Haya maisha haya! Acheni tu

Internet haipotezi kumbukumbu.....
 
Hawa wapumbavu ndo huwa wanafanya hata watu wengine wenye shida 'genuine' wasisaidike...Yaani matapeli yamejaa kila kona
 

Ni kweli kwenda chuo sio guarantee ya kutoboa maisha,lakini tusisahau kuwa elimu ni ufunguo wa maisha. Kutokana na maelezo ya ndugu yetu, anaonyesha anamsaka elimu kwa udi na uvumba. Utagundua kuhangaika kote huko, nia ilikuwa ni kupata fedha ya kugharamia elimu, lakini kwa bahati mbaya mambo hayakuwa kama alivyotegemea.

Kwenye nia kuna njia, ndugu yetu usikate tamaa, endelea kupambana, utafika utakako. Magumu uliyokutana nayo yasikukatishe tamaa, badala yake yakuimarishe uweze kusonga mbele. Kwa sisi wenye imani, hayo uliyopitia tunachukulia kama majaribu tu na kwamba Mungu hajakuacha. Yawezekana Mungu alikupitisha huko ili kukuepusha na jambo baya zaidi (kibinadamu, kuamini hili ni ngumu), lakini pia tunaamini mtu akianguka, husimama tena na kuendelea na safari.

Kwa hiyo ndugu yangu ninachotaka kusema hapa ni kuwa, kazania kutimiza unachoamini kutoka moyoni mwako. Kutokana na maelezo yako hapo juu, unaamini elimu ndiyo mkombozi wako, lakini ikajitokeza changamoto ya gharama, lakini kama una nia ya dhati, utaishinda changamoto hii na hatimaye kufikia malengo yako. Mungu awe pamoja nawe.
 
Niwatoe wasiwasi Ushimen na wengine. Kuna baadhi ya vipengele sijaviweka wazi kwa sababu ya privacy. Alafu sometime hii simu Kuna ndugu huwa wanaitumia. Ndo maana ile post ya kufeli kidato Cha nne imeandikwa na binti (rejea uisome vizuri).

Kama binadamu ukiona hivo lazima upate wasiwasi lkn Sina Nia mbaya.
Hata hivo sijaomba hela Kama hela nimeomba connection. Kwa lolote lile tutaandikishana kisheria na wadhamini watakuepo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…