Hatujui kwa mfano uhuru wa vyombo vya habari utaruhusiwa lini au ndo imetoka hivyo, hatujui bunge litarudishwa live au ndo kwa heri, hatujui vyama vya siasa vitaruhusiwa kufanya mikutano yake au ndo vimefutwa, hatujui kama utaribu wa kisheria wa kuwajibisha watumishi utarudishwa au tutafuata huu wa mkulu anaotaka.
Hatujui kama utaratibu wa kuendesha serikali kisheria utarudishwa au kila siku tutasubiri saa 2 taarifa ya habari kujua leo wale wakubwa wawili wametoa amri gani. Hatujui kama tutanunua sukari kama ilivyokuwa kwa kumtuma mtoto kwa Mangi au tutaendelea kupanga mstari kwenye maroli.
Hatujui utaratibu wa wizara kujipangia matumizi kama utarudi au tutafuata huu wa mkulu kuamka asubuhi akasema hizi nazipeleka huku?
Mfumo huu wa kuchanganyikiwa utaisha lini?