Haya ni mateso wanayopata walimu wetu

del moe

JF-Expert Member
Apr 4, 2016
827
1,023
Ukiangalia photo hapo... Huo ni mtihani wa upimaji darasa la nne ngazi ya wilaya.
Nijambo zuri sana na nampongeza afisa elimu wa wilaya hiyo kwa kujali watoto wetu. Kinacho nishangaza
1.mtihani mhimu kama huu umeandikwa ubaoni maswali yote 25 ikiwemo na comprehension
Najaribu kuwaza kwa sauti maisha ya Leo na kukua kwa tekinolojia bado walimu wetu wanandika mtihani ubaoni?

2 angalia ubao , umechimbika kisi kwamba unaweza panda mgomba na ukaota vizuri tu!

Hivi afisa elimu hilo umelizingatia? Bado vitisho umeona hiyo scene shot wakifelisha wanajieleza....


Ombi langu mamlaka husika wasaidieni walimu wetu





IMG_20180517_084917.jpg
View attachment 779702
Screenshot_2018-05-17-12-05-38.jpg
 
Unahisi kwanini siku za Karibuni waalimu thamani yao imeshuka?

Zamani Mwl alikuwa anaheshimika sana na alikuwa anaonekana kama Mtu muhimu katika jamii ila nahisi hata wao hawajui thamani yao muda mwingine.
 
Mamlaka zimekusikia mwalimu. Msalimie huyo mwenye picha yake, mwambie amependeza.
 
Walimu zamani walikuwa wanaandika maswali 50 ubaoni na bado waliheshimika, bado tulifaulu. Lkn hawakuwa na maslahi mazuri, hawakuwa wanapanda daladala bure nk. Acheni Mwalimu aitwe mwalimu kuandika unaoni ni moja ya kazi zake za msingi.
Lkn pia kama wewe ni mwalimu huzijui Code of Conduct za kazi yako, iweje sms ya kikazi ya Boss wako uianike kwenye media? Chukua hatua utakuja kuta kumekucha.
 
Umekosea sana kuweka jina la wilaya yako,ni rahisi kutrack shule yenye ubao huo na kumjua mpiga picha,utakapo fukuzwa kazi,njoo tuambie.
Hi awamu ni pongezi na shangwe sio kukosoa.
Watch out!
 
Haha nimekuja kuna hilo shimo la kupandia mgomba, aisee poleni walimu.
 
Yapo mambo ambayo serikali inayashughuliakia bila kuyatangaza mfano hili tayari limeanza kuchukuliwa hatua mkuu wa mkoa wa rukwa ameshamwagiza katibu tawala wa mkoa huo kumchukulia hatua za kinidhamu mkurugenzi wa wilaya ya kalambo kwa kuonyesha uzembe katika utendaji. Kwa kuanzia nahisi inaridhisha
 
Elimu bure Ina changamoto zake pesa hazitoshi..wafanyeje..kuna bwana aliniambia kuhusu hili..
 
wakome tu hawa walimu nyambafu!

wanaisaidiaga sana CCM kwenye chaguzi kwa kubeba mabox yenye kura feki.
 
Mi nadhani wanaoteseka zaidi ni wanafunzi ambao
maswali ubaoni yanafutwa wakati mtu bado
hajamaliza kunakiri.
Serikali iangaalie upya taratibu zinazotumika
ili maboresho yafanyike.
 
ni mfumo mzuri kwani wanafunzi huandikiwa majibu pia ubaoni na hivyo kuondoa midomodomo ya maafisa elimu kuuliza ni kwanini wanafunzi wamefeli.hongereni walimu....naona mtarejea kwenye ethics miradi ikikamilika !
 
Back
Top Bottom