Hatuko sawa, hata wanyama wanafahamu

Hatuko sawa, hata wanyama wanafahamu

Egwugu

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2011
Posts
17,558
Reaction score
8,551
Mungu alikuwa sahihi kumuumba mwanaume, na alikuwa sahihi pia kumuumba mwanamke. Alijua na ndo maana hata kimaumbile hawako sawa, hata kwa uwiano wa viungo vyao haviko sawa pia.

Lakini Mungu alienda mbali na akatofautisha hata upatikanaji wao, kuzaliwa hadi kukua hawako sawa kabisa kulingana na somo la biolojia. Mtoto wa kiume si mtoto wa kimchezo hadi ukamkuze unahitaji kujipanga, na ndo maana labda hata mahospitalini hawazaliwi sana na hata wakizaliwa vitoto vingi vya kiume vinaibiwa sana kulinganisha na wa kike.

Lakini Mungu alijua hata kwenye majukumu hawa watu hawako sawa, ni hasiri ya mwanamke kujipodoa na kutaka kuvutia. Si sehemu ya maisha ya mwanamke kupitia shuruba ila kutokana na maisha "wachache" wao hulazimika kujikakamua. Shuruba (kazi) saizi yake ni mwanaume na hilo linadhihirika hata misuli yao ilivyokaa, tizama mikono yao uone tofauti zao ...kwanini?

Sasa ajabu zaidi, eti tunaaminishwa tuko sawa. Haya ni maajabu ya ulimwengu huu uliofitinika, kibaya zaidi hata iweje, kilichoumbwa kitabakia vile vile hadi kurudi kwa Yesu. Kuna kitu kiliniacha hoi katika hili, kumbe hata wanyama nao wanalifahamu hili ijapo sie na madegree yetu hatuonekani kusadiki

Kuanzia Jogoo, Ngedere, Nyani, Beberu, Kondoo n.k vyote hivi vinamfahamu mtu jinsia ya kike na vinamdharau sana. Sielewi ni kwanini lakini ni viumbe ambao vikiamua, mwanamke hata aweje hawezi kuvitisha na havimwogopi. Vinamchukulia inferior sana tofauti na mwanaume hata kama ni katoto kadogo vinakatii. Sasa akina mama hawa wanaoonekana weak hata kwa viumbe wa hivi, mwanaume unakuwaje wewe unazidiwa uelewa na hawa wadudu? ni sawa na kusema hawa wadudu wana ufahamu mkubwa kuliko sie wanadamu

Kwa navyofikiri, endapo hawa wanyama wangelikuwa na uwezo wa kuongea basi wanaume tungekuwa na hari ngumu sana. Uenda wangediriki hata kutuchapa bakora hadi tujitambue kama wao wanavyotukubali. Kwamba mwanadamu wa kiume ni dhaifu na ana uelewa mdogo sana kuliko wanyama wengine wa kiume katika kujitambua na kuheshimu uumbaji wa aliyewaumba.
 
Hata Dr Magufuli si Sawa na mhe mbowe
Dunia inajua Magufuli ni mashine nyingine
 
Eti haki sawa hakuna haki sawa ni siasa tu hizo za wanasiasa......hata Mbinguni tu kwenyewe hakuna haki sawa ije kuwa duniani? Kwa nini huko kuna Malaika mkuu na wa kawaida
 
Eti haki sawa hakuna haki sawa ni siasa tu hizo za wanasiasa......hata Mbinguni tu kwenyewe hakuna haki sawa ije kuwa duniani? Kwa nini huko kuna Malaika mkuu na wa kawaida
Teh teh teh, mie nilikuwa nawaburudisha tu mkuu. Hivi niulize, ndo maana hata Lucifer alifukuzwa kwa vile alitaka usawa na Mungu eti? hakika kama ni kweli basi usawa halikuwa kusudio la Mungu. Sijui wanadamu sie tumelipata wapi wakati Mungu wetu mwenyewe alilinda mamlaka yake usiku na mchana hadi wa leo, na sijui Lucifer naye alidanganywa na nani kutaka kuwa sawa na aliyekuwa superior kwake
 
Ndo hapo sasa hakuna usawa kote duniani na mbinguni ndo maana Lucifer alifukuzwa eeh!
 
Hata wao wananijua ni viumbe dhaifu ndiyo maana wanadiriki hata kuvaa suruali ili angalau waonekane sawa na wanaume lakini thubutuuuu! Wanajidanganya.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom