Hayawi hayawi sasa yamekuwa...

Hayawi hayawi sasa yamekuwa...

Phlagiey

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2013
Posts
3,500
Reaction score
1,688
Ni muda umepita nikiishi maisha ya kibachera baada ya kukwepa mizinga kibao ya kina Mwajuma huku wengine ni kila kwa mkopo, ila sitamsahau Pude pamoja na ujanja wangu wote wa kukwepa mizinga lakini hapa nilitekwa na bastora ya toi mikono nikaweka juu, nilingia kichwa kichwa mtoto akanikoleza kumbe alikuwa ananitega kushituka nimesha honga simu mpyaa dah...Kwa mkono wangu nikachana wallet nakutoa misimbazi kadhaa.


Movie ya ubachera ina season nyingi sana ila kali na ngumu kuliko zote ila ya pale gheto zile scrept za kujipikia, kufua, usafi wa chumba, hapa ndo huwa sasa star wa movie anafikilia kumtafuta mwandani kama nilivyo fanya mimi.


Niwengi nimekuwa nao katika mahusiano na kuhaidiana mengi sana likiwemo la kuona lakini hatukuweza kutimiza ahadi, hatimae leo nimebainika.



Kila kitu kimeshakuwa tayari kamati imeweka mambo sawa, na suti yangu ya single batani nilio enda kushonesha kwa fundi imesha kuwa tayari, japo nilimwona fundi kaivaa jumapili iliyopita kanisani kumuuliza akaniambia alikuwa anaitest nikaona isiwe tabu sanaa... nisije nikawa naingilia majukumu yake. Kiukweli kaitoa safi sana..Siamini siku hiyo mmasai ndani ya suti sijui itakuwaje sijui nitatembeaje mwondoko gani utafaa kwa matumizi!! Nishazoea kupiga mitambo huko mitaani nikiwa natembeza kiloriti(dawa) sipati picha siku hiyo ya suti..


Tukio litakuwa ni mwezi huu..
29/2/2014 ndo nitakuwa nafunga ndoa!!!


Karibuni sana jamaa zangu...!!!
 
Masai kapatikana leo ...........!!
 
Pole sana maana kalenda yako cjui ya wapi...........hakuna tarehe hiyo kwa mwaka 2014
 
mkuu Phlagiey, hii ni ndoa ya kiasili au?

usije kutuambia tukutane machungani bana! hahaaa!!

nipo nasubiri matokeo...
 
Last edited by a moderator:
..hiyo tarehe ya ndoa tu, imenifanya nijue kuwa UMEWATUSI WOTE waliotangulia hapo juu..unaumwa uso wewe!!!!!!! hapo kapona dray tu
 
Back
Top Bottom