Haya ndio madhara ya Elimu yetu !!!

mtunzasiri

JF-Expert Member
Dec 24, 2012
1,446
988
Copy and paste from Fbook.
Rafiki yangu niliyemaliza nae kidato cha nne 2010 akakosa nafasi ya kwenda kidato cha sita kutokana na ufaulu wake (alikosa credit), akaenda uwalimu wa shule ya msingi, mimi nikajaa misifa ya kwenda kidato cha tano. Nafaulu kidato cha sita naanza mwaka wa kwanza chuo, rafiki yangu anaajiriwa shule moja huko kijiji flani kwa mshahara usiozidi laki 3 nikaona tunalingana tu maana muda huo namimi nina "boom" lisilopungua laki 5 kila baada ya miezi 2, nikajaa misifa kuwa nasoma bado napata na hela wazo la kupembua kuwa huu ulikuwa mkopo na ule ni mshahara halikuwepo na hapo nikawa na matumaini makubwa ya maisha baada ya chuo (nitaajiriwa, nitapata mshahara, nitaoa, nitanunua kiwanja, nitajenga, nk).

Nimemaliza chuo bodi ya mikopo inaleta taarifa kuwa nadaiwa milioni 12 na nisipoanza kulipa kulipa ifikapo mwezi julai 2017 basi nitapewa adhabu ya 10% ya deni hilo (10% ya milioni 12 = ? ) wakati huo najipa tu matumaini kuwa huwenda ktk bajeti ya nchi 2017/18 ajira zaweza kutoka ni muda ambao naambiwa kuwa " MWALIMU WA SANAA HAKUNA AJIRA.

1. Rafiki yangu anawaza akope milioni ngapi benki afanyie miradi yake, mimi nawaza nitazilipaje milioni 12 ambazo nilichofanyia hakipo.
2. Rafiki yangu anawaza mwakani walau akajiendeleze kielimu awe walau na diploma akafundishe sekondari na mshahara upande, mimi nahangaika walau kuomba tempo kweny tuition centre
3. Rafiki yangu ana mke, anajenga na amenambia akimaliza tu nyumba yake atafanya mpango wa kununua usafiri, mimi sina hata kiwanja, naishi kwa watu na binti niliyepanga kumuoa hataki tena kusikia hizo habari na kashasepa

N. B:
"Tusikariri maisha"

Naomba tu mnitumie wimbo wa kalajeremiah "usikate tamaa"

Mwl. Wa Sanaa
 
mambo ya facebook huku yanatuhusu nini mkuu?
binafsi sijasoma ulichokopi...
 
Back
Top Bottom