Haujakaa Uswazi!!!

* Kama hujawahi kumuona Albino (Zeruzeru) ukajitemea mate mwilini ! (eti usipofanya hivyo nawe utakua kama yeye!)
* Kama hujawahi ng'oa jino ukamtupia Kunguru ukisema "Kunguru chukua jino lako bovu unipe zima"
* Kama hujaogopa kutembelea karibu ya nyumba zilizokua zimejengwa mbali ya zingine (nyumba iliyojitenga na imezungukwa aidha na miti au vinginevyo iliitwa ya mumiani , mnyonya damu)
* Kama hukucheza kachiri saga!
* Kama hukua captain wa timu ya mtaani, wenzio wakachanga pesa mnunue gozi (mpira) na wewe ndiyo muhazini ukala pesa ya timu! Na ulaji wenyewe wa pesa sanasana hua ni mishkaki, ice cream, maembe, maandazi, kashata n.k.
 
Hiyo ya arnold ya jini terminator imenibidi ni cheke kwanza.Massawe bill blanks ndo umenikumbusha huko
 
au kuchamba kwa kukaa chini na kujiparuria kwenye mchanga

Saas, tumekubambika wewe haya yote.

Utakuwa wa Tabora wewe
Kama hujawahi kuchamba kwa kutumia gunzi la hindi au ukuta basi wewe bado
 
Last edited by a moderator:
Kama ujawai kuwa na njiwa chokichoki na sonara
Kama ujawai paisha kishada
Kama ujawai cheza kula mbakishie baba
Kama ujaangua maembe
Kama ujanywa togwa,kula visheti na ubuyo shuleni
Kama ujawai kula aiskrim kijiti chelewa
Kama ujatengeneza magari kwa madebe na matairi ya ndalankuwinda ndege na manati
 
kama hujawah kuchezesha joyce wowowo na kupata cent
kama hujawah kucheza ki-bruslee huu haa
kama hujawah chezesha sinema 6a mabuksi nyuma kibatari,
kama hujawah kucheza nilonge, nisilonge,
kama hujawah kuiba kopo la kujitawazia ukatengenezea magari, dah longi sana
 
aisee The Finest,
Hiyo ya Mniga kuliwa na mamba the Hard way nimeipenda. Umenikumbusha mbali kweli yani.
 
kama haujachoma wenzio na mbegu za ubuyu baada ya kuzisugua chini class.
 
Kufuga samaki wa urembo!!!gapi,teksido!red!zebra!tambara!gold!mkasi!black more n.k!!!!njiwa kama sanaa,fungo,choki,kombokombo,kwankwaruu,kwankwaruu kisoda,choki matepe!!!!!!.......
 
....ni noumer....
..kama hujawahi goma kwenda church kwa kutonunuliwa nguo za skukuu....
...kama hujajifunza vuta sigara kwa kusokota karatasi....

kaka unalijua gosho!??basi ile mtoto anaweza akafa akijaribu iga dingi yake anapiga marlboro!!piga sana yale ma-kitu aisee!
 
da kwa ujumla mwanzisha thread katukumbusha mbaliii....enzi za trela loketo, bongo man, madilu system, yondo sister..kama hujaenda kutembea sikukuu na kikundi cha watoto wenzio halafu wewe ndo kiongozi wao...mnanunua miguu ya kuku,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…