Kuangalia video hizo sehemu ya Jamatini alikuwa ni fever tu kutokana na nyazifa zetu wakati huo.

Siku hiyo tulikuwa tunaangalia mkanda wa video kati ya Brazil na Argentina , matokeo ni Brazil ilishinda 3 -1. Brazil walikuwemo Dr. SCRORATES, Bebeto na wengine, Argentina alikuwemo gwiji Maraddona katika mechi hiyo Maradonna alitolewa kwa kadi nyekundu.

Nachotaka kumwambia huyu dogo Kumwembe sina uhakika kama 1982 alikuwa amaeisha zaliwa, Mwenzetu Sengwaji alikuwa ana mawazo kama ya Eddo kwa bahati mbaya alilopoka akasema aise Maraddona anacheza zaidi ya PELE, duuu Advocate Kumwembe alimfokea kama mtoto mdogo akimkataza kabisa asimulinganishe Pele na huyo teja Maraddona.

Eddo ukome kumulinganisha Pele na Maradona au Messi kumuenzi baba yako kwa sababu zifuatazo:

Pele angeweza kucheza vizuri zaidi ya Messi au Maraddona kama nay eye angekuwa kizazi hiki ambacho kila kitu kimeboreshwa, Mipira, viwanja pia sheria,

Pele alikwa anacheza gozi la ng`ombe hawo wengine vimpira vyao lainiiii, lakini pia mabeki waliokuwa wanamkaba Pele wakiwakaba hao akina Messi wanavunjika vipande vipande.

Eddo hupenda sana kutumia kigezo cha Pele hakucheza ulaya, Pele hakucheza ulaya siyo kwa kupenda kwake bali alitangazwa na taifa lake la Brazil kwamba yeye ni nyala ya taifa na kwamba hauzwi kwa pesa yoyote aliahidiwa angepewa pesa yoyote anayotaka akiwa pale Brazil tu na anakula kuku mpaka leo.

Lakini pia sisi wote tumewaona Pele na hao wengine lakini Eddo kamwona Messi tu labda na Maraddona.

Mwaka 1972 PELE na SANTOS Yake walialikwa na Yanga babati mbaya wakati ulipowadia mke wa PELE akajifungua ikabidi Santos ije bila Pele, ziala hiyo ilifutwa kwani Pele bila Santos ni kazi bure, lakini eti PSG ikialikwa bongo bila hata Messi itakuja tu.

Tukija kwenye uchezaji pele alikuwa na vitu vyote, speed, Alikuwa anatumia miguu yote kufunga, alikuwa anapiga vichwa , faulo pia alikwa anafunga kwa mpigo ya kunyumbulika yaani tik-tak, scorpion kick.scissorsers –kick vitu vyote lakini MESSI ana foot work tu.

Eddo hebu mheshimu baba yako.

Niko Mtwara maeneo ya Ligula nimestaafu Eddo ukitaka kuniona muulize Shilingi dalali au referre Jimbwi watakuelekeza nilipo uje uone mapicha amayo wewe huna na nitakuachia.

N.B Advotcate Kumwembe na Sengwaji wote ni marehemu mimi bado nipo.
 
Edo kumwembe anayo andika au kusema ni mawazo yake binafsi ni Kama mashabiki wengine wanavyo toa maoni yao. Watu wanao uelewa mpira Duniani wanashangaa jinsi tuzo inavyo poteza uhalisia na kuwa biashara binafsi za watu wachache.
 
Ila sijuagi kwanini watu wa zamani tunaaminigi mambo yetu ya zamani ndio bora always na hatutakagi kabisa kuona vizazi vipya vinakuja na mambo mazuri juu yetu. Always tunakuwa wakali mno mtu akisema kitu fulani cha siku hizi ni bora kuliko cha zamani.

Anyways kila mtu atazeeka tu na njia ni moja.
 
Mambo ya baba yake Eddo Kumwembe yanatuhusu nini? Na kuna ulazima gani wa mawazo ya Eddo Kumwembe kufanana na mawazo ya baba yake?


Nimejitahidi sana kua na adabu maana unaonekana unakaribia umri wa baba yangu. Ila busara huna!
 
Yani nikiangalia Michambo yako kwenye huu basi sijaona dalili ya kuwa Mwaka Una miaka zaidi ya 50 kama ulivyojieleza kwenye Uzi kubwa Mwaka 1982 unaangalia World Cup.
Ninachokiona hapa ni kuwa unasubiri matokeo ya Mtihani uliomalizika last week wa Kidato cha nne.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom