Hawa ndio wabaya wa Lowassa


nyerere mwenyewe alishangaa lowasa anaupatia wapi utajiri wake.....hiyo haina maana kuwa hakuwa na taarifa bali ni wanajua ila huwezi ongea kila kitu....
je kama anauza tigo,huoni itakuwa kumuabisha kutamka wazi?
 
Very fan, kwamba hawajui utajiri katoa wapi, akiamia upinzani, utasikia mengi vyanzo vyote vitawekwa bayana
Nchi hii inasifika kwa upelelezi toka nikiwa mtt nasikia haya, sasa wameshindwa vipi kumchunguza, au kumchunguza ni kujichunguza
 
Hizi taarifa ambazo wanadai mwenyekiti anazo juu ya mtu huyu ni taarifa gani?
 



Ndio maana hapo juu kwenye maelezo ya Mkapa kasema "Tunajua mambo mengi, mengine hatuwezi kuyataja"

Ni pamoja na hayoo ya utajiri wa Lowassa!
 
Hizi taarifa ambazo wanadai mwenyekiti anazo juu ya mtu huyu ni taarifa gani?



Haswaa! Hili ndio swali la msingi la kujiuliza...!

Na sidhani kama watasema, maana Mkapa kasema "Tunajua vitu vingi, na vingine hatuwezi kuvitaja"
 
Uliona wapi waziri mkuu akawa rais wa nchi? Mkae mkijua Edo ahami chama ng'o!! Hata kwa mnyororo hatoki!!
 
Uliona wapi waziri mkuu akawa rais wa nchi? Mkae mkijua Edo ahami chama ng'o!! Hata kwa mnyororo hatoki!!

So hiyo ndio sababu? Rais wa sasa wa Russia ashawahi kuwa waziri mkuu
 
Aisee only in Tanzania......yaani kama kweli TISS walipendekeza jina la Lowassa likatwe kisa ni fisadi au JK anajua ni fisadi then wakupigwa mawe ni JK na TISS
 
TISS hawajui kuwa JK anamiliki makampuni ya mafuta kupitia Rizone? Hawajui kuwa kajenga maghorofa lukuki kupitia rizone? Wasitutie kichefuchefu hapa
 
Wamteteao Lowasa wote ni hamnazo.Haıkuhitajika hata taarıfa ya TISS kubainı kuwa n hatarı kwa maslai mapana ya taifa.

Kama ni hatari kwanini ameachwa siku zoote hizo ?! Siangekuwa jela ! Ni wivuu tuu.
 

Ulimwengu tulio nao hivi sasa ni wa ukweli,uwazi na kidemokrasia zaidi. Zile enzi za kuaminishwa na kuimba zidumu fikra za mtu umepitwa na wakati. Sawa m/kiti anazo siri nyingi ni vizuri na kidemokraksia zaidi zikawekwa wazi kwa wajumbe wengine. Na yeye si ameambiwa au kuandikiwa? Unajuaje aliekwambia/kukuandikia kafanya hivyo kwa malengo mabaya ya kuchafulia mtu sifa baada ya kukosa toka kwake hiki au kile? Unapoweka mezani hayo unayoyaona ni mabaya wenzio watatafakari uwezekano wa hayo kufanywa na anaejadiliwa. Ikibidi mhusika anaweza kuitwa na kujulishwa pengine akawa na maelezo mazuri. Kungangania tu heshima ya m/kiti na heshima ya kiti haitoshi ulimwengu wa sasa usio na siri. MSISAHAU UMDHANIAE NDIYE KUMBE SIYE NA UMDHANIAE SIE NDIE.
 

Wazo zuri sana kaka, ila hilo ni rahisi kufanyika katika medani ya sheria kuliko siasa.

Maamuzi ya kisiasa yanazongwa na sababu ambazo ni zaidi ya uhalisia. Nafikiri hii ni kwa nchi nyingi. Imeshafanyika hapa kwetu sio mara moja wala mbili. Ila kutokana na utandawazi na uwezo wa kupashana habari basi huonekana ni jipya. Naamimi maamuzi ambayo amefanyia edo si ya kwanza na yeye hatakuwa wa mwisho
 
lowasa akipitia hii thread sijui hali yake itakuwaje...

mwacheni kdg hadi atoe tamko lake..
 
Lakini hao hawakuwemo kwenye orodha ya watia nia, wangalikuwemo tungaliwata majina yao. Tathimini hufanyika kabla ya kupitishwa siyo baada wala hujatia nia. Kabla ya EL kuomba kupitishwa na CCM kuwa mgombea wa urais mbona hatukumgusa kwa sababu alikuwa anajiwakilisha mwenyewe na mkewe, sasa anataka kutuwakilisha sisi sote, lakini sisi siyo mafisadi tutawakilishwaje na fisadi. Tanzania hii mafisadi ni wachache kuliko wasiokuwa mafisadi. Kundi dogo wa watu litawakilishaje kundi kubwa?
Kiwete ni fisadi no 1,rz 1 utajiri wake hauelezeki wote majambazi wasitudanganye kw wao ni wasafi H M, B M, ssm if tu Haina masilahi kwa tz ife
 
Hakutendewa haki. Jina lake lingeletwa mbele ya Kamati, wamhoji, wamwambia mabaya yake, halaf ndo wamkate. Lakini hiyo ya mtu kutembea na majina yake matano mfukoni ndo nini?
Kwani alikatwa pekee yake, amekatwa PM na VP, who is Mamvi by then! Shida ni nyie wapambe mlijiandaa sana kugawana keki ya nchi.
 
Hizi taarifa ambazo wanadai mwenyekiti anazo juu ya mtu huyu ni taarifa gani?

Hukuna haja ya kumdhalilisha zaidi, kumkata inatosha, akitaka kuleta za kuleta ndio kila kitu kitawekwa hadharani
 
hawa watu wa pwani mbona wamemwandama sana lowasa???
nyerere alifanya kosa kubwa sana kumwamin mwinyi kushika uongozi.
sipendezw hata kidogo na jinsi wanavyomsakama lowasa kwan kikwete ni jambaz namba moja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…