Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,746
- 25,644
Nafasi ambazo hazikupata watu ni ya uwaziri wa Maliasili na Utalii ambayo baadaye ilijazwa na Profesa Jumanne Maghembe, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, baadaye akapewa Profesa Makame Mbarawa, Wizara ya Fedha na Mipango akapewa Dk Philip Mpango, Wizara ya Elimu, Sayansi Teknolojia na Ufundi akateuliwa Profesa Joyce Ndalichako.
Kati ya mawaziri hao, wasiofanikiwa kuvuka na kuingia mwaka wa nne wa uongozi wa Dk Magufuli ni Profesa Jumanne Maghembe aliyeteuliwa baadaye kujaza nafasi ya uwaziri wa maliasili na utalii. Mawaziri wengine waliong’olewa katika nafasi zao ni George Simbachamwene aliyekuwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora.
Wengine waliong’olewa ni Mwigulu Nchemba aliyeanza na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kabla ya kuhamishiwa Wizara ya Mambo ya Ndani, baada ya Charles Kitwanga aliyekuwa akiishikilia kuondolewa.
Mawaziri ambao walianza kushika nyadhifa zao na hadi leo bado wanazishikilia na wizara zao kwenye mabano ni Ummy Mwalimu (Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto),William Lukuvi, (Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi), January Makamba (Waziri wa Nchi ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira), Jonista Mhagama (Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu), Dk Augustino Mahiga (Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa), Dk Hussein Mwinyi (Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa).
Mawaziri wafuatao wametimiza miaka mitatu ndani ya serikali ya Magufuli lakini wamebadilishiwa wizara, hao ni Dk Harisson Mwakyembe ambaye alikuwa wizara ya katiba na sheria na sasa yupo Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Profesa Mbarawa ambaye alianza na Wizara ya Maji na Umwagiliaji, akapelekwa Wizara ya Mawasiliano na uchukuzi lakini sasa karejeshwa Wizara ya Maji.
Hawa wafuatao walianza wakiwa manaibu waziri lakini sasa ni mawaziri kamili; Dk Hamisi Kingwangalla alianza na unaibu wizara ya afya, sasa ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Luhaga Mpina alianza kuwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais sasa ni Waziri wa Mifugo.
Wengine ni Isack Kamwela alianza kuwa Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, sasa ni Waziri wa Uchukuzi, Mawasiliano na Ujenzi na Suleiman Jafo alianza kuwa Naibu waziri, Ofisi ya Rais Tamisemi sasa ni waziri wa wizara hiyo.
Waliopoteza uwaziri ni Profesa Sospeter Muhongo (Madini), Charles Kitwanga (Ndani), Nape Nnauye (Habari,) Profesa Jumanne Maghembe (Maliasili na Charles Mwijage (Viwanda, Biashara).
Kwa upande wa utawala, panguapangua na tumbuatumbua ya mawaziri ni kati ya matukio ambayo hayatasahaulika kwa mwaka uliopita.
UTEKAJI
Tukio kubwa lililotikisa nchi ni la kutekwa kwa mfanyabiashara maarufu Tanzania, Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’, lakini wapo watu wengine walipatwa na masaibu hayo na kusababisha hofu kubwa kwa jamii.
Watoto kadhaa walitekwa na wengine kupatikana kwenye mazingira ya kutatanisha huku yule wa Tegeta jijini Dar, Idrissa Ally (13) akiwa hajulikani alipo mpaka leo.
AJALI NA VIFO
Ajali kubwa kuliko zote zilizotokea nchini kwa mwaka 2018 ni ile ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere katika eneo la Ukara ndani ya Ziwa Victoria wilayani Ukerewe na watu 224 walifariki dunia.
Kwa upande wa barabarani zimetokea ajali nyingi zilizohusisha magari ya serikali na yale ya watu binafsi na kusababisha vifo vya watu wengi.
VIONGOZI KUTUPWA GEREZANI
Mwaka 2018 umeisha huku Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko wakiwa gerezani baada ya kunyimwa dhamana ya kesi ya jinai inayowakabili wao na viongozi wengine wa Chadema, Katibu Mkuu, Vincent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara, John Mnyika, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya.
Mwaka wa 2018 pia ulikuwa mchungu kwa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ambaye mwezi Februari alifungwa gerezani miezi mitano baada ya kupatikana na hatia ya kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli