Hatuna viongozi wa soka bongo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatuna viongozi wa soka bongo

Discussion in 'Sports' started by Kiduduye, Aug 1, 2012.

 1. K

  Kiduduye New Member

  #1
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 25, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Hapo ndo mtakapojua kuwa soka la bongo la majungu, kukomoana, fitina na chuki. Hivi mtu na akili yako kweli unadiriki kufanya ujinga kama huu aliofanyiwa Ngasa? hilo suala dunia nzima hakuna lipo tz tu, na kwa hali hii soka letu halitasogea milele. Mtu kama Geofrey kaburu mtu mwenye heshima zake hawezi kujiaibisha kiasi hiki umewahi kuona wapi mchezaji anauzwa tu kama nyanya au vitunguu vilivyo sokoni. Jambo la msingi ni kwamba pande zote 3 zinatakiwa zikae zikubaliane hapa namaanisha kwamba azam, simba na mrisho ngasa mwenyewe wafikie makubaliano na usajiri wake lakini cha ajabu viongozi wanafanya mkomoeni. Km leo mlisikia michezo ya clouds fm yule katibu wa azam anaongea kama kaladhimisha vile nadhani kisa ni mrisho ngassa kuibusu logo ya yanga, sawa kimichezo ngassa kafanya kosa lakini walitakiwa wamuonye au apewe adhabu kulingana na vifungu vya sheria. Ulishawahi kusikia wapi duniani eti mtu anauzwa kwa mkopo wa pesa kiasi kweli jamani mm naona kuna njama fulani hapa inafanyika ili kumuharibu ngassa kisaikolojia, hata kama ningekuwa ni ndo mchezaji nisingekubali kamwe kulazimishwa kufanya maamuzi hayo cha msingi kama mmeona ngassa hamumtaki tena mnavunja mkataba na mnamlipa pesa yake anakuwa huru kucheza timu yoyote anayoitaka, siyo kwamba eti kisa anaipenda yanga ndo akatae hapana hata kama angekuwa kapelekwa yanga kwa staili kama hii sidhani kama angekubali. Jambo la msingi hapa wadau ni kusapoti vitu vinavyoeleweka na sio unafiki tu eti kisa unaipenda simba ndo usapoti ujinga nakataa katakata. Azam muacheni ngassa afanye maamuzi yeye kama yeye, si mmesikia leo Daniel Agger liverpool wamekubali ofa ya west ham pn mil 19 lakini mchezaji kagoma huo ndo msimamo. Big up kwa wanangu mliogoma kupelekwa kwa mkopo Shamte ally, ramadhani chombo redondo huo ndo ushujaa mohamed banka. Nitashangaa sana kama ngassa akikubali kuchezea simba.
   
 2. B

  Baba Kiki JF-Expert Member

  #2
  Aug 2, 2012
  Joined: May 31, 2012
  Messages: 1,368
  Likes Received: 489
  Trophy Points: 180
  Lakini kuna vitu vya kuangalia hapa. Ngasa kwa sasa yuko wapi? Yuko klabuni kwake kama wachezaji wenzake au yuko ktk klabu nyingine? Na hizi taarifa zilizozagaa kuwa baada ya mechi ya fainali ya Kagame kuwa Ngasa aliambatana na Yanga badala ya Azam, ni habari nzuri kwa nchi yetu inayotaka kujenga professionalism katka soka?

  Je! Kuibusu logo ya Yanga wakati anaitumikia azam lilikuwa ni jambo la busara? Ni wangapi katika nyie watoa maoni mliandika kukemea au tu kukosoa upuuzi ule?

  Azam wameamua kumweka sokoni mchezaji na kusisitiza nia ya kumuuza Yanga ambako ameonyesha mapenzi nako lakini hadi deadline ya bid inafungwa Yanga hawakuwa wameonesha hata ile kutaka ku-negotiate kupunguziwa au kulipa kwa installment fee ya ngasa. Mlitaka Azam wafanyeje? Wampeleke kwa nguvu Yanga?

  Nadhani kinachoanza ni mazungumzo ya klabu na klabu na kisha mazungumzo na mchezaji husika na sio kinyume chake. Huo ndio utaratibu na bado mchezaji anao uwezo wa kukataa kwenda Simba kama hataridhika na maslahi yake au hata mapenzi yake tu.

  Tusiwe tunahukumu upande mmoja tu kutokana na kufumbwa macho na upofu wa mapenzi ya vilabu vyetu na badala tuchambue mambo kwa kina na kuangalia mazingira yanayozunguka tukio.
   
