Hawa watu walijitolea kufa kwa ajili ya Tanzania lakini Tanzania ya ccm imekosa ubinadamu juu yao.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hawa watu walijitolea kufa kwa ajili ya Tanzania lakini Tanzania ya ccm imekosa ubinadamu juu yao..

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by figganigga, Dec 5, 2011.

 1. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #1
  Dec 5, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Salum Ally ama ukipenda kwa jina maarufu kwa jijini Dar es Salaam na katika baadhi ya mikoa ambayo hufanyia shughuli zake ni (Mzee Cuf), huyu yeye ni Mpiga picha maarufu wa picha za kuuza al-maarufu kama Picha za Banyaa.


  Picha za Banyaa ni zile picha zinazopigwa katika shughuli yeyote ikiwa ni Mkutano ama sherehe bila mpigwaji kuwa na mkataba na mpigaji na kisha huletewa picha ikiwa tayari na kuuziwa.

  Mzee Cuf, aliyewahi kushiriki katika mchakato wa kumuondoa Nduli Idd Amin Dada katika Mipaka ya Tanzania, mwaka 1978, anasema kuwa pamoja na kuwa mkakamavu kutokana na kuwahi kuwa 'Mjeda' Afande wa Jeshi la JWTZ na kushiriki Vita ya Kagera lakini bado anaamini hatua kubwa ya maisha yake imetokana na Kamera ambayo hadi hii leo anaitumia kwa kupiga picha za Banyaa na kumwezesha kujipatia kipato chake cha kila siku cha kuitunza familia yake pamoja na matumizi ya kawaida yanayohitajika katika familia. sasa serikali ya kikwete inashindwa nini kumfanya awe mpiga picha wa Ikulu? RUSHWA, UBADHILIFU NA UPENDELEO ndio unao imung'unya na kuitafuna serikali ya ccm chini ya Rais Jakaya Murisho Kikwete na wale walio mtangulia. Mafao mumewanyima hata kazi ya kupiga picha mnawanyima..??.


  Kwa mujibu wa Mzee Cuf mwenyewe, alishiriki katika Vita ya Kagera akiwa katika Kikosi cha Kakunyu No, 824 kilichokuwa chini ya Captain Alenguya.
  [​IMG]
  Mzee Cuf, akipozi kwa picha na kamera yake akiwa katika moja ya hafla za Kitaifa miaka ya nyuma, (kulia) ni Mpiga picha wa Waziri Mkuu wa sasa, Hirary Bujiku.
  [​IMG]
  Mzee Cuf akiwa katika moja ya pori wakati akiwa katika Vita ya Kagera, kwa mujibu wa Mzee Cuf ilikuwa ni Agost 24, 1978.
  [​IMG]
  Mzee Cuf (kulia) akiwa na mwenzake, wakiwa katika harakati za vita ya Kagera, 1978. Ccm be smart bana.. MIA
   
 2. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #2
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  mtakufa mumesimama na tai shingoni. mia
   
 3. Humphnicky

  Humphnicky JF-Expert Member

  #3
  Dec 6, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 1,808
  Likes Received: 524
  Trophy Points: 280
  Kina Moris Nyunyusa wamekufa wakiwa hohe hae wa kutupwa, huku TBC ikitumia midundo yake ya ngoma bila kumpa hata shilingi moja.
   
 4. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #4
  Dec 10, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  hii nchi isha halibika. isha kua ni nchi ya watu fulani, kabila fulani. kama wewe huna mtandao kupata kazi ni ndoto na siku zote wanaopata kazi ni wale ambao hawana hata taluma. inasikitisha sana. Mia
   
Loading...