Hatutawavumilia wanaopinga Muungano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatutawavumilia wanaopinga Muungano

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Apr 22, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Apr 22, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=1][/h]Posted on April 21, 2012 by zanzibaryetu
  [​IMG]Kundi la watu wanaotaka kuitishwa kura ya maoni kuamuliwa juu ya Muungano uwepo au usiwepo wakiwa katika viwanja vya baraza la wawakilishi

  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema haitawavumilia wanaharakati au kikundi chochote kinatakachohatarisha amani kwa kisingizio cha kupinga Muungano wa Zanzibar na Tanganyika kwa kutumia mihadhara na makongamano. Hayo yameelezwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi wakati akifunga kikao cha Baraza la Wawakilishi kilichomalizika juzi huko Chukwani Mjini hapa.
  Balozi Seif alisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar haitaki kupoteza amani na utulivu na kurejea katika vurugu na uhasama uliojengeka katika jamii kwa maika kadhaa. Napenda niweke wazi msimamo wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar haitakivumilia kikundi chochote kitakachoonekana kuhatarisha amani, utulivu na umoja wa wananchi wetu” alisema Balozi Seif.
  Alisema serikali haiku tayari kurudishwa nyuma ambako wananchi waliishi kwa khofu kubwa huku chuki na uhasama zikiwa zimetanda miongoni mwao.
  “Hatutasita kuvizuwia vikundi vyovyote vinavyoendesha mihadhara au makongamano tutakayobaini yanahataridha usalama wan chi yetu. Na hili hatutakuwa na muhali na mtu yeyote Yule” alisema Balozi Seif wakati wa kufunga baraza.
  Alisema kuna kikundi cha watu wachache wanaoendesha makongamano kwa lengo la kuwakashfu na kuwatukana viongozi, badala ya kutumia jukwaa hilo kwa shughuli za uelimishaji.
  Alisema lengo la serikali zote mbili ni kuona watu wanajitokeza katika tume iliyoundwa na Rais Kikwete kwenda kutoa maoni juu ya katiba na sio kutumia majukwaa kwa kuwapotosha watu na kupinga Muungano.
  Alisema masuala ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yana nafasi yake ya kujadiliwa na kwamba wanaotaka kufanya hivyo fursa hiyo wataipata kupitia mchakato ujao wa kukusanya maoni kuhusu mabadiliko ya katiba.
  Alisema awali waliamini kwamba wanaoendesha makongamano hayo wana nia njema ya kutoa elimu kwa umma lakini badala yake wamekwua wakitumia makongamano na mihadhara hiyo kwa kuwakashifu viongozi, kejeli na matusi kwa viongozi na watu wenye kuunga mkono Muungano.
  Kauli ya Makamu wa Pili wa Rais, imekuja wakati tayari wanaharakati wanaopinga Muungano na wanaotaka kuitishe kura ya maoni ya kuwauliza wazanzibari iwapo wanataka kuendelea na Muungano uliopo au hawautaki wamo katika mikono ya jeshi la polisi baada ya kushikiliwa hapo juzi katika viwanja vya baraza la wawakilishi.
  Wanaharakati hao 12 juzi walikamatwa na jeshi la polisi baada ya kudaiwa kukataa kutii amri halali ya jeshi hilo mbele ya viwanja vya baraza hilo kabla ya kuonana na Spika wa baraza hilo, Pandu Ameir Kificho ambaye walitaka kumuelezea lengo lao la kufika hapo.
  Kwa mujibu wa barua yao waliomuandikia Spika Kificho, na kutiwa saini na kiongozi wa kundi hilo, Rashid Salum Adiy ilisema wazanzibari wana haki ya kikatiba kudai uhuru wa Zanzibar na hivyo wanachotaka ni kuitetea nchi yao kwa mujibu wa sheria zilizopo ambapo.
  Akizungumza na waandishi wa habari, Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa alikiri kwamba wanaharakati hao walipanga kumwona Spika kwa lengo la kushinikiza baraza lipitishe uzimio kuruhusu wazanzibari kupiga kura ya maoni ya kuukataa au kuukubali Muungano.
  Kamishna Mussa alisema sio tatizo wananchi kudai haki hiyo ya kura ya maoni lakini kinachotakiwa ni kufuata taratibu na sheria za kuweza kufika katika viwanja hivyo vya baraza la wawakilishi na sio kwenda bila ya taratibu.
  “Sio shida wananchi kwenda pale lakini napenda watambue kwamba Baraza la Wawakilishi sio viwanja vya sikukuu, kama kila mtu anaweza kwenda tu na kusherehekea” alisema Kamishna huyo.
  Alisema watub wanaweza kudai haki zao bila ya kuvunja sheria na jeshi la polisi limejipanga kukabiliana na vitendo vyote viovu na vyenye kuhatarisha amani ya nchi.
  Aidha alisema wananchi wanaodai kuukataa Muungano wanaweza kufanya hivyo kwa kufuata taratibu na wale wenye kuunga mkono Muungano pia wanaweza kufanya hivyo lakini kwa kufuata misingi ya sheria zilizopo na jeshi lake halitamvumilia mtu ambaye anakiuka sheria kwa kisingizio kama hicho.
  “Wanaopinga Muungano wanaweza kupinga lakini kwa kufuata taratibu maalumu na sheria na wale wenye kutaka Muungano pia wanaweza kuunga mkono lakini kama hatuwezi kuwaachia wneye kupinga kwa kusababisha fujo na hivyo hivyo hatuwezi kuwaruhusu wenye kuunga mkono kwa furaha zao wakenda uchi eti kwa sababu wanaunga mkono…lazima sheria na shuruti zitimizwe na sisi tupo hapa kwa ajili ya kuwashurutisha wale wasiotaka kufuata shuruti” alisema Kamishna Mussa.
  Uchunguzi wa Gazeti hili umegundua kwamba tayari wanaharakati hao wameshahojiwa na jeshi la polisi ambapo baadhi yao walikataa kutoa maelezo akiwemo kiongozi wa kundi hilo hadi hapo wakili wao atakapofika kituoni.
   
 2. m

  mzaire JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwambie huyo Sefu Idi awaachie wazenji waamue wenyewe asiwatishe, hamuoni dr. salmini yaliyompata??
   
 3. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #3
  Apr 22, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,273
  Trophy Points: 280
  Hili usivunjike twambie faida zake na hasara zake ndo tuone kama unamuhimu au lah.
   
 4. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #4
  Apr 22, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,957
  Likes Received: 1,283
  Trophy Points: 280
  vunja tu. Mi Mtanganyika naona hasara tu.
   
 5. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #5
  Apr 22, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Mkuu kakke, mbona wao wamewavumilia nyinyi mnaopenda muungano kwa miaka chungu nzima, mnashindwaje nanyi kuwavumilia wanaoupinga?
   
 6. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #6
  Apr 22, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mimi ni MTANGANYIKA. Kuzuia watu kuhoji juu ya muungano ni upuuzi, ni solution ya muda mfupi.
   
 7. M

  Mwanantala Senior Member

  #7
  Apr 22, 2012
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 120
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Serikali zetu zimeshindwa kuonyesha umuhimu wa muungano kwa vitendo. Inaelekea muungano unatumiwa kwa faida ya viongozi wachache wa visiwani kupandikizwa na wabara. Ni heri uvunjike.
   
 8. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #8
  Apr 22, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Wangeacha wananchi tuamue wenyewe mustakbali wetu kukataza ndio wanatupa wasi wasi!
   
 9. n

  n.ngereja Member

  #9
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  muungano kichefuchefu
   
 10. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #10
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Sijui hadi lini waheshimiwa wataendelea kuulinda huu muungano, labda kwa kuwa ni kwa gharama za wadanganyika.
  Na kama waking'ang'ania huu muungano tutaweka katika katiba uraisi wa mpokezano. hapo naona watauvunja wenyewe watake wasitake.
   
 11. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #11
  Apr 22, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Unanilazimisha ndoa ambayo siiitaki
   
 12. ITEGAMATWI

  ITEGAMATWI JF-Expert Member

  #12
  Apr 22, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 4,223
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Mimi ni Mtanganyika,Lakini kwa nguvu zote naunga mkono kuwa suala la muungano lirudishwe kwa wananchi waamue hatima yake,kuendelea kuwazuia siyo suluhisho endelevu!Kama wengi hawautaki na uvunjwe tu wala siyo wakwanza sisi kuvunja muungano,ilikuwepo USSR ikafa kifo cha mende sembuse Tanzania?
   
 13. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #13
  Apr 22, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Muungano basiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
   
 14. m

  mtalii1 Member

  #14
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  i like
   
 15. C

  CHIEF MVUNGI Senior Member

  #15
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mi mtanganyika nko Zanzibar naomba muungano ufe kwani wazanzibar wananyonywa bora ufe amkeni wazenji kama mnataka muungano ufe chagua chama pinzani muue CCM kwanza.
   
 16. k

  karafuu Member

  #16
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hakuna haja ya kutoa vitisho kwa wananchi,hao ndio wadau wakubwa wa maamuzi na ndio wenye mamlaka ya mwisho basi tukubali matokeo tuu viongozi,hizo propaganda za kutukanwa viongozi si hoja yenye mashiko.
   
 17. Vijijini Lawama

  Vijijini Lawama JF-Expert Member

  #17
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 300
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  In this world you can not full people all the time!!! Hvi muungano ni wa viongozi tu tena wa CCm na familia zao au wananchi?
   
 18. m

  mwarain Member

  #18
  Apr 22, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acheni wananchi watoe maoni yao kuhusu muungano kwa uhuru kama katiba inavyoelekeza. Na huyo makamu wa Rais anaposema watajadili suala hilo kwenye marekebisho ya katiba anawatia mchanga wa macho ikizingatiwa mimi kwa masikio yangu JK akisema suala la muungano kuwepo au kutokuwepo HALITAJADILIWA kwenye huu mchakato!
  Viongozi hii nchi ni ya wote ITISHENI REFERENDUM!!!!!
   
Loading...