Hatutaki vita Tz

Hatutaki vita Tz

Egwugu

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2011
Posts
17,558
Reaction score
8,552
Lowassa kutangaza majeshi yetu yako tayari wakati wa sakata la ziwa Nyasa na wakati waziri wa mambo ya nje yupo, wakati waziri wa ulinzi yupo, wakati rais yupo ni jambo amabalo linaongea zaidi na hasa juu ya uwezo wa mhusika. Tena nichukue nafasi hii kumpongeza Membe kuweza kusettle disputes zile na rais Kikwete, kwa Mara ya kwanza naona umuhimu wa vipngozi hawa na inanifanya nijiulize ingelikuwaje Lowasa angelikuwa ndo mkuu wa majeshi ama amiri jeshi mkuu? nchi haiitaji mihemko, Ikulu ni sehemu nyeti ya kufanya maamuzi na ni sehemu ya kuleta maelewano ndani na nje, hatuwezi kuwa na rais wa kusema piga basi watu wanapiga, wakija wahuni wakamwambia piga hao na yeye akapiga itakuwaje? Ikulu hatuwezi kupeleka mtu kama kumpa zawadi, hatuwezi kumpeleka mtu Ikulu kana kwamba tumekosa mtu, urais siyo zawadi wala si harusi, urais ni kazi na kazi inahitaji mtu aliye tayari kiakiri na kimwili nje ya hapo tuachane na kuwaweka watu kama zawadi, kama ni zawadi mpelekeni shopping mkampige viwalo ama mpelekeni tour ili a enjoy ila Ikulu tupeleke wa kufanya kazi zetu na kuheshimu majirani bila mihemko.
 
Umepotea mkuu. Hayo unayoeleza hapa sio mahali pake. Nadhani unapoteza tu muda wako na nina imani watu wengi watakupuuza tu
 
Umepotea mkuu. Hayo unayoeleza hapa sio mahali pake. Nadhani unapoteza tu muda wako na nina imani watu wengi watakupuuza tu

Ukinipuuza wewe siyo mbaya kwasababu nilitaka kutoa dukuduku langu kama mtanzania ..ukiona vipi we ipotezee tu
 
Ngoja nikupuuzie tu, nadhani uko katika kipindi cha Hangover!
 
Ukinipuuza wewe siyo mbaya kwasababu nilitaka kutoa dukuduku langu kama mtanzania ..ukiona vipi we ipotezee tu

Ndio, nimeshakupuuza tyr. Si unaona watu hata hawachangii. Fanyeni kazi ya kumtangaza mgombea wenu basi Dr.Magufuli, ni mpweke sana. Kumsema Lowassa kila wkt mnatusaidia kufanya uenezi sisi UKAWA. Ushauri huu ni wa bure, siuzi. Ni vizuri ukauchukua mkuu
 
Kama bado unafanya kazi ya ccm umepotea ,pia ukumbuke sheria ni lazima ipindishwe kwa maslahi ya umma
 
Hata magufuli hana busara ana kauli chafu, alishawahi tuambia watu wa kigambon tupige mbizi...hizi ni kauli za mtu anayefaa kukaa ikulu kweli?
 
Njaa zinawasumbua kupe nyinyi wala hamlijuhi kosa lenu
 
Back
Top Bottom