Panya alimeza kipande cha dhahabu mwenye
dhahabu akachanganyikiwa na kuamua
kumkodi mpelelezi mmoja ili aje amuue panya
aliyemeza dhahabu. Mpelelezi alipofika alikuta
panya zaidi ya 500 lakini alishangaa kumuona
panya mmoja kajitenga,ndipo alipomkamata
na kumuua,alipompasua akakuta kipande cha
dhahabu akamkabidhi mwenyewe.Yule jamaa
alipigwa na butwaaa huyu mpelelezi alimjuaje
yule panya ikabidi amuulize.
Jamaa:aisee we mkali,ulijuaje kama huyu
ndiye panya aliyemeza dhahabu?
Mpelelezi:hawa panya nao ni kama raia
Watanzania wakiwa na mali hujitenga na
wenzao.