“Hauko sawa !!!”, “ Unataka Kuwa Sawa!!!”

KANOSAWA

Member
Joined
Sep 16, 2016
Posts
55
Reaction score
39
NDOA
MAHUSIANO YA NDOA
- HIVII, NDOA NI NINI HASA ?!!!
Ndoa ni tendo la kujamiana baina ya jinsia mbili ya kike na kiume katika mahusiano halali baina ya jinsia mbili hizo, kwa kibali cha wazazi wao na baraka za dini zao au serikali.

- MAHUSIANO HUANZAJE ?
Mahusianao hayo huanza na mvuto wa upendo aliouweka Mwenyezi Mungu, ndani ya nafsi zao. Inatokea mmoja anampenda mwenzie,au wote wanapendana kwa kutamaniana; hali hiyo hutokeza urafiki baina yao.
Baadae urafiki huo hupelekea hao wawili kuchumbiana, ambapo ndipo wazazi wa pande zote mbili huhusika kutoa kibali cha hao kuoana.
Baada ya ya hatua ya mahari kulipwa, jamii hujulishwa na hatimaye zoezi huwa likakamilishwa kwa Baraka za kidini au kiserikali, kwa maana nyingine hizo taasisi za dini au serikali hutoa hati au cheti cha ndoa kuhalalisha kujamiana kwa wawili hao.

- HARUSI AU SHEREHE YA NDOA
Kwa kuwa zoezi loote tangu mahusiano ya kirafiki mpaka cheti cha ndoa huwa ni la furaha basi huambatana na shamra shamra kama vile Kitchen Party au sherehe ya kumfunda mwali au biharusi; Send off au sherehe ya kumuaga biharusi na hatimaye Harusi yenyewe au sherehe ya ndoa ambayo ndo siku ya kupewa hati au cheti cha ndoa ambayo pia huitwa siku ya kufunga ndoa.

- MASHAKA YA NDOA
Dhamira ndani ya nafsi ndiye hakimu mkuu mwenye haki. Na dhamira ni msemakweli. Hivyo basi kama wawili wanaishi pamoja na hatua nilizoziainisha hazikufuatwa, kila mmoja anaendelea kuugua moyoni na kwa kuwa maumivu daima hutafutiwa dawa, hufikia wawili hawa kutafuta kuijibu dhamira kwa kutafuta taratibu zifuatwe hata kama imewachukuwa wawili hao kuishi muda mrefu pamoja, pengine hata kupata watoto.
Ndiyo maana hatushangai siku hizi mtu anafunga ndoa hali ana wajukuu. Lengo huwa ni kutafuta mwarobaini wa dhamira inayomsuta kila kukicha.

- AJALI ZA MAHUSIANO / KUISHI PASIPO NDOA
Wengine hutokea kuishi kama wanandoa kutokana na sheria za lazima za serikali. Mfano, mtumishi mahali fulani anataka kuongezwa cheo au hatua fulani, wanamwambia ni lazima awe ameoa. Hivyo hupelekea yule mtumishi au mfanyakazi kuoa, au kuolewa, kisha wanendelea kuishi pasipo kufunga ndoa.
Wengine hutokea wamefanya tendo la kujamiana kwa matamanio tu na ikatokea huyo binti au mama kupata ujauzito. Hivyo inakuwa lazima aolewe na huyo mwenza. Na wanaoana bila ndoa.
Wengine wanakutana baa, au safarini au kazini na wanaanzisha mahusiano ya kuishi pamoja, yaani wanaoana pasipo ndoa.
Wengine mila zinawalazimisha baada ya kukutwa wakijamiana au kuhisiwa wakijamiana, hivyo hupelekea kuwalazimisha kuoana pasipo ndoa na wakati mwingine huitwa ndoa ya mkeka.
Wengine hutokea wakahusiana kupitia mitandao kama ya Facebook, Twitter n.k na wakaishi pamoja pasipo ndoa.
Wengine wanaishi maisha ya upweke lakini kiukweli wana wake au waume wao kwa siri, kwa maana hiyo wameoana pasipo ndoa.
Wengine na wengine na wengine namna hiyo. Hizo zoote naziita Ajali za Mahusiano.

- NDOA AU AJALI ZA MAHUSIANO
Swali ni kwamba je woote tunaoishi katika mahusiano, je uko eneo gani kati ya haya mawili.
1. Mahusiano ya Ndoa ??
2. Ajali za mahusiano ??

- ASILI YA NDOA
Siku ile Mungu alipo tamka neno la ‘Zaeni, mkaongezeke’;
Mwanzo 1:28
28Mungu akawabariki na akawaambia,“Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze tena nchi, na kuitiisha, mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.’

ndipo ndoa ilipoanzishwa kwa viumbe woote kwa utaratibu aliojiwekea Mungu mwenyewe. Na utaratibu huo Mungu aliuzamisha ndani ya nafsi zetu, hutawaliwa na kitu kinaitwa Dhamira. Ndiyo maana ukiwa kinyume na utaratibu wa Mungu, hata bila kuambiwa na mtu yeyote, nafsi inakusuta tundani kwa ndani kuwa, hauko sawa !!!!

Ndipo ninapo kuja na makala hii, kukuamsha kuwa tutajaliwa kuingia mwaka 2017 hivi punde; kama nafsi yako inasema “Hauko sawa !!!”, nakushauri na ninakuomba ujichunguze, kwa sababu hiyo ni sauti ya Mungu mwenyewe inazungumza ndani yako. Jipange na weka nadhiri au ahadi kwa Mungu kuwa “ Unataka Kuwa Sawa!!!”

NINAKUOMBEA MUNGU AKUTIE NGUVU, 2016 UIVUKE NA UWEKE MAMBO SAWA 2017.
 
Back
Top Bottom