Hayati Mwalimu Nyerere aliiogopa CCM - Prof. Mbele

Hayati Mwalimu Nyerere aliiogopa CCM - Prof. Mbele

hokani

Senior Member
Joined
Mar 26, 2013
Posts
102
Reaction score
77
Ingawa alikuwa mwanzilishi wa CCM, kwa nia njema ya kuendeleza mapinduzi katika nchi yetu, miaka ilivyozidi kwenda Mwalimu Nyerere alishuhudia jinsi CCM ilivyobadilika na kuwa mzigo kwake na pia tishio kwa usalama wa Taifa.

Mwaka 1993 Mwalimu alichapisha kitabu kiitwacho Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania (Harare: Zimbabwe Publishing House, 1993). Pamoja na mambo mengine katika kitabu hiki, Mwalimu alisema kuwa kuna kansa katika uongozi wa CCM. Nanukuu baadhi ya maneno yake:

Chama cha Mapinduzi, kwa sababu ya uzito wa historia yake, hadhi ya jina lake, mfumo wa wavu wake, mazoea ya watu, na ubovu wa Vyama vya Upinzani, kinaweza kuchaguliwa na Watanzania, pamoja na kansa ya uongozi wake. Au watu wanaweza wakachoka, wakasema, "potelea mbali:" wakachagua Chama cho chote, ilimradi tu watokane na kansa ya uongozi wa CCM. Hainifurahishi kuyasema haya, lakini uhai
wa Nchi yetu unataka yasemwe.
(Ukurasa 61)


Mwalimu hakuishia hapo, bali aliongezea namna hii:
Nilisema awali kwamba kansa ya uongozi ndani ya Chama cha Mapinduzi isingekuwa ni jambo la kutisha sana kama tungekuwa tumeanza kuona Chama kizuri cha upinzani kinachoweza kuiongoza Nchi yetu badala ya CCM. Ubovu wa uongozi ndani ya CCM ndio uliofanya nikapendekeza tuanzishe mfumo wa Vyama Vingi.

Nilitumaini kuwa tunaweza kupata Chama kingine kizuri ambacho kingeweza kuiongoza Nchi yetu badala ya CCM; au ambacho kingekilazimisha Chama cha Mapinduzi kusafisha uongozi wake, kwa kuhofia kuwa bila kufanya hivyo kitashindwa katika uchaguzi ujao. Lakini bado sijakiona Chama makini cha upinzani; na wala dalili zo zote za kuondoa kansa ya uongozi ndani ya CCM. Bila upinzani mzuri wa nje, na bila demokrasia halisi ndani ya Chama cha Mapinduzi, Chama hiki kitazidi kudidimia chini ya uzito wa uongozi mbovu. Kwa hali yetu ya kisiasa ilivyo nchini hili si jambo la kutarajia bila hofu na wasi wasi! (Ukurasa 66)

Ni wa-Tanzania wangapi wenye utamaduni wa kusoma vitabu? Ni wangapi wanaosoma vitabu vya Mwalimu Nyerere? Ni wazi kuwa umbumbumbu miongoni mwa wa-Tanzania ni neema kwa CCM.

Ikumbukwe tu kwamba wakati Mwalimu alipoandika, upinzani haukuwa makini na wenye nguvu kama ilivyo leo. Nyerere angekuwa hai leo, nina hakika angeungana na CHADEMA katika kupambana na ufisadi. Yeyote ambaye amefuatilia mawazo ya Mwalimu katika hotuba na vitabu vyake mbali mbali, atakubaliana nami kwa hilo.
 
Soma TUJISAHIHISHE utapata dhana nzima ya chama cha siasa na aina ya viongozi wanaostahili kuongoza nchi. Mwalimu ni Encyclopedia au information bank!!!
 
Kumbe wazo la vyama vingi ni la Nyerere!sasa naelewa kwa nini baada ya mwalimu kufariki vyama vya upinzani "vinakiona cha moto" kuanzia visu vya Mahita hadi ugaidi wa wahaya!sitashangaa ukija kusikia wazo la kurudisha mfumo wa chama kimoja tena baada ya kuharamisha upinzani ili uonekane ni kitu kisichofaa ili watakaposema wanafuta upinzani,kelele ziwe kidogo!ila situation haiendi vile wanavyotaka.!na dunia haiwezi kukaa kimya!
 
Kwanza, nikupongeze kwa kutukumbusha kitabu hiki. Hivi unafahamu misukosuko aliyopata Mwl. kufuatia uandishi wa kitabi hicho? Unajua kilichapwa baadaye nakala zote zikanunuliwa na kufichwa hatmaye baada ya jitihada kubwa ndio kikachapwa kwa siri ili kisiwe hijacked? Kwa ufupi, Nyerere sio kwamba alikuwa adui wa CCM au tuseme aliiogopa. Hapana, Mwalimu alikuwa muwazi kukosoa, hakuwa mfitini au mwoga, ndo maana maneno yake sio tu kwenye kitabu hicho tu bali kwenye vitabu, hotuba na matendo yake mengi, Nyerere alikuwa tofauti na mambo ya ovyo.

Mimi hupenda sana kusoma hotuba zake, Kama Manyerere Jackton anavyosema, Nyerere was beyond! Hebu chukua hii nukuu toka kwenye kijitabu cha Nyerere- TUJISAHIHIUSHE!

"Makosa ni makosa na dhuluma ni dhuluma japo watendao makosa hayo au dhuluma ile ni wakubwa au ni wengi. Chama kinachopenda ukweli na haki, hakina budi kiwape wanachama wake uhuru na nafasi ya kusahihisha makosa na kuondoa dhuluma. Wanachama hawana budi waone kuwa ni wajibu wao kuutumia uhuru huo na nafasi hiyo. Wanachama wasio tumia uhuru huo, na nafasi hiyo, kwa sababu ya kuogopa kuchukiwa au kupoteza nafasi zao, wanafanya kosa kubwa la unafsi, ambalo ni adui wa haki na ukweli"

Nani atapenda kutumia maneno haya ya Mwalimu kujisahihisha? Ni rahisi CHADEMA na wapinzani kumnukuu Mwalimu kuliko CCM mana hawapendi "KUJISAHIHISHA".
 
Kwanza, nikupongeze kwa kutukumbusha kitabu hiki. Hivi unafahamu misukosuko aliyopata Mwl. kufuatia uandishi wa kitabu hicho? Unajua kilichapwa baadaye nakala zote zikanunuliwa na kufichwa hatmaye baada ya jitihada kubwa ndio kikachapwa kwa siri ili kisiwe hijacked? Kwa ufupi, Nyerere sio kwamba alikuwa adui wa CCM au tuseme aliiogopa. Hapana, Mwalimu alikuwa muwazi kukosoa, hakuwa mfitini au mwoga, ndo maana maneno yake sio tu kwenye kitabu hicho tu bali kwenye vitabu, hotuba na matendo yake mengi, Nyerere alikuwa tofauti na mambo ya ovyo.

Mimi hupenda sana kusoma hotuba zake, Kama Manyerere Jackton anavyosema, Nyerere was beyond! Hebu chukua hii nukuu toka kwenye kijitabu cha Nyerere- TUJISAHIHISHE!

"Makosa ni makosa na dhuluma ni dhuluma japo watendao makosa hayo au dhuluma ile ni wakubwa au ni wengi. Chama kinachopenda ukweli na haki, hakina budi kiwape wanachama wake uhuru na nafasi ya kusahihisha makosa na kuondoa dhuluma. Wanachama hawana budi waone kuwa ni wajibu wao kuutumia uhuru huo na nafasi hiyo. Wanachama wasio tumia uhuru huo, na nafasi hiyo, kwa sababu ya kuogopa kuchukiwa au kupoteza nafasi zao, wanafanya kosa kubwa la unafsi, ambalo ni adui wa haki na ukweli"

Nani atapenda kutumia maneno haya ya Mwalimu kujisahihisha? Ni rahisi CHADEMA na wapinzani kumnukuu Mwalimu kuliko CCM mana hawapendi "KUJISAHIHISHA".
 
Ahsante sana Prof. Mbele kwa kutukumbusha hayo maneno ya busara ya hayati baba wa Taifa, nafikiri ni mwiba mkali kwa CCM. Maneno hayo aliyesema Nyerere 1993, nafikiri wakati huo CHADEMA kilikuwa bado hakijawa chama MAKINI na Kikubwa cha UPINZANI. I wish kama angekuwepo leo angekubali kabisa kwamba CHADEMA ni CHAMA MAKINI CHA UPINZANI ambacho kiko tayari kuchukua dola. Masikini Nyerere amekufa bila kuona hiyo ndoto yake ya CHADEMA kuchukua dola 2015 ikitimia.

BTW, Prof Mbele hiyo "hokani" ndiyo ID yako ya JF. Wasalimie wote huko Marekani I miss you guys so much.
 
Nisaidieni! Hayati Mwalimu aliposema "CCM SIO MAMA YANGU! Alikua anamaanisha nini?
 
Kwa wale wasiojua sababu za Kikwete na genge lake kumchukia Mwalimu kwa matendo yao, basi someni hizo nukuu zake hapo juu ili mjiridhishe!!
 
Nisaidieni! Hayati Mwalimu aliposema "CCM SIO MAMA YANGU! Alikua anamaanisha nini?

Maana yake ilikuwa kwamba yeye asingeweza kukaa ccm milele bali alikuwa na uhuru wa kujitoa/kukihama chama!!!
 
Nisaidieni! Hayati Mwalimu aliposema "CCM SIO MAMA YANGU! Alikua anamaanisha nini?

Nenda kasali kwenye kaburi lake ili akupe jibu. Si unajua tayari yeye ni Mtumishi wa Mungu kwa mujibu wa Vatican.
 
Soma TUJISAHIHISHE utapata dhana nzima ya chama cha siasa na aina ya viongozi wanaostahili kuongoza nchi. Mwalimu ni Encyclopedia au information bank!!!

Kumbuka tujisahihishe alikiandika May 1962. Kama ndani ya hii miaka 51 hawajakielewa basi kuna haja ya kuwaita madhaifu.
 
Chama alichokianzisha yeye akakitawala kwa miaka mingi bila kukiwekea misingi imara halafu anakuja kuwalaumu viongozi wa CCM ambao ni product yake mwenyewe!
 
Soma TUJISAHIHISHE utapata dhana nzima ya chama cha siasa na aina ya viongozi wanaostahili kuongoza nchi. Mwalimu ni Encyclopedia au information bank!!!

Nyie wakina Manyerere mnapenda kutuaminisha kuwa ni wafuasi wa maandiko ya mwalimu Nyerere at the same time mnapokea mshiko wa bahasha kutoka kwa mafisadi wakina Karamagi na Lowassa!!! Acheni unafiki huo.
 
Back
Top Bottom