Hayati Magufuli aliwahi kusema Rostam Mwekezaji bora na hakuna aliyehoji

Hayati Magufuli aliwahi kusema Rostam Mwekezaji bora na hakuna aliyehoji

Blasio Kachuchu

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
573
Reaction score
359

Nchi nyingi za Afrika zimekuwa zikibadilisha mitazamo na sera zake kuhusu uwekezaji mara kwa mara, jambo ambalo mara nyingine huleta changamoto katika kujenga mazingira thabiti ya biashara. Tanzania nayo haiko mbali na hali hii.

Mfano unaoonekana wazi ni ule wa Rostam Aziz, ambaye aliwahi kutunukiwa na Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dk. John Pombe Magufuli, cheo cha Mwekezaji Bora wakati wa uzinduzi wa kiwanda chake cha ngozi mkoani Morogoro. Rais alisisitiza kuwa wawekezaji wa aina hiyo ndio wanaohitajika ili kuinua uchumi wa Taifa, huku akimtaka Rostam kuendelea kuwashawishi wawekezaji wengine kufika nchini.

Hata hivyo, hali imebadilika kwa sasa. Rostam Aziz, ambaye alisifiwa kwa jitihada zake, sasa anapakwa matope na kutuhumiwa kuwa mhujumu uchumi. Ni kana kwamba hakuna taasisi za Serikali zilizo na mamlaka ya kusimamia na kulinda rasilimali za nchi, na badala yake anaonekana kama mtu mwenye nguvu kubwa kuliko dola.

Cha kushangaza zaidi ni kwamba baadhi ya wanaoibua tuhuma hizi waliwahi kuwa na nafasi kubwa serikalini – nafasi ambazo ziliwawezesha kutoa ushauri au kupinga mapema kama kweli kulikuwa na hoja za msingi dhidi ya uwekezaji wa Rostam.

Kwa taifa linalohitaji sana wawekezaji ili kuchochea ukuaji wa uchumi, siasa za kupakazana matope katika eneo nyeti la uwekezaji zinaweza kuleta madhara makubwa. Badala ya kujenga mazingira rafiki, tunaweza kuishia kuwakatisha tamaa wawekezaji wa ndani na wa kimataifa, hali itakayosababisha Taifa kupoteza nafasi za biashara, ajira, na ushirikiano wa kimataifa.

Ni wazi kwamba, kama tunataka Tanzania izidi kung’ara kiuchumi na kuaminika mbele ya macho ya dunia, tunapaswa kuacha siasa za maonevu na badala yake tujenge mazingira yenye uthabiti, uwazi na uaminifu. Uwekezaji unahitaji sera endelevu na usalama wa kisheria ili mwekezaji yeyote awe na uhakika kwamba kesho hatageuzwa adui baada ya kusifiwa leo.
Soma > Rais Magufuli afungua kiwanda cha Ace Leather kinachomilikiwa na Rostam Aziz mjini Morogoro
 
Kama kipindi cha magufuli alifuata sheria za uwekezaji na kulipa kodi stahiki kwa taifa basi alikuwa muwekezaji borankabisa..

Kwa sasa sidhani maana kununua mali zetu za urithi wetu kwa pesa ya karanga na kurubuii rubuni viongozi wetu basi amekengeuka na inaonyesha uhalisia wake ujambazi wa mali zetu itakuwa kipindi cha magufuli alikuwa akimuigizia Mangu tu.
 
Kwa hiyo unataka kusemaje?
Miafrika bhana ... ndo mana ikauzwa UTUMWANI KAMA NGEDERE
 
Mkuu unashindana na Mwendazake!...khaaa!....woooooy!!!
All in all alikuwa na madhaifu mengi ila mazuri aliyoyafanya ndiyo yanayowapiga na kitu kizito, Pumzika JPM
 
Back
Top Bottom