 3. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #3
  Aug 2, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Baba Kiki nataka nikuambie kwanza hutakiwi kuamini sana hizi habari za haya magazeti ya kibongo ya kwamba sijui Ngassa afichwa Hotelini au vp,kabla ya kumhukumu Ngassa kuwa hakuandamana na team yake baada ya mchezo wa fainali ungefanya uchunguzi kwanza wachezaji wengine wa Azam baada ya mechi ile walikwenda wapi,je walirudi Kambini au walipewa ruhusa na kama walirudi Kambini Ngassa hakurudi Viongozi wa Azam walichukua hatua gani,manake taratibu za Kambi yeyote zinajulikana kama Ngassa alitoweka Kambini bila ruhusa walikuwa na haki ya kumchukulia hatua ksbb bado kisheria ni mchezaji wao regardless vitendo alivyovifanya vya kuonyesha mapenzi kwa team nyingine,wangeweza hata kumwadhibu kwa kumfungia.
  Kuibusu logo ya Yanga mimi sioni kama inaweza ikawa issue saana ya kuanzisha haya yote,wapo wachezaji wa Ulaya baada ya kuhama wameshawahi kuonyesha mapenzi yao kwa team zao za zamani walizozichezea kwa mafanikio akiwemo Thiery Henry sasa kwanini kwa Ngassa iwe tatizo la kugharimu kipaji cha mtu, Ngassa kuipenda Yanga hajaanza leo,inawezekana tokea utotoni labda kabla hata hajaanza kucheza soka la ushindani,Azam walimchukua Ngassa kutoka Yanga wakifahamu ana mapenzi na Yanga,lkn still bado aliwafanyia kazi ksbb Ngassa kama mtu mzima anajua kuwa mpira ndo kazi yake na hivyo despite mapenzi yake kwa sehemu fulani lkn anapaswa kuutumikia mkataba wake ipasavyo kitu ambacho amekuwa akikifanya kwa kipindi chote alichokuwa Azam,sasa point hapa ni kuwa kama wao wanafikiria kuna vitu alivyokosea ilikuwa ni kumuonya,kumuwekea utaratibu mpya wa kazi au hata kumwadhibu jambo ambalo nina uhakika lingemfunza zaidi kuliko mbinu wanayotaka kutumia kumkomoa.
  Point ya Simba kupanda dau zaidi ya Yanga,mimi nakuomba usiichukulie juujuu,unajua Yanga ndo walikuwa wa kwanza kubisha hodi Azam wakitaka kumchukua kwa mkopo,Azam wakakataa...Yanga wakataka waambiwe bei,still bado Azam wakagoma,wakasema hauzwi basi Yanga wakatulia,baada ya kuona mchezaji mwenyewe hawataki Azam wakatangaza bei US $ 50,000,ile hela Yanga wakaona kubwa,Azam wakawauliza Yanga wako tayari kutoa shing'api Yanga wakasema Mil 20,hapohapo Azam wakawasiliana na Simba wakawaambia offer ya Yanga,na wakawaambia wapande bei zaidi - yote ni katika kumkomoa Ngassa,Simba wakapanda Mil 25,Yanga wangefika 30,Simba wangepanda Mil 35...sasa biashara gani hiyo?
  Kihalisia kabisa hapa hakuna biashara iliyofanyika hapa ni ujanjaujanja wa kutaka kumkomoa mchezaji basi, hlf sasa walivyo wajinga wanajichanganya mara ni mkopo,mkopo gani wa ada ya uhamisho? na mshahara anapokelea team yake mpya,gazeti moja limemnukuu kuwa atakipiga kwa mkopo Simba miaka miwili,wakati mkataba wake kwa Azam ulibakisha mwaka mmoja...mkopo gani una'exceed duration ya mkataba,hivyo ndo wanavyokopesha Unga na Cola zao?
   
 4. M

  Masuke JF-Expert Member

  #4
  Aug 2, 2012
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Mimi nilishawahi kusema humu ndani Kaburu anahujumu timu yetu, kitendo cha kujumuisha jina la Yondani kwenye mashindano ya Kagame ilikuwa hujuma hata sasa kulipa hela kwa ajili ya Ngasa wakati hajaongea na Ngasa nayo ni hujuma pia, itabidi siku ya mkutano watueleze yote hayo.
   
 5. B

  Baba Kiki JF-Expert Member

  #5
  Aug 2, 2012
  Joined: May 31, 2012
  Messages: 1,368
  Likes Received: 489
  Trophy Points: 180
  Ndugu Anselm - nakubaliana na mazingira ya utata yanayozunguka swala hili. Lakini na wewe umetumbukia ktk shimo lilelile ambalo umenihukumu kwa kuamini habari za magazeti hasa pale unapodai kuwa Azam walikuwa wanawasiliana na Simba kila Yanga walipoweka dau. Nina wasiwasi na hili. Hata hivyo nakupongeza kwa kuweka argument zenye mashiko hasa unapodadisi duration of contract mara sijui mkopo n.k.

  Yetu macho, acha tuone sinema hii itakavyoisha maana Bongo haiishi vituko.
   
Loading...