Uchaguzi 2020 Haya ndio tunategemea kuyasikia kutoka kwenye Ilani za vyama vya siasa kwa uchaguzi 2020

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,173
18,486
Ili kuandaa ilani vyama vinahitaji watalaam waziefu na wenye uelewa wa mahitaji ya Watanzania.. Kinyume cha hapo vyama vitajikuta vinaeleza nadharia na mambo ambayo hayatekezeki au kujikuta vinajikita kwenye mambo ambayo siyo muhimu kwa Mtanzania wa kawaida.

Ilani za vyama lazima zijikite kwenye utatuzi wa changamoto na kumwezesha mwananchi kuwa mzachangiaji katika uchumi wa nchi.

Na Ilani lazima iwe na mpango mkakati wa utejelezaji ili kuyafikia mambo yote ndani ya kipindi cha miaka 5.

Na mpango mkakati lazima uwe na malengo yanayo tekelezeka na yanapimika.

Mfano wakisema wanajenga hospitali 30 za wilaya bila kutaja hizo hispitali 30 zimeziba pengo kiasi gani la hospitali za wilaya lengo linakua halina maana sana.

Kwa hiyo vyama vya siasa kabla ya kuja na ilani vinatakiwa viwe vimesha fanya tafiti nankujua ukubwa wa changamoto zinazo wakabili wananchi.

Maswali ya kujiuliza (mfano).

1. Tanzania inahitaji zahanati ngapi, na ngapi zinahitaji kujengwa na ngapi zinahitaji ukarabati.. the same kwa vituo vya afya.

2. Tanzania inahitaji shule ngapi za msingi, ngapi zinahitaji kujengwa na ngapi zinahitaji ukarabati?

Wote tumeshuhudia kazi nzuri ambayo Magufuli ameifanya ya ujenzi wa vituo vya afya lakini hawaja wahi kutwambia hivyo vituo vya afya 400 vimeziba pengo kiasi gani, unaweza kuta Tanzania inahitaji vituo vya afya 3000 zaidi na sisi tunashangilia vituo 400.

Kwa hiyo tunahitaji ilani za vyama zije kwa namba zenye malengo yanayo pimika.

Je tuliwapa dhamana watamaliza matatizo katika secta zifuatazo kwa kiasi gani.

1. Maji ( Je vijini ma mijini) maji yatapatikana kwa kiasi gani.

2. Elimu : changamoto za Miundo mbinu ya elimu Vijiji na mijini ( madarasa, majengo, nyumba za walimu) lina ukubwa gani na watalimaliza kwa ukubwa gani.

3. Barabara kuu .. Mikoa mingapi bado haijaunganishwa na barabara kuu na za mikoa.. kiasi cha kilometer na watalimaliza tatizo kwa kiasi gani na lini?

Kwa ufupi Ilani ambazo zipo jumla jumla ni porojo, Miaka 5 ni ya kazi toka day 1... Ilani kama haina targets na deadlines hiyo ni Ilani Mfu.

Bado natafuta Ilani za vyama vyote.

FB_IMG_1596633452950.jpeg
FB_IMG_1596667393509.jpeg
 
Jamani naombeni msaada kwenye tuta. Tangu asubuhi niko makini huku na kule kwenye mitandao mingine angalau nisikie huko NCCR Mageuzi wagombea Urais ni kina nani hata hawatajwi. Naombeni fununu basi ili na sisi tuweze kuona na kudadavua ilani yao. Au wote wamekimbia kugombea Urais baada ya kuahidiwa wabunge mbao (20) na mwenyekiti wa kinachotawala? Maana naona kila mmoja anataka Ubunge na mpaka mwenyekiti wao. Naombeni msaada wanaotajwatajwa ni kina nani?
 
Nimesikia wagombea karibia wote wamejitoa na mmoja ndio kabaki.. jina ndio sijui
Jamani naombeni msaada kwenye tuta. Tangu asubuhi niko makini huku na kule kwenye mitandao mingine angalau nisikie huko NCCR Mageuzi wagombea Urais ni kina nani hata hawatajwi. Naombeni fununu basi ili na sisi tuweze kuona na kudadavua ilani yao. Au wote wamekimbia kugombea Urais baada ya kuahidiwa wabunge mbao (20) na mwenyekiti wa kinachotawala? Maana naona kila mmoja anataka Ubunge na mpaka mwenyekiti wao. Naombeni msaada wanaotajwatajwa ni kina nani?
 
Kwanini mkuu?
Jamii yetu kufikia level hiyo ya uelewa ambapo wanaweza kuhoji mgombea mambo ya msingi namna hii kwa upana na ukubwa wake inahitaji muda sana kufikia huko. Kwa sasa badala ya kuhoji mambo ya msingi ni kupigia makofi na kelele nyingi za ndio tu kwa wapenzi wa vyama vyetu.

Hebu tuangalie hata kwa wabunge wetu kule mjengoni badala ya kuihoji serikali inapopeleka hoja za bajeti kabla ya kuunga mkono hoja wabunge walipaswa kupata majibu yenye kweli na hakika badala ya majibu mepesi tu ya "mchakato wa upembezi yakinifu unaendelea" au "tutalishughulikia sijui nitakaa na kamati yangu tutalipitia" hapana tunapaswa kupata majibu yaliyotosheleza na sio bla bla bla tu afu mtu anapigiwa makofi mengi mengi tu.

Yaani nchi haijitambui inahitaji nini na iko wapi. Ukiwakuta wapenzi na mashabiki wa vyama wanavyoshabikia wagombea wao utadhani nchi hii tumemaliza matatizo yote, kumbe hata 30% tu hatujaifikia tangu uhuru.
 
Back
Top Bottom