kumekuwepo na mijadala mingi katika mitandao ya kijamii ikiwemo hapa jf ambayo Mara nyingi huhusisha kushambuliana kwa tuhuma mbalimbali nyingi zikihusisha ni Chama au vyama gani vya Siasa vinavyofuga au kuwa na viongozi mafisadi na wala rushwa. kila upande huwa unajitetea kwa kutupa lawama upande wa Chama kingine. sasa naomba tutumie hili sakata la wajumbe wa kamati mbalimbali za bunge kupata ukweli japo kidogo kuwa wanaotuhumiwa hasa ni wa chama gani cha Siasa? na je Chama hicho na wanachama wake waendelee kujinasibu kuwa Chama chao kina viongozi na wanachama wasafi